Kwahiyo Nawakaribisha Mueleze Wale Wote Mlotendwa Na Wachungaji,pia Pale Tag Magomeni Mnakumbuka Yule Mch.Aliyefumwa Na Mume Wa Mchumba Ambae Alikuta Sms Za Mchungaji Kwenye Sm Ya Mchumba Wake Za Mapenzi Akimtongoza Na Kijana Kuzipeleka Baraza La Wazee Na Wazee Kulipeleka Mbele Na Kisha Akaishia Kufukuzwa? Hebu Leta Na Wewe Unachojua Kuhusu Kukengeuka Kwa Wachunga Kondoo Hawa,ni Wachungaji Wangapi Wamefumaniwa?Hebu Weka Picha Na Maelezo Kama Unayo Ili Tuelimishane
... KAMA unaamini wachungaji wote watakwenda
peponi basi utakuwa unakosea. Hebu sikia hii.
Mchungaji mmoja aliyejulikana kwa jina la
Michael Njoroge kutoka nchini Kenya
amekumbwa na skendo nzito baada ya
mwanamke mmoja ambaye ni changudoa
kuibuka hadharani na kudai alinunuliwa na
pastor huyo kwenda kanisani kutoa ushuhuda
wa uongo, Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya
nchini humo, kahaba huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Ester Mwende, awali alifuatwa na
mtumishi huyo wa Mungu na kumtaka
wafanye mapenzi zoezi ambalo lilifanyika.
Akasema baada ya zoezi hilo, ndipo mtumishi
huyo wa Kanisa la Fire Ministries Embakasi
alimtaka afike kanisani hapo ili kutoa
ushuhuda wa uongo na kumuahidi kwamba
angemlipa kiasi cha shilingi 10,000 za Kenya
(kama 180, 000 za Tanzania).
Mwande ambaye alikuwa akitoa ushuhuda
huo kwenye Kituo cha NTV cha nchini humo,
alisema alikubali na kesho yake alikwenda
kanisani kwa mchungaji huyo anayesifika
sana kwa miujiza na upako.
Akasema: Nilipofika nilikaa na kujifanya
nimepinda midomo. Muda wa maombezi
mchungaji akasimama na kusema mimi nina
matatizo, nimepinda midomo kwa sababu
kuna kanisa nilikwenda nikasema kuna
mchungaji amebaka mtu kwa hiyo pigo langu
lilikuwa kupinduka midomo.
Mwande aliendelea kusema kwamba mpaka
anatoka kanisani hapo bado alikuwa
amejipindisha midomo jambo lililomfanya kila
mtu aliyemuona aamini.
Akasema kesho yake alirudi tena na muda wa
watu kushuhudia uponyaji, yeye alitoka mbele.
Mchungaji alipomwona aliwaangalia watu na
kuwaambia: Huyu mama ni yule aliyekuja jana
akiwa amepinduka midomo kwa sababu ya
kuwasema vibaya watumishi wa Mungu.
Mwande alisema alishuhudia kwamba baada
ya maombezi ya siku iliyopita anamshukuru
Mungu alimponya na midomo yake iko
sawasawa kama zamani, kauli iliyosababisha
kanisa zima kulipuka kwa shangwe za
kumtukuza Mungu.
Mwande alisema aliamua kuweka wazi madai
hayo baada ya mtumishi huyo kumrusha
fedha nyingine walizokubaliana akidai
kwamba mbali na yeye pia mchungaji huyo
alimtaka amtafutie makahaba wengine watatu,
jambo ambalo alilitekeleza lakini nao pia
hakuwalipa.
Makahaba wenzake Mwande, wao walisema
walimtumikia mtumishi huyo kwa kutoa
shuhuda za uongo lakini hakuwalipa ujira wao
na walipomfuata aliwajeruhi miguuni.
Walisema baada ya tukio hilo, walitoa ripoti
kwenye Kituo cha Polisi cha Embakasi lakini
maafande hao walikuwa wakisuasua kumtia
mbaroni mtumishi huyo.