Msiposhtuka mapema mtaendelea kushangaa. Wanaume badilikeni. Mnapendaga kutumia biblia kama mfano wa kuigwa, hicho kitabu kimeandikwa na wanaume miaka elfu gani iliyipoita? Mambo ya mwaka 4 BC mnaleta mwaka 2017.
Nyie wanaume mnajijua mlivyo tabia zenu, mnajua jinsi mnavyo treat wanawake kwenye maisha yenu, kwahiyo msishangae mwaka wanawake wakiamua kuachana na nyie. We have options now, tuna uwezo wa kuchagua ni maisha gani tunataka kuishi hapa duniani sababu wanasema life is short, lakini ukiwa na mwenza ambae hamuendani yaani maisha ni magumu na marefu. So kama wanawake wana uwezo wa kuchagua, kwanini wawachague nyie? Ukinijibu bila kutumia maandiko ntakusikiliza.
Kama mnavyojua, watoto hujifunza toka kwa wazazi wote wawili. Je ni bora watoto waishi kwenye nyumba yenye magomvi, mateso, unyanyasaji ; au bora kuishi na mzazi mmoja na familia ( ya mama) yenye amani na upendo?
Jiulizeni, zaidi ya pesa na nguvu za kimwili, na uwezo wa kuzalisha mwanamke ( na hizi quality si wote walizonazo tehehee), ni nini hasa value ya mwanaume?? What else do you bring to the table that women do not? Kuweni wapole kidogo, heshimuni wanawake na muanze kutambua mapungufu yenu haraka sana.