Wanaume tunakufa na tai shingoni

Wanaume tunakufa na tai shingoni

Oscar Lyrics

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
2,732
Reaction score
4,652
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wanaume tunapitia changamoto nyingi kama ilivyoandikwa, tutakula kwa jasho.

Mwanaume anapambana ili kuitunza familia yake, analipa Gharama zote za chakula, ada, matibabu, mavazi nk

Siku zinaenda watoto wanamaliza masomo wanapata kazi wanaanza kusema nani kama mama.

watoto wanaanza kumgombania mama, Huku mzee anatelekezwa mwisho wa siku anakufa na stress.

Siyo wote wanaofanya hivyo but kwa wale wenye tabia ya ubaguzi kwa wazazi muache mara moja,
kweli wapo wanaume ambao wameripotiwa kuzitelekeza familia zao laini wengine wanasingiziwa.

Na huu uchonganishi huwa unatoka kwa mama, utasikia baba yenu alikuwa analewa na wanawake zake wakati mimi nikihangaika kuwatunza peke yangu.

Ndo maana kwenye familia nyingi unakuta wababa wanatangulia kufa, Mwanaume halii, anakufa na machungu yake moyoni.

Msondo ngoma waliimba wimbo unaosema 'wanaume tumeumbwa matesoo, matesoo kuhangaika.

Eeeh mwenyezi Mungu tusaidie wanaume tuwe na mwisho mwema.
old-man-1775239_640.jpg
 
Sikuja duniani kuteseka mimi au kutesekea wengine.

Huu msemo wa wanaume tuliumbiwa mateso nilisha ukataa.

Watoto na mwanamke nitawajali kwa kiasi chao.

Lakini fungu kubwa, nguvu kubwa na jasho kubwa nimewekeza kwangu kwanza.

Kuwekeza nguvu kubwa kwa mke au watoto bila kujijaji wewe huo nao ni ujinga.

Watoto wakikua wataondoka kwangu nitabaki mwenyewe.

Sasa lazima ni enjoy jasho langu uzeeni kwa amani.

Watoto wataenda huko na wao watakuwa na maisha yao.
 
Hii comment imenitia nguvu sana

Mimi kuepukana na hili sikupenda kabisa kufuga raia(watoto na mke) lakin kuna raia mmoja alikuja kwangu kitapeli na bahati mbaya nikampa ujauzito

Yaan mpaka sasa nabaki najiuliza hv huyu mtu kwanini aliamua kunitapeli na wakat nilimwambia kabisa kuwa sina ratiba ya kuoa mimi,mbaya zaidi kaja kwenye maisha yangu na mashariti yake mpaka huwa namtazama nashindwa kumuelewa,nilitaka kuwa huru afu mtu anakuja kuiba uhuru wangu
 
Hapa duniani bwana freedom is the key.

Haya mambo yakubanwa banwa nilishakataa.
 
Back
Top Bottom