kuna dada nilivutiwa naye nikiwa la tatu.. Alikuwa dawati la mbele yetu. Nikamwambia rafiki yangu wa dawati moja,yeye alikuwa akijifanya ni mjuzi wa mambo mengi. Akaniambia usipate shida,mwandikie barua.
Nikaogopa suala la barua,akasema angeandika yeye,na kuandika jina langu. Nikamwambia dili ikibaunsi tukifika kwa mwalimu mi na wewe urafiki wetu utaisha,we nipe mistari,niandike mwenyewe. Akaanza,mpendwa ......... Naomba kile kitu kilicho chini ya kitovu chako... Nikamuuliza mbona kama matusi? Ataelewa au ataona nimemtukana.. Akasema hiyo ndiyo njia ya kikubwa ya kufanikisha,na hakuna mwanamke yeyote anayekataa njia hiyo.
Akazidi kuniambia hata watu wazima,au walimu wa kike,yaani wanawake wote ni rahisi,na kuwa wanawake wanampenda mwanaume anayewatongoza. Mi kwa shingo upande nikanyosha nikampa na kumwambia akasomee nyumbani. Naye alikuwa mbishi,akasema atasoma palepale,bahati mbaya akamwonyesha na jirani yake. Ilikuwa ni aibu,kwani niliomba anirudishie barua yangu akakataa..mwenzake akampump,eti apeleke kwa mwalimu wa darasa,ambaye binti yule alikuwa ni bibi yake...
Nikamwomba radhi sana,ila hakuwa amechukia,ila alionyesha kutotegemea jambo lile kutoka kwangu.. Akaamua kwenda kwa mwalimu wa darasa ambaye alikuwepo mbele anaandika na kusahihisha daftari. Nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie ndani. Nikaomba bora nichapwe yaishe,kuliko niiambiwe nije na mzazi wangu. Alienda dada yule na kukaa kama dakika tano,kisha akarudi akiwa ameninuna na amejaa hasira. Nikasubiria kuitwa,sikuitwa hata siku moja. Nadhani alinisamehe hivyo hakupeleka barua ile. Nilimlaumu aliyenipa mistari ya barua,naye akasisitiza,mwanamke kuichukia barua ile lazima atakuwa mshamba..Nilimshangaa sana. Uhusiano hata wa salamu ulikufa kati yangu na dada yule..
Cha ajabu tulipokuwa la saba nilirudia tena mchezo wa barua na dada yule. Nikamwambia akasomee nyumbani akasema hataki kusubiri,ila alijawa furaha sana. Siku hiyohiyo tulikutana mstarini saa nane. Akaniambia angenijibu kesho yake. Sasa ikawa akiniona ananipenda ikaishia hapo.Kampani tu ya kawaida. Hata hivyo mi ilinitosha sana. Kwa sasa ameolewa ana watoto wawili,na ni air hostess wa shirika fulani la ndege..