Wanaume tubadilike jamani

Wanaume tubadilike jamani

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,724
Nitangulize shukrani ya uzima kwa muumba wa mbingu ....

Nitoe shukrani pia kwa wana Jf kwa ushauri na uzoefu nilioupata humu ...hakika humu ni shule tosha..


Mada yangu ni hii tabia hasa kwa sisi wanaume ...tumekuwa viumbe wasahaulifu kwa mema tuliyotendewa na wapenzi wetu hasa pale tunapofanikiwa kidogo..

Unakuta msichana wa watu alikupenda ukiwa mchafu ...una nguo mbili..kila Siku...suruari unafungia kamba...muda mwingine alikukuta huvai hata boxer lkn alikuvumilia...alikufichia aibu...alikupenda ...pamoja na masharobaro kumfata aliwatolea nje....

Leo umefanikiwa kwenda chuo kikuu au umepata kazi flani unamuona takataka unamdharau na kumuona sio hadhi yako tena kisa umekutana na masista duu....umesahau ulipotoka....

Kisa tu umejua kunyoa kiduku...umejua kuvaa jinsi na mlegezo na boxer....

Nawasihii wanaume wenzangu tubadilike....tukumbuke tulipotoka...

Tuwapenda wapenzi wetu...hasa wale wavumilivu ktk shida na raha.

Niwatakie siku njema
 
Kila jamo (likiwamo la mapenzi) na wakati wake! Khaa utampendaje mpenzi muda wote kwani yeye ni pesa?
 
Sidhani Kama sisi wanaume wengi wa humu tulifikia hatua hiyo ya kufungia Kamba siruali...
 
ujumbe mzuri. Ila na wao wakibadilika inakuaje hapo?
 
endelea kulelea....siku ukimwaga urudi utoe mrejesho
 
Sidhani Kama sisi wanaume wengi wa humu tulifikia hatua hiyo ya kufungia Kamba siruali...

Kwan kuwa humu ndio hujapitia shida?? Au unadhan kila MTU aliye jf katoke USA....
 
Ni vyema mkikumbushana kwan kuna baadhi yenu ni wepesi wa kusahau.
 
Back
Top Bottom