Wanaume, tendo la kujamiiana na Afya mgogoro!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
couple-lying-in-bed1.jpg


Kwa mujibu wa madaktari wengi , uwezo wa kujamiiana kwa wanaume ni kipimo cha afya yake pia. Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya afya ya mwanaume na uwezo wake wa kujamiiana. Hii ni taarifa rasmi ya kitabibu na imesheheni ukweli mkubwa sana.

Inafahamika vyema kwamba, magonjwa ya moyo, pia na kisukari, simanzi, kunenepeana, kudhalilishwa na matatizo mengine ya afya na saikolojia, vinaweza kuathiri uwezo wa mwanaume kusimika. Kusimika si jambo la moja kwa moja kama kujaza hewa kwenye puto. Ni taratibu yenye mchakato maalum ambapo mishipa ya damu, misuli, homoni, mfumo wa ufahamu na akili vinafanya kazi kwa pamoja.

Ikiwa moja ya sehemu hizo haifanyi kazi vizuri, huathiri mtiririko wote wa tendo hilo.
Kama mwanaume akigundua kwamba ana matatizo kwenye tendo la ndoa, hasa kusimika, yaani nguvu za sehemu zake za siri, inabidi aanze kuwa na waswasi na afya yake na hivyo kujikagua. Wanaume vijana wanaovuta sigara, huvuruga afya zao. Matokeo ya kuvurugika kwa afya hizo huonekana kwenye namna wanavyoshindwa au kuonesha udhaifu kwenye harakati za tendo la ndoa.

Baadhi ya watu walioko katika taaluma ya tiba ya kujamiiana wanakubali kwamba, uwezo wa kusimika unaweza kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na afya ya jumla ya mtu hasa kuhusiana na moyo wake. Ili uweze kusimika, uume ni lazima uwe na damu ya kutosha. Matatizo ya moyo yanayofahamika kama atherosclerosis, ambapo mafuta hujazana kwenye mishipa ya damu kiasi cha kukwamisha mtiririko wa kawaida wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, huweza kusababisha damu kutofikia uume na hivyo kusababisha matatizo ya kusimika.

Kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi, matatizo ya shinikizo la damu, kisukari na uvutaji wa sigara ni sababu kuu za mtu kupatwa na matatizo ya atherosclerosis.
Kuwa na uume uliosimama kwa nguvu sana, huweza kuongeza furaha ya mwanaume katika kufanya mapenzi, ama kuongeza kujiamini kwake kama mwanaume. Wanaume wengi mara nyingi huonekana kuvutika na ukubwa wa maumbile ya uume wao, lakini uwezo wa kusimika ndicho kitu cha muhimu zaidi.
 
Makala nzuri sana, tatizo limeelezwa na ufumbuzi, thx
 
ungemuuzia shigongo story yako, angetoa kwenye magazeti matatu-3, sumarise your work-be precise!
 
Back
Top Bottom