Wanaume njooni tuongee

Wanaume njooni tuongee

Cryspina

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2020
Posts
298
Reaction score
398
Wanaume ninyi ndio baba zetu na viongozi wetu. Mbona mnakubali kubaki nyuma katika jamii na kuacha mambo yafeli? Ni nani atakuwa mtetezi wetu sisi akina mama na watoto kama ninyi mnaogopa na mnakuwa wadhaifu. Najua na sisi kuna vijitabia ambavyo huwakwaza na kuwafanya mkose morali ya kushika nafasi zenu.

Ila si mnakumbuka kuwa ninyi ndio mlipewa dhamana ya uongozi wa kutuongoza sisi pamoja na kusimamia shughuli zote za dunia hii? Haya mambo yoyote tunayofanya ya kuwakosea ni ninyi mnatakiwa kusimama na sisi kutunyoosha aidha kwa ukali au upendo. Mwanamke anakuwa hakutext eti na wewe unamnunia.... Unaanzaje kumnunia mwanamke badala ya kumuelekeza na kumbadili tabia.

Mwanamke anakuja kukulilia njaa na matumizi, huyo anakupa ujumbe kuwa amekuamini wewe kuwa caretaker wake unachotakiwa ni kumtaarifu kuwa unataka muwe rasmi na sio ubabaishaji wa kudanganyana tu na kutumiana.

Najua kada ya kike tunawakosea sana na ni ukweli uliowazi kuwa tutalipia siku si nyingi kwa kutokuwa makini na maelekezo yenu mnapokuwa mnatukanya, mtusamehe na msiache kutuongoza.

Ninyi ni viumbe adimu na muhimu sana katika hii dunia.... Ndio maana hata katika uzao mwanaume hupatikana kwa taabu sana na mwili hutumia nguvu ya ziada katika kuumba mwanaume tofauti na mwanamke. Hii ni wazi kuwa ninyi ni jinsia teule na mliumbwa kuwa viongozi.

Katika Bible, kile kitabu cha Sira 9 mstari wa 2,imewekwa bayana kuwa..... "Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa" why mnatuacha sisi ndio tuwe na mamlaka ya kusimamia uchumi wa nyumbani mnataka watoto wawaoneje na kujifunza nini?! Why mnachukulia maisha ni mepesi kwa lugha nyepesi kama kusema hakuna ajira, au maisha magumu.

Hivi mnaona wenzenu akina Diamond anavyopambana hadi anaitoa familia yake katika aibu ya ufukara leo wanaheshimika, mama Naseeb anapopita na ile gari yake ya bei hakuna asiyeshtuka.

Hebu oneni akina Chris brown, Kevin hart, Will Smith, Idris Elba, Harmonize, Fred vunja bei na wengine wengi ambao hawafahamiki ila wanapambana na wanasimama nafasi zao, tazama wanavyowasitili wake zao na mama zao na dada zao na fedheha na taabu za hii dunia. Ninyi mnakwama wapi kufanya jambo lolote ili kusimamia jina lako ling'ae na kujenga ukoo imara na kumpa heshima mkeo na mama yako?!

Mataifa makubwa, jamii imara na zenye uwezo ni matokeo ya wanaume imara na wanaoshika nafasi zao bila kutetemeka. Tazama leo wachagga jamii ilikuwa imara sana ila kwasasa inazidi kudumaa na ndio wanaongoza kwa kuwa na vijana marioo, wanaume wa wasukuma na wamasai kidogo bado wanapambana kushika nafasi yao. Na ndio unaona ndio wanashika nafasi kubwa akina laizer, na baadhi ya viongozi.

Ninyi ndio makepteni wa hii dunia, mkilala ninyi nani atasimama na sisi. Achana na haya maneno ya hawa wanaharakati wanaosema mwanamke akiwezeshwa sijui nini hayo ni maneno ya kuficha msiba mzito tulio nao wa kukosa wanaume mashujaa katika jamii hii.

Mimi si kwamba siungi mkono wanawake kutafuta la hasha ni wajibu katika mazingira ya sasa ya kiuchumi ila sasa ndio isiwe hali ya kudumu. Mwanamke anajukumu lake la asili nalo ni kusimamia nyumba yake, mume wake na watoto wakati mumewe akiwa huko nje anapambana.

Jamani wanaume..... Nawaita tena wanaume..... Haijalishi upo umri gani, kuanzia 18,wewe ni mwanaume na unakila sababu ya kukamata nafasi yako na kushika usukani wa uongozi wako. Msitususie haya maisha kwa kukata tamaa. Mnatuachia sisi wanawake ndio tushike mamlaka za uongozi na maamuzi kwann mnafeli hivyo jamani?!

Popote ulipo kaka, rafiki yangu,mdogo wangu wa kiume, naomba usimame kishujaa piga kifua chako sema mimi ni mwanaume na ninakwenda kushika nafasi yangu duniani na kuimarisha mamlaka niliyopewa na wanaume wenzangu. Kama upo nyumbani kwa wazazi umekata tamaa naomba usimame na ujipe wiki moja au mbili na uweke nadhiri ya kutoka hapo ndani na kwenda kuwa na nyumbani kwako. Mkeo wako ambaye haujamuona bado yupo huko anakutafuta kwa maombi na kilio cha moyo na hajaonana na wewe kwasababu tu umechagua kukata tamaa umelala na kujificha ukisema maisha magumu na hakuna pa kutokea.....

Ewe baba ambaye katika familia umeona mkeo ndie mbeba gharama za familia, hebu ionee aibu hiyo hali na tazama upya vyanzo vyako. Huyo ni mkeo sio sponsor wako hadi unamuachia asimamie bili za nyumbani kwa kisingizio cha ugumu wa maisha.

Hapana maisha sio magumu, unayaangalia kwa ugumu. Yangekuwa ni magumu basi kuna watu huko nje wasingekuwa wanafanikiwa nyakati hizi. Ugumu wa maisha haya ni fumbo umewekewa na ukitumia kichwa chako vema utaona njia tofauti. Usiogope kubadili mbinu za maisha katika kutafuta.

Sisi kwetu upendo kutoka kwenu huwa tunausoma kwa namna mnatuhudumia na kutupa matunzo na ulinzi. Sio maneno matupu. Mkifanya hiyo ni dhahiri kuwa heshima itakuja kwenu bila ubishi na mtatupenda zaidi.

Msikate tamaa baba zetu, tunawapenda sana na kuwategemea ninyimsituangushe... Ninyi ndio viongozi wetu na ndio wafalme wetu. Tania na mienendo yetu ya ajabu mtusamehe bure hatuwahi wekwa unyago na kufunzwa kama mama zetu, tunajifunza kupitia matatizo yanayotukuta. Ndio maana single mother ni muelewa kuliko binti ambaye hajazalishwa na kuachwa.....

Mtuvumilie na mtusitiri kwa huruma. Wanaume mna mioyo ya pekee sana na yenye upendo wa dhati ya ndani sana. Sisi tukiwa na ninyi katika maisha huwa tunajiwazia sisi kwanza. Hii ni sifa yetu sisi mabinti wa sasa. Mwanamke naweza kuwa na shillingi 50,000 nikaja kuomba 5,000 yako ambayo ndio ipo kulinda mfuko wako na still ukanipatia. Wanaume MUNGU amewapa moyo wa upendo ajabu sana.

Sisi wanawake bila kujijua au kusudi tunawakwaza bila kujali ila mnatusamehe na mnaendelea kuwa na sisi na maudhui yetu. Tunasema unyanyasaji wa kijinsia hufanyiwa wanawake zaidi ila tunapuuza mateso na unyanyasaji wa kisaikolojia mnaopitia kutokana na vituko vyetu vinavyowaumiza mioyo yenu kila uchao, mtusamehe na mturekebishe kwa upole sana.

Tunawapenda na tunawahitaji sana.... Tafadhali msitususie hii dunia na changamoto zake.... Simameni na sisi simameni mtupiganie na sisi tunaahidi kuanza kubadilika na kuwa nyuma yenu.....
 
Dada umeshaolewa naomba uje inbox tafadhali kwa faragha
 
Ukiwa na mke wa namna kwenye nyumba halafu ukawa hoe hae tengemea amsha amsha hadi kero ila ndio vizuri napenda mwanamke wa namna hii
 
Ndefu sana ila jambo moja tu unaweza usilolijua unaweza kumuongoza mwanamke yule tu aliye tayari kuongozwa na sio kila mwanamke..

Hata uwe gentle vipi ukionana na izi kenge za mjini lazima ukubali yaishe maana hazisikii wala haziambiliki...
 
ndefu sana ila jambo moja tu unaweza usilolijua unaweza kumuongoza mwanamke yule tu aliye tayar kuongozwa na sio kila mwanamke..
.
hata uwe gentle vip ukionana na izi kenge za mjini lazima ukubali yaishe maana hazisikii wala haziambiliki...
Natamani uje ulete uzi wao hapa aisee
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Nimesoma mpaka mwisho, umeandika vitu kuntu, nimevipenda ila muwe sometimes mnaridhika na mwanaume unayekuwa nae kama unapata chakula, mavazi(Mara moja kwa mwaka) na malazi vumilia sio unahitaji zaidi wakati vitu muhimu unapewa.

Na msivyokuwaga na huruma nyie mburu kenge mwanaume akikupa kila kitu ukala ukashiba na unataka akugonge vizuri pia, kumbuka kuwa mwanaume mpambanaji hawezi kupiga show kali kila siku, badala ya kuvumilia unaenda kutafuta kajamaa kanakokula na kulala kwao afu kanakukaza kwa sifa, afu ndio unakaona ka mwanaume ka ukweli.
 
Mmmmmmhmn inafikirisha
Screenshot_20201129_162338.jpeg
 
Wanaume ninyi ndio baba zetu na viongozi wetu. Mbona mnakubali kubaki nyuma katika jamii na kuacha mambo yafeli?!

Ni nani atakuwa mtetezi wetu sisi akina mama na watoto kama ninyi mnaogopa na mnakuwa wadhaifu.

Najua na sisi kuna vijitabia ambavyo huwakwaza na kuwafanya mkose morali ya kushika nafasi zenu.

Ila si mnakumbuka kuwa ninyi ndio mlipewa dhamana ya uongozi wa kutuongoza sisi pamoja na kusimamia shughuli zote za dunia hii?!

Haya mambo yoyote tunayofanya ya kuwakosea ni ninyi mnatakiwa kusimama na sisi kutunyoosha aidha kwa ukali au upendo. Mwanamke anakuwa hakutext eti na wewe unamnunia.... Unaanzaje kumnunia mwanamke badala ya kumuelekeza na kumbadili tabia.

Mwanamke anakuja kukulilia njaa n amatumizi, huyo anakupa ujumbe kuwa amekuamini wewe kuwa caretaker wake unachotakiwa ni kumtaarifu kuwa unataka muwe rasmi na sio ubabaishaji wa kudanganyana tu na kutumiana.....

Najua kada ya kike tunawakosea sana na ni ukweli uliowazi kuwa tutalipia siku si nyingi kwa kutokuwa makini na maelekezo yenu mnapokuwa mnatukanya, mtusamehe na msiache kutuongoza.

Ninyi ni viumbe adimu na muhimu sana katika hii dunia.... Ndio maana hata katika uzao mwanaume hupatikana kwa taabu sana na mwili hutumia nguvu ya ziada katika kuumba mwanaume tofauti na mwanamke. Hii ni wazi kuwa ninyi ni jinsia teule na mliumbwa kuwa viongozi.

Katika Bible, kile kitabu cha Sira 9 mstari wa 2,imewekwa bayana kuwa..... "Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa" why mnatuacha sisi ndio tuwe na mamlaka ya kusimamia uchumi wa nyumbani mnataka watoto wawaoneje na kujifunza nini?! Why mnachukulia maisha ni mepesi kwa lugha nyepesi kama kusema hakuna ajira, au maisha magumu.

Hivi mnaona wenzenu akina diamond anavyopambana hadi anaitoa familia yake katika aibu ya ufukara leo wanaheshimika mama Naseeb anapopita na ile gari yake ya bei hakuna asiyeshtuka.

Hebu oneni akina Chris brown, Kevin hart, will smith, idris elba, harmonize, fred vunja bei, na wengine wengi ambao hawafahamiki ila wanapambana na wanasimama nafasi zao, tazama wanavyowasitili wake zao na mama zao na dada zao na fedheha na taabu za hii dunia. Ninyi mnakwama wapi kufanya jambo lolote ili kusimamia jina lako ling'ae na kujenga ukoo imara na kumpa heshima mkeo na mama yako?!

Mataifa makubwa, jamii imara na zenye uwezo ni matokeo ya wanaume imara na wanaoshika nafasi zao bila kutetemeka. Tazama leo wachagga jamii ilikuwa imara sana ila kwasasa inazidi kudumaa na ndio wanaongoza kwa kuwa na vijana marioo, wanaume wa wasukuma na wamasai kidogo bado wanapambana kushika nafasi yao. Na ndio unaona ndio wanashika nafasi kubwa akina laizer, na baadhi ya viongozi.

Ninyi ndio makepteni wa hii dunia, mkilala ninyi nani atasimama na sisi. Achana na haya maneno ya hawa wanaharakati wanaosema mwanamke akiwezeshwa sijui nini hayo ni maneno ya kuficha msiba mzito tulio nao wa kukosa wanaume mashujaa katika jamii hii.

Mimi si kwamba siungi mkono wanawake kutafuta la hasha ni wajibu katika mazingira ya sasa ya kiuchumi ila sasa ndio isiwe hali ya kudumu. Mwanamke anajukumu lake la asili nalo ni kusimamia nyumba yake, mume wake na watoto wakati mumewe akiwa huko nje anapambana.

Jamani wanaume..... Nawaita tena wanaume..... Haijalishi upo umri gani, kuanzia 18,wewe ni mwanaume na unakila sababu ya kukamata nafasi yako na kushika usukani wa uongozi wako. Msitususie haya maisha kwa kukata tamaa. Mnatuachia sisi wanawake ndio tushike mamlaka za uongozi na maamuzi kwann mnafeli hivyo jamani?!

Popote ulipo kaka, rafiki yangu,mdogo wangu wa kiume, naomba usimame kishujaa piga kifua chako sema mimi ni mwanaume na ninakwenda kushika nafasi yangu duniani na kuimarisha mamlaka niliyopewa na wanaume wenzangu. Kama upo nyumbani kwa wazazi umekata tamaa naomba usimame na ujipe wiki moja au mbili na uweke nadhiri ya kutoka hapo ndani na kwenda kuwa na nyumbani kwako. Mkeo wako ambaye haujamuona bado yupo huko anakutafuta kwa maombi na kilio cha moyo na hajaonana na wewe kwasababu tu umechagua kukata tamaa umelala na kujificha ukisema maisha magumu na hakuna pa kutokea.....

Ewe baba ambaye katika familia umeona mkeo ndie mbeba gharama za familia, hebu ionee aibu hiyo hali na tazama upya vyanzo vyako. Huyo ni mkeo sio sponsor wako hadi unamuachia asimamie bili za nyumbani kwa kisingizio cha ugumu wa maisha.

Hapana maisha sio magumu, unayaangalia kwa ugumu. Yangekuwa ni magumu basi kuna watu huko nje wasingekuwa wanafanikiwa nyakati hizi. Ugumu wa maisha haya ni fumbo umewekewa na ukitumia kichwa chako vema utaona njia tofauti. Usiogope kubadili mbinu za maisha katika kutafuta.

Sisi kwetu upendo kutoka kwenu huwa tunausoma kwa namna mnatuhudumia na kutupa matunzo na ulinzi. Sio maneno matupu. Mkifanya hiyo ni dhahiri kuwa heshima itakuja kwenu bila ubishi na mtatupenda zaidi.

Msikate tamaa baba zetu, tunawapenda sana na kuwategemea ninyimsituangushe... Ninyi ndio viongozi wetu na ndio wafalme wetu. Tania na mienendo yetu ya ajabu mtusamehe bure hatuwahi wekwa unyago na kufunzwa kama mama zetu, tunajifunza kupitia matatizo yanayotukuta. Ndio maana single mother ni muelewa kuliko binti ambaye hajazalishwa na kuachwa.....

Mtuvumilie na mtusitiri kwa huruma. Wanaume mna mioyo ya pekee sana na yenye upendo wa dhati ya ndani sana. Sisi tukiwa na ninyi katika maisha huwa tunajiwazia sisi kwanza. Hii ni sifa yetu sisi mabinti wa sasa. Mwanamke naweza kuwa na shillingi 50,000 nikaja kuomba 5,000 yako ambayo ndio ipo kulinda mfuko wako na still ukanipatia. Wanaume MUNGU amewapa moyo wa upendo ajabu sana.

Sisi wanawake bila kujijua au kusudi tunawakwaza bila kujali ila mnatusamehe na mnaendelea kuwa na sisi na maudhui yetu. Tunasema unyanyasaji wa kijinsia hufanyiwa wanawake zaidi ila tunapuuza mateso na unyanyasaji wa kisaikolojia mnaopitia kutokana na vituko vyetu vinavyowaumiza mioyo yenu kila uchao, mtusamehe na mturekebishe kwa upole sana.

Tunawapenda na tunawahitaji sana.... Tafadhali msitususie hii dunia na changamoto zake.... Simameni na sisi simameni mtupiganie na sisi tunaahidi kuanza kubadilika na kuwa nyuma yenu.....

Miezi 2 imepita nilihudhuria msiba wa jamaa yetu alifariki kutokana na kushindwa kuhimili vituko alivyokuwa akifanyiwa na mkewe, akanywa vidonge na pombe nyingi akafa.
Hongera sana kwa kujua mapungufu yenu ombeni sana mapungufu hayo yawatoke.

1. Ubinafsi i.e umesema mkiwa na sisi mnajifikiria ninyi kwanza hilo ni kosa kubwa sana labda kwa zile ndoa mme mmoja wake zaidi ya 1 lakini una mme mmoja na watoto ombeni Mungu mtangulize ndoa kwanza yaani kila kitu ni kwa faida ha ninyi wawili na watoto , msiishi na mume kama unaishi na hawara.
Acheni ule msemo cha mke cha mke cha mume cha mke pia iwe vyote ni vyenu na watoto.

2.Uhuru i.e mkiolewa msahau kuhusu uhuru mjue mke unawajibika kwa mume na mume anawajibika kwa mke sasa nyie wa kizazi mnajiita cha saaa mnataka uolewe halafu uwe huru kuishi unavyotaka mkiona , vyema mmegundua mnakosea katika ukristo neno linasema mnakuwa mwili mmoja kunia pamoja mkielewa hilo na kulitenda mtaimarisha ndoa zenu.

3. Tendo la ndoa
Msirudie tena kumkatalia mume tendo la ndoa kama silaha ya kumuadhibu mume , mnanyima mume unyumba miezi 6 mwaka mwanaume atakosa kukata tamaa nanyi sababu mume akilazimisha inakuwa amebaka na upendo unakuwa haupo hapo.

4. Ridhikeni na waume zenu msilinganishe msaidie mumeo na ulieidhike kinachopatikana zaidi kuzidisha utafutaji kila iitwapo leo , mnalinganisha Diomond mnamuona mzazi mwenza wake anavyomchezesha shere simba pamoja mafanikio na umaarufu wake . Mme wako hawezi kuwa Diomond , Dangote wala Davido na nyie wake zetu hamuwezi kuwa Hilary Clinton , michele obama wala Mhe Ummy Mwalimu hivyo mridhike na
Machaguo yenu. Acheni hizo kupunguza stress nje na kula mema ya nchi waume watarudi kwenu haraka mkijifunza kushirikiana na waume zenu kuimarisha ndoa nyakati zote hata kama
Mnaamsha
Waume zenu muwe wavumilivu wakati mnawapush waume zenu sio mnawakandandia huku ukweli ndio walinzi wenu wakubwa wacare wenu wakubwa na walezi no 1.

4.Mawasiliano
Mmeo ndio awe muwasiliano
Mkuu na mme pia mke ndio awe muwasiliano
Mkuu kwa mambo yote ya maisha yenu
Na watoto
MKIFANYA HAYO HAKUNA MWANAUME ATAYEWASUSA NA VIJANA WANAO SHAKA KUO NA KUOLEWA NDOA NYINGI ZA VIJANA ZITAFUNGWA NA NYIE WAKE MNATAKIWA MUWAFUNDE MABINTI JINSI YA KUWA WAKE BORA NYIE MTAPOBADILIKA MKIWA WAKE BORA .

Mwisho hongera kwa article yako ni mara ya kwanza au ya pili kuona niseme kuona humu JF zijengezo kama hii yako , barikiwa.
 
Wanaume ninyi ndio baba zetu na viongozi wetu. Mbona mnakubali kubaki nyuma katika jamii na kuacha mambo yafeli?!

Ni nani atakuwa mtetezi wetu sisi akina mama na watoto kama ninyi mnaogopa na mnakuwa wadhaifu.

Najua na sisi kuna vijitabia ambavyo huwakwaza na kuwafanya mkose morali ya kushika nafasi zenu.

Ila si mnakumbuka kuwa ninyi ndio mlipewa dhamana ya uongozi wa kutuongoza sisi pamoja na kusimamia shughuli zote za dunia hii?!

Haya mambo yoyote tunayofanya ya kuwakosea ni ninyi mnatakiwa kusimama na sisi kutunyoosha aidha kwa ukali au upendo. Mwanamke anakuwa hakutext eti na wewe unamnunia.... Unaanzaje kumnunia mwanamke badala ya kumuelekeza na kumbadili tabia.

Mwanamke anakuja kukulilia njaa n amatumizi, huyo anakupa ujumbe kuwa amekuamini wewe kuwa caretaker wake unachotakiwa ni kumtaarifu kuwa unataka muwe rasmi na sio ubabaishaji wa kudanganyana tu na kutumiana.....

Najua kada ya kike tunawakosea sana na ni ukweli uliowazi kuwa tutalipia siku si nyingi kwa kutokuwa makini na maelekezo yenu mnapokuwa mnatukanya, mtusamehe na msiache kutuongoza.

Ninyi ni viumbe adimu na muhimu sana katika hii dunia.... Ndio maana hata katika uzao mwanaume hupatikana kwa taabu sana na mwili hutumia nguvu ya ziada katika kuumba mwanaume tofauti na mwanamke. Hii ni wazi kuwa ninyi ni jinsia teule na mliumbwa kuwa viongozi.

Katika Bible, kile kitabu cha Sira 9 mstari wa 2,imewekwa bayana kuwa..... "Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa" why mnatuacha sisi ndio tuwe na mamlaka ya kusimamia uchumi wa nyumbani mnataka watoto wawaoneje na kujifunza nini?! Why mnachukulia maisha ni mepesi kwa lugha nyepesi kama kusema hakuna ajira, au maisha magumu.

Hivi mnaona wenzenu akina diamond anavyopambana hadi anaitoa familia yake katika aibu ya ufukara leo wanaheshimika mama Naseeb anapopita na ile gari yake ya bei hakuna asiyeshtuka.

Hebu oneni akina Chris brown, Kevin hart, will smith, idris elba, harmonize, fred vunja bei, na wengine wengi ambao hawafahamiki ila wanapambana na wanasimama nafasi zao, tazama wanavyowasitili wake zao na mama zao na dada zao na fedheha na taabu za hii dunia. Ninyi mnakwama wapi kufanya jambo lolote ili kusimamia jina lako ling'ae na kujenga ukoo imara na kumpa heshima mkeo na mama yako?!

Mataifa makubwa, jamii imara na zenye uwezo ni matokeo ya wanaume imara na wanaoshika nafasi zao bila kutetemeka. Tazama leo wachagga jamii ilikuwa imara sana ila kwasasa inazidi kudumaa na ndio wanaongoza kwa kuwa na vijana marioo, wanaume wa wasukuma na wamasai kidogo bado wanapambana kushika nafasi yao. Na ndio unaona ndio wanashika nafasi kubwa akina laizer, na baadhi ya viongozi.

Ninyi ndio makepteni wa hii dunia, mkilala ninyi nani atasimama na sisi. Achana na haya maneno ya hawa wanaharakati wanaosema mwanamke akiwezeshwa sijui nini hayo ni maneno ya kuficha msiba mzito tulio nao wa kukosa wanaume mashujaa katika jamii hii.

Mimi si kwamba siungi mkono wanawake kutafuta la hasha ni wajibu katika mazingira ya sasa ya kiuchumi ila sasa ndio isiwe hali ya kudumu. Mwanamke anajukumu lake la asili nalo ni kusimamia nyumba yake, mume wake na watoto wakati mumewe akiwa huko nje anapambana.

Jamani wanaume..... Nawaita tena wanaume..... Haijalishi upo umri gani, kuanzia 18,wewe ni mwanaume na unakila sababu ya kukamata nafasi yako na kushika usukani wa uongozi wako. Msitususie haya maisha kwa kukata tamaa. Mnatuachia sisi wanawake ndio tushike mamlaka za uongozi na maamuzi kwann mnafeli hivyo jamani?!

Popote ulipo kaka, rafiki yangu,mdogo wangu wa kiume, naomba usimame kishujaa piga kifua chako sema mimi ni mwanaume na ninakwenda kushika nafasi yangu duniani na kuimarisha mamlaka niliyopewa na wanaume wenzangu. Kama upo nyumbani kwa wazazi umekata tamaa naomba usimame na ujipe wiki moja au mbili na uweke nadhiri ya kutoka hapo ndani na kwenda kuwa na nyumbani kwako. Mkeo wako ambaye haujamuona bado yupo huko anakutafuta kwa maombi na kilio cha moyo na hajaonana na wewe kwasababu tu umechagua kukata tamaa umelala na kujificha ukisema maisha magumu na hakuna pa kutokea.....

Ewe baba ambaye katika familia umeona mkeo ndie mbeba gharama za familia, hebu ionee aibu hiyo hali na tazama upya vyanzo vyako. Huyo ni mkeo sio sponsor wako hadi unamuachia asimamie bili za nyumbani kwa kisingizio cha ugumu wa maisha.

Hapana maisha sio magumu, unayaangalia kwa ugumu. Yangekuwa ni magumu basi kuna watu huko nje wasingekuwa wanafanikiwa nyakati hizi. Ugumu wa maisha haya ni fumbo umewekewa na ukitumia kichwa chako vema utaona njia tofauti. Usiogope kubadili mbinu za maisha katika kutafuta.

Sisi kwetu upendo kutoka kwenu huwa tunausoma kwa namna mnatuhudumia na kutupa matunzo na ulinzi. Sio maneno matupu. Mkifanya hiyo ni dhahiri kuwa heshima itakuja kwenu bila ubishi na mtatupenda zaidi.

Msikate tamaa baba zetu, tunawapenda sana na kuwategemea ninyimsituangushe... Ninyi ndio viongozi wetu na ndio wafalme wetu. Tania na mienendo yetu ya ajabu mtusamehe bure hatuwahi wekwa unyago na kufunzwa kama mama zetu, tunajifunza kupitia matatizo yanayotukuta. Ndio maana single mother ni muelewa kuliko binti ambaye hajazalishwa na kuachwa.....

Mtuvumilie na mtusitiri kwa huruma. Wanaume mna mioyo ya pekee sana na yenye upendo wa dhati ya ndani sana. Sisi tukiwa na ninyi katika maisha huwa tunajiwazia sisi kwanza. Hii ni sifa yetu sisi mabinti wa sasa. Mwanamke naweza kuwa na shillingi 50,000 nikaja kuomba 5,000 yako ambayo ndio ipo kulinda mfuko wako na still ukanipatia. Wanaume MUNGU amewapa moyo wa upendo ajabu sana.

Sisi wanawake bila kujijua au kusudi tunawakwaza bila kujali ila mnatusamehe na mnaendelea kuwa na sisi na maudhui yetu. Tunasema unyanyasaji wa kijinsia hufanyiwa wanawake zaidi ila tunapuuza mateso na unyanyasaji wa kisaikolojia mnaopitia kutokana na vituko vyetu vinavyowaumiza mioyo yenu kila uchao, mtusamehe na mturekebishe kwa upole sana.

Tunawapenda na tunawahitaji sana.... Tafadhali msitususie hii dunia na changamoto zake.... Simameni na sisi simameni mtupiganie na sisi tunaahidi kuanza kubadilika na kuwa nyuma yenu.....
Dunia ya sasa ni 50/50 hakuna cha nani mwanamke nani mwanamume, kila mmoja apambane na hali yake, kuna wanawake madereva boda boda, kuna wanawake madereva wa magari, kuna wanawake mafundi ujenzi, kuna wanawake viongozi wa nchi tena mataifa makubwa, mfano: angel mark wazir mkuu ujeruman, kina asha migiro, Samia Suluu hao ni baadhi tu na wapo wengi zaidi ya hao.

Uanaume/ujinsia ulikuwa ni enzi za miaka 500 BC, (yaani kabla ya Yesu na wakati ule wa Yesu) iliyopita kwa sasa hiyo kitu hamna binadam wote ni sawa, hakuna cha kusema haya ni majukumu ya ''me'' au ya ''ke'' na hili swala la usawa ndo wanawake wanalipenda na kulipambania kila kukicha. Dunia ya leo haina tena ujinsia, ujinsia umebakia tu kwenye swala la kuzaliana/ kuongeza familia.

NB; Watu wote ni sawa kila mmoja awajibike kwa kazi, uongozi, cheo, utafutaji, majukumu ya namna ya aina yoyote yale katika familia, jamii na taifa bila utegemezi au visingizio vya ujinsia eti kwamba kisa ni mwanamke au mwanamume, kwaajili ya maslahi mapana na maendeleo ya famili, jamii na Taifa kwa ujumla.
 
dunia ya sasa ni 50/50 hakuna cha nani mwanamke nani mwanamume, kila mmoja apambane na hali yake, kuna wanawake madereva boda boda, kuna wanawake madereva wa magari, kuna wanawake mafundi ujenzi, kuna wanawake viongozi wa nchi tena mataifa makubwa, mfano: angel mark wazir mkuu ujeruman, kina asha migiro, samia sluu hao ni baadhi tu na wapo wengi zaidi ya hao.
uanaume/ujinsia ulikuwa ni enzi za miaka 500 BC, (yaani kabla ya yesu na wakati ule wa yesu) iliyopita kwa sasa hiyo kitu hamna binadam wote ni sawa, hakuna cha kusema haya ni majukumu ya ''me'' au ya ''ke'' na hili swala la usawa ndo wanawake wanalipenda na kulipambania kila kukicha. Dunia ya leo haina tena ujinsia, ujinsia umebakia tu kwenye swala la kuzaliana/ kuongeza familia.
NB; Watu wote ni sawa kila mmoja awajibike kwa kazi, uongozi, cheo, utaftaji, majukumu ya namna ya aina yoyote yale ktk familia, jamii na taifa bila utegemezi au visingizio vya ujinsia eti kwamba kisa ni mwanamke au mwanamume, kwaajili ya maslahi mapana na maendeleo ya famili, jamii na Taifa kwa ujumla.

Mkuu
Umefanya utafiti au angalia tafiti kazi na vipato kwa ujumla hapa Tanzania vya wanawake ukalinganisha na wanaume. Usemacho kimefanikiwa EU na USA sababu kuna ruzuku maalum huku Afrika, Tanzania ikiwemo, mwanaume bado ana wajibu wa kumuongoza na kumsaidie mwanamke, wanawake wetu wenyewe wanaanza kuona ukweli huu na ndio uzi wa mada hii.
 
Mkuu
Umefanya utafiti au angalia tafiti kazi na vipato kwa ujumla hapa Tanzania vya wanawake ukalinganisha na wanaume . Usemacho kimefanikiwa EU na USA sababu kuna ruzuku maalum huku Afrika , Tz ikiwemo mwanaume bado ana wajibu wa kumuongoza na kumsaidie mwanamke , wanawake wetu wenyewe wanaanza kuona ukweli huu na ndio uzi wa mada hii.
hamna kitu hapo, tatizo la wanawake wa tz, Africa wanapenda kitonga mno (mteremko) na ndo maana wengi wao hurubuniwa kirahisi wakitanguliza tamaa mbele, kwa kutazama/kuangalia na kumendea pesa za wanaume, wasizojua namna ya kuzitafuta na zinatafutwaje. Inafkia kipindi mpaka wanakubali kujizalilisha kwa namna mbalimbali kwa ajili ya pesa za mteremko(kitonga).
Wengine wanadiriki mpaka kutembea au kuolewa na watu wa marika ya babu zao na baba zao kwaajili ya tamaa zao za pesa za mteremko (kitonga) kutoka kwa wanaume wasizojua zimetaftwaje au zimepatikana vipi.
NB; Wanawake wa Tz, Africa wavivu, wazembe wanataka haki sawa ya kufanana na wanaume, ila linapokuja swala la kutafuta pesa hawachachariki kuzitafuta, hawafanyi kazi, badala yake wanakalia kutegemea wanaume, yabidi wafanye kazi wawe mafundi ujenzi, wawe madereva wa magari na bodaboda, wawe viongozi wa familia, jamii na taifa kama wanawake wa EU na USA, ilikusudi waachane na vitonga, kuomba omba na utegemezi kutoka kwa wanaume pia ili waheshimike. Bila shaka hii ndo haki sawa na itakuwa ndo haki sawa wanayoitaka ya kufanana na wanaume.
 
Back
Top Bottom