Wanaume nao hunyanyasika kijinsia makazini tofauti na inavyodhaniwa!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
15,419
upload_2017-4-22_11-47-44.png


Kama uki google kwa picha ‘Unyanyasaji wa kijinsia makazini’ utashangaa, kwani takribani asilimia 90 ya mapicha picha utakayoyaona yanawaonyesha wanawake wakifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na wanaume.

Lakini ukweli ambao hausemwi ni kwamba wanawake ni wachokozi zaidi ya mara 9 kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi. Najua kuna baadhi ya wanawake wanaweza kutokwa na povu lakini huo ndiyo ukweli wenyewe.

Kwa kawaida unyanyasaji wa kijinsia ni kitendo cha kumchokonoa mtu wa jinsia tofauti au hata jinsia moja kwa kumfanyia vitendo au ishara za kimapenzi kwa nia ya kumtega, kumshawishi au kumlazimisha kufanya naye mapenzi.

Na hii inaweza kufanywa na mtu mwenye madaraka mahali pa kazi dhidi ya walio chini yake au kati ya wafanyakazi wenyewe kwa wenyewe. Na tatizo hili dhidi ya wanaume limekuwa likikua siku hadi siku katika maeneo ya kazi hapa nchini ni vile tu halisemwi kama linavyosemwa pale muathirika anapokuwa ni wa jinsia ya kike.

Wanawake wamekuwa wakijificha kwenye kichaka cha kujiona kama vile wao ndiyo waathirika wakubwa wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia mahali pa kazi wakati wanaume kwa upande wao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya namna hiyo lakini wamebaki wakiumia ndani kwa ndani kwa sababu hawana pa kusemea.

Ni nani asiyejua kwamba wanawake licha ya kuvaa mavazi yenye kuacha sehemu ya miili yao ya faragha wazi lakini pia mikao yao isiyo ya staha inawaweka baadhi ya wanaume katika wakati mgumu na kushindwa kufanya kazi. Hilo linaweza likaonekana si tatizo, lakini je vipi kuhusu mazungumzo yenye kushawishi ngono yanayofanywa na wananawake au vitendo vya kuwashika wanaume sehemu zao za siri ili kupima maumbile yao, vitendo vya aina hii viitweje kama siyo unyanyasaji wa kijinsia. Je vitendo vya kuwatomasa tomasa wanaume kunakofanywa na baadhi ya wanawake pale wanapoelekezwa kazi au kufundishwa kazi fulani huo siyo unyanyasaji wa kijinsia?

Kuna baadhi ya mabosi wanawake wamekuwa wakiwataka kimapenzi wanaume walio chini yao kwa nguvu na kama wakikataa watakiona cha mtema kuni. Wapo baadhi ya vijana wa kiume wamegeuka kuwa watumwa wa ngono wa mabosi wao na hawathubutu kufanya fyoko maana hatma ya kazi yao imo mikononi mwa hao mabosi wanawake.

Kuna haja sasa ya wanaume kusema sasa basi imetosha na sisi tutafute jukwaa la kusemea madhila yetu maana wenzetu wamejiweka kwenye kundi la waathirika wa vitendo hivyo kumbe na wao wamegeuka Chui ndani ya ngozi ya kondoo.
 
Siyo makazini tu, barabani, majumbani, mtaani na maeneo mengine hutunyanyasa sana.

Imagine demu anakuonesha utamu msaliboko unafyatuka sikilizia shughuli ya kuuficha usikutie aibu mbele ya kadamnasi.
 
Kuna njemba moja ni mwalimu mkuu wa kashule kamoja hivi huko Kasulu mkoani Kigoma kimemtongoza shemeji yangu coz alikuwa ni matron katika mabweni ya wanafunzi wa shule ya msingi. Binti alivyomkatalia akamfukuza kazi tena sio official yaani amemtuma matron mwenzie tu mwambie fulani nafasi yake itajazwa na mtu mwingine.

Hapa ninawmuwazia haka jamaa nikachukulie hatua gani maana amenitia hasira sana hivi sisi huku maofisini kwetu tukiwafanyia hivyo waliochini yetu kazi zitafanyika kweli au itakuwa ni mapenzi tu badala ya kazi.

Ila unyanyasaji wa kijinsia nahisi umezidi sana kwa wanawake kuliko wanaume kwa hapa nchini kwetu sijui kwa nchi za majirani zetu.
 
Hivi dawati la jinsia kwenye vituo vya polisi,vinashughulikia pia vitendo vya unyanyasaji wakijinsia kwa wanaume vinavyofanywa na wanawake?


Cc: mahondaw
 
Kiuhalisia wa tamaduni zetu wewe mwanaume ukipekeka kesi hiyo wenzio wataona ya kuwa wewe huna rinda
 
Unyanyasaji upo sana tu, sema kwa jamii yetu ukilalamika unaongeza tatizo badala ya kulitatua. Bora ugugumie moyoni na kutafuta suluhisho kimya kimya mkuu.
 
Aiseeee mimi ninaombea nipate nafasi ya kunyanyaswa kijinsia na mwanamke.

Bosi wangu please kama ukiona ujumbe huu naomba ninyanyase. Usawa wenyewe huu nitachekelea kwelikwwli
 
Back
Top Bottom