Wanaume na tabia kama ya paka

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Jana nilikuwa najibu swali nililotupiwa na mpenzi wangu, alisema kama mwanaume akiamua kuchepuka basi anakuwa hamthamini mkewe, nikamwambia siyo,

Mwanaume anaweza akawa anampenda sana mkewe lakini akatoka nje, mwanaume kuchepuka si kuwa hamthamini mkewe, la hasha!.

Ili kumwelewesha ilibidi nimtolee mfano wa paka, maana tabia hiyo ya wanaume inafanana sana na tabia ya paka, ni hivi, paka hata awe ameshiba kiasi gani hawezi kumwacha panya anayekatisha mbele yake, lazima atamkimbiza tena kwa bidii utadhani ana njaa kweli, akimkamata basi atamchezea weee hadi afe na akifa asilani hawezi kuacha kumla kichwa, unakuta panya kaliwa kichwa tu unajiuliza kulikoni?

Hapo jua paka alikuwa kashiba ila kichwa hawezi kukiacha hata wawe panya kumi.

Hivyo ndo ilivyo kwa wanaume pia, hata kama anamthamini vipi mkewe bado havumilii kuona mwanamke anapita mbele yake.

Hivyo basi nitumie fursa hii kuwapa matumaini wanawake, kwamba mwanaume kuchepuka si kwamba hakupendi, la hasha bali ni haka ka tabia kama ka paka.
 
Heheheh mkuu nimeacha michepuko siku nyingi...sijui ndio paka nimezeeka.

paka hata akizeeka panya akapita lazima amfukuze na akimshika lazima ale KICHWA.
 
Duh!hatari sasa ,lakini hiyo tabia inaweza kuepukwa pia!

inaweza mkuu ila inahitaji kazi kubwa, kama kutaka kumfanya mtu mfupi arefuke, maana hii tabia ni inborn na ni genetically inherited.
 
Yaani nachukia kusika habari za michepuko,kuchepuka....jamani hebu ifike mwisho tuache hizo mambo....

Mbona mi siwezi kuchepuka??? ooooh mamaaa.....:loco::loco:
 
Mwanaume ni sawa na kunguru hata umfuge vip porin atarudi tu.
Mwanamke uliyenaye anaweza kuwa na kila sifa ya uzur na ndani ni aman kabisa lakin akikatiza mwngine lazma anyakuliwe hata kama hana sifa kama za mke wake.
Najiuliza sana sijui kwann hii hali imetukumba sana wanaume
 
Men are canal creatures they are allways controlled by their dick
 

Nyaaaaauuuuuh!!!
 

Wanajiendekeza tu icho sio kilema tuseme mtu kazaliwa nacho.
 
Hapana ni kujiendekeza na tamaa tu, mana mtu mwingine anachapuka ukiangalia uwo mchapuko wenyewe hata mwenzi wako akiambiwa anaanza kujiuliza! chapuka mwenzako akisikia mwenyewe anaona hapa mwenzangu kweli kashindwa kujizuia sasa swali je ikitokea hali hiyo inatokea kwa mwanamke je?
 

Uzinifu tu
 

mwanamke ni marufuku kuchepuka, jaribu uone sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…