Wanaume mliokuwa mnataka kuwafahamu na kuwajua wanawake, UKWELI huu hapa

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
Wanaume wengi tumekua tukisema wanawake hawaeleweki...

Ni kweli sababu wenyewe wana jiendesha katika taswira tata.

Ujumla wa taswira hiyo tata ni kwa manufaa ya uwepo wao ila kikubwa zaidi ni kwa usalama wao na asili ya dunia.

Sasabu panapo tokea changamoto yoyote wao ndio waathirika zaidi,na huu utata wao sio kwasababu wamejiweka hivyo...hapana wameumbwa hivyo kwa ajili ya ulinzi na usalama wao na kuilinda dunia.

Kabla sijaanza zungumza chochote ifahamike kua asili inamlinda mwanamke zaidi imlindavyo mwanaume....

Sababu mwanaume mmoja kwa manufaa ya asili ni sawa na wanawake 30,hivyo wanaume ni bidhaa ya kutosha kuliko wanawake...


Mwanamke mmoja akipotea ni sawa umepoteza wanaume 3 katika mwezi mmoja na ukipoteza mwanaume ni sawa umepoteza 0.3 ya mwanamke katika asili kwa mwezi mmoja.

Anyway tuiache hiyo ni somo la kesho...

Twende katika nguvu ya mwanamke...

Vitu vikuu ambavyo wanawake wanatumia kutimiza utata wao ni WOGA, UDHAIFU, na UNYONGE...

Vitu hivi vitatu ndiyo siraha kubwa ya Mwanamke vinavyo mlinda na kushinda vita au mfumo dume kirahisi sana...


Kama ulidhani,udhaifu,woga na unyonge wa mwanamke kimaumbile na kibaolojia ni vitu vinavyo mfelisha,hapana ulikua unajidanganya na ndiomana humuelewi!

Mwanamke ni anti mindwise...usipoteze muda wako kumuelewa huta weza,mwanamke ni mfumo tata,ulioumbwa hivyo kuijilinda na mifumo ya kidume,sababu wao ni bidhaa muhimu ndiyo maana wanazaliwa wengi...japo bado si ya kutosha.

Utata na hali ya anti mindwise ni vitu vinavyo mfanya kua imara na hatari mara milioni ya Mwanaume Jasiri,na mwenye nguvu za kutisha.

Vitu hivyo ni kama bom la nyikilia,kama mwanamke akitumia vitu hivyo,kukumaliza ni kitendo cha sekunde tu....

Ndiyo maana hakuna vita ambayo mwanaume atakukuja kushinda kiasili kwa mwanamke,na ndio maana asilimia kubwa ya mifumo ya kidunia ya mifumo dume,imemuweka mwanamke katika mazingira ya captive...

Sababu ni kiumbe chenye uwezo mkubwa kama kikiwa huru,uhuru ambao mwanaume anaona unaweza hatarisha usalama wa mifumo dume.


FAHAMU SIRAHA HIZO HATARI ZA MWANAMKE

1. WOGA

Woga wa mwanamke husababisha ajijengee Ulinzi katika asili yake ya kuishi (Security cover for survival)

Atahakikisha kila ambacho kitamuweka salama dhidi ya dunia na mwanaume au mfumo dume awenacho...

*Mfano wa vitu hivyo ni

(i) Utii,Heshima,Unafiki na Usiri...hivi ni vitu au silaha muhimu sana kwa kujenga usalama mbele ya mwanaume au mfumo dume na dunia dhidi yake.

Mfano siraha hizi hutumiwa sana pia na majeshi dhidi ya kiongozi wao.

Mwenye kukuonesha vitu hivi kama ana nia ovu na wewe huyo ni hatari sana,sababu utampa uaminifu wako...

Na hapo ndipo wanawake wanapataka...umpe nafasi ya kumwamini,anajua ukimwamini atakua salama.

Pia wanatekeleza baadhi ya mambo yao kwa usiri mkubwa...ni ngumu kujua kila kitu cha mwanamke...

Na siri ndiyo nguzo kuu ya usalama wa kidunia,mfano Mungu ana siri pia Serikali yako ina siri na siri ndiyo nguzo kuu ya usalama na ulinzi,Mwanamke ana ulinzi na usalama wa siri zake.

(ii) Usalama wa maisha na usalama wakesho yake.

Asilimia kubwa wanawake ni wahatamia hazina,wabahili na Wabinafsi

Hivi ni vitu muhimu sana,na hawajapenda kua hivyo,ni asili inawataka kua hivyo...

Sababu ni viumbe ambao kama ikitokea changamoto ya kifizikia au kimaumbo na kiutawala katika dunia wao ndiyo hua waathirika wakubwa.

Sababu ukweli ni kwamba they have mentality power and not a phyisical power...

Kutokana na asili mwanamke anajiona yupo kwenye hatari na wasiwasi wa kesho yake,kulingana na tabia za ulimwengu na mifumo dume...

Usalama na imani kuu ya mwanamke ipo katika hazina yake ya mali na fedha.Fedha na mali kwa mwanamke ni tumaini kuu kwa ajili ya usalama kwanza na sio utajiri.

Mwanamke ni mgumu kutoa,ila ni mwepesi kupokea sababu anachozingatia ni uhakika au ukuaji wa hazina yake ambayo yeye anaamini kati ya vitu vinavyomhakikishia usalama wa maisha yake ya leo na kesho ni akiba yake,akiba ya mwanamke si kwasababu ya utajiri wake bali usalama wake kwanza.

Hivyo wanawake "they have high security of money and asset"

2. UDHAIFU

Udhaifu wa mwanamke humfanya ajenge mazingira ya kukwepa hatari(Non risk taker)

Wanawake hawapendi kujihusisha na mazingira yoyote ambayo yanaonesha kuwa na 50/50 ya hatari ya usalama wa kiafya na kiuchumi...

Tabia hii imewafanya wawe upande ambo ni salama zaidi dhidi ya afya zao na uchumi wao.

3. UNYONGE

Unyonge wa mwanamke ni siraha maalumu kwa kurubuni mitazamo ya mwanaume kiasili,na sio kwa hiari.

Hali hii ya kuonekana mwanamke ni mnyonge humpa faida ya kutoonekana kua na madhara,au effect ya maamuzi ya kimapinduzi...

Jambo baya ni kwamba unyonge ambao mwanaume anauona akimtizama mwanamke ni katika umbile lake,ongea yake,utii na heshima yake,ila inasahaulika kuwa binadamu sio umbile peke yake bali binadamu hasa yupo katika ubongo au akili yake...

Na kitu kibaya zaidi kuhusu akili ya mwanamke,amepewa uwezo wa "ku-read mind" kwa asilimia kubwa mara tatu ya mwanaume

Licha ya kua na akili sawa na mwanaume ila ana uwezo huo,ambao ni mahususi kwa ajili ya kujilinda yeye,pia kumlinda mtoto...


Hivyo kwa lugha ya kifizikia tunaweza sema Mwanaume ni strong ila katika muktadha wa mind domination and intelligency mwanamke ni number one...

Sasa tukirudi duniani ni kipi kinatawala?! je...ni fizikia au akili?


Kama itabaki hivi basi wanaume ndio dhaifu.

Huu ndiyo ukweli ndio maana mwanaume anatumia kila mbinu kumfanya mwanamke kuwa captive....

Kuna kanuni za kidunia na sheria za baadhi ya dini zinamfanya mwanamke awe captive...

Wanafanya hivyo sababu tayari wamejua nguvu na matokeo ya mwanamke kama akiwa sawa na mwanaume...

Ndio maana matumizi ya nguvu na hasira,dhidi ya kummiliki mwanamke yamekua yakitumika sana na mwanaume

Matumizi ya nguvu na hasira na ukatili hua ni ishara ya uwoga mkubwa wa mwanaume kupoteza umiliki na utawala dhidi ya viumbe hawa.

Wanawake ni Strong mara milioni zaidi ya mwanaume that is why men apply captive methodology to reduce women power.

Japo ifahamike kuwa nguvu kubwa anayoitumia mwanamke kwa siraha zake hizi si kua mtawala au mwenye nguvu zaidi ya mwanaume kiulimwengu au kidunia...HAPANA ni katika kujilinda yeye na kizazi chake...

Wanawake hawapo kwa ajili ya utawala au utajiri ila kuilinda asili,na si kwasababu wamependa kua hivyo bali wameumbwa hivyo....

Jambo hili ndiyo linawachanganya wanaume wengi,ndiyo maana wameamua ku-apply captive methodology dhidi ya mwanamke.

JAPO Matumizi ya captive methodology yanaonekana kuweza kutawala ulimwengu wa mwanamke ila kama nilivyo sema awali mindset na ulimwengu wa wanawake hua tata au kinyume cha fikra za mwanaume ni hivi kama ukimuweka captive mwanamke utageuka kua mtumishi na mtumwa wake kumuhudumia na kumkamilishia mahitaji ya kiasili...

Anyway ngoja niishie hapa..

Nawakilisha...
 
Toa uthibitisho wa uliyoongea. Ulifanya wapi research au umeyatoa kichwani? Umetumwa?!

Tunataka tafiti otherwise umeandika pumba
Tafiti zinaumbwa na mwanadamu au Mungu,je tafiti ni lazima ziwe nje ya mtamkaji...Kama ni hivyo...hatuaminiani!

Na kama hatuaminiani ukombozi wetu wa kifikra ni tegemezi????!!!!!

Na kama tegemezi Tunamtegemea naniii????
 
Kwanza nani kakuambia kuwa wanaume hawawaelewi wanawake? Lini?
Naona umeandika mauza uza... huna uthibitisho. Uzi wako ni muflisi... potea!...
Muktadha wa itirafu zako za kuelewa ni uwasilishaji sahihi wa changamoto ya kimahusiano ya kijinsia...

Hata hivyo Asante kwa kutupa chemko la ubongo wako kwasababu ni msaada katika tafiti...
 
What mental case is this...

Unaongea utafkiri mnyama huko mwituni kapewa kishkwambi a type. Yani uko sehemu ya hatari sijui vitani una Kazi ya kujilinda na maadui!!!!!

Yani nimepiga picha una kwato na mkia mkuu, umesimamia miguu minne una type

Ndo shida ya kujifananisha na wanyama...

Women are not your enemy.
 
By the way yes men are getting weaker they'll go extinct, read here 👇🏾

 
Kuna hoja hapo japo sio sana.
Kamfano kadogo.
Ukiwa na mahusiano na single maza ndio utajua haya ya ndugu muandishi

hamsumbuani kuanzia mawasiliani,kutoa mbususu,anakusikiliza na heshima tele,yani anaishi kama wife material nk kwakua anahitaji ulinzi wake na watoto .ila nyuma ya pazia sasa
 
Kuna hoja hapo japo sio sana.
Kamfano kadogo.
Ukiwa na mahusiano na single maza ndio utajua haya ya ndugu muandishi

hamsumbuani kuanzia mawasiliani,kutoa mbususu,anakusikiliza na heshima tele,yani anaishi kama wife material nk kwakua anahitaji ulinzi wake na watoto .ila nyuma ya pazia sasa
Huyo single mother anayekupa mbususu mlete hapa nim
images (55).jpeg
 
Back
Top Bottom