ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,368
- 50,737
Sio mara chache nimeshasikia kuwa kuna baadhi ya wanawake fulani wana neema sana. Unapowaoa basi baraka zinamiminika na mafanikio makubwa unayaona. Sote tunafahamu karibu kila mafanikio ya baadhi ya wanaume basi behind anakuwepo mke.
Ni sawa ingawa sio kwa wote maana watu wametofautiana pia. Kuna wengine wanazungumzia eti kuna baadhi ya wanawake wa makabila fulani ukiwaoa basi mabalaa yanafuata. Hizo ni imani zipo na ni tamaduni zetu tunasema kila siku sifa za watu fulani wabaya, kabila fulani wabaya. Ila hatujitanabaishi kama sisi ni wakabila. Ni sahihi mitazamo hii ipo hata kwenye mambo mema kwamba nimeskia stori eti unapotaka mke ni muhimu kuangalia vigezo fulani fulani.
Swali kwa wanaume wanaomini kuwa mafanikio yao kimaisha yametokana na juhudi ila pia ipo nguvu ya mke wake ni kweli kwetu sisi vijana kuchagua mke kwa kuangalia baadhi ya mambo kama kiwango cha elimu,dini,kabila fulani (rahisi kutoka nae kimaisha),familia yake.Au tuendelee kuusikiliza moyo kwa vigezo vyake kama uzuri, tabia.
Kijana wenu nipo na wasichna kibao nataka niingie kwenye uchumba kisha ndoa na nitumie akili zaidi,wanawake wapi wana baraka? Sitaki kukosea kuoa.