Wanaume hebu tuwe ''wanaume''

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,815
Habarini humu wapendwa!!!

Siku hadi siku wale wanaume wenye mambo hasa ya kiume wanazidi kupotea,wanaume wengi wamepoteza majukumu muhimu yanayomtambulisha kama mwanaume,kwa kukosa utambulisho halisi wa kiume wanawake nao wameshindwa kujivunia hao wanaume nao wanajifanya kama wanaume ili kuziba pengo hili.

Mwanaume ni mtu wa kwanza kuumbwa,kwa wale wanaoamini katika Mungu nafikiri tunakubaliana na hili, lakini haina maana eti ni muhimu zaidi kuliko wanawake la hasha, pia Mungu alijua kutakuwa na ndoa hivyo mapema akapanga majukumu au tunaweza kisema katiba mama itakayoongoza ndoa hizo, ndipo aliposema 'mwanaume anatakiwa kumpenda mke wake na mwanamke anatakiwa kumtii mume wake, ila pia akampa mamlaka mwanaume ya kumtawala mwanamke,ndo maana alisema mwanaume ni kichwa,pia akasisitiza mwanamke ni kiumbe dhaifu kwahiyo lazimla kuishi nacho kwa ''AKILI'',

Ili uweze na kuwa na haki ya kumtawala mke wako lazima utimize sharti la kumpenda na kama utampenda means utamtawala kwa haki na utawala wowote wa haki unaleta amani,tena inabidi kupenda sana,ndipo akasisitiza mpende mke wake kama Kristo alivyolipenda kanisa,naye mwanamke akaambiwa mtii mume wako kama unavyomtii Kristo, kwa upande wa ndugu zangu waislamu wanaruhusiwa kuoa hadi wanawake wanne hii inaonesha kwamba kuna kitu cha ziada ambacho mwanaume anacho na mwanamke hana ili sio cha kujivunia wala kutuletea kiburi maana tumepewa tu kwa utukufu wa Mungu.

Tatizo ni kwamba wanaume tumeshindwa kutumia kile tulichopewa na Mungu kwa faida ya wanawake wetu,tumepindisha ukweli na kudhani kuwa tumepewa ili kutawala kwa hila na kulazimisha mawazo yetu pasi na haki,wanawake wapo automatic kuhisi kama naishi na mwanaume wa aina gani na hapo anakuwa pia automatic kwenye kuamua namna ya kuishi naye,baadhi ya vitu vya msingi ambavyo wanaume wengi wamepoteza ni...

1.KUJIAMINI 2.UKWELI 3.UAMINIFU 4.KUHUDUMIA FAMILIA NA KUIJALI 5.KUWA MFANO WA KUIGWA 6.KUTOA MWONGOZO KATIKA FAMILIA 7.UVUMILIVU 8.AKILI NA BUSARA 9.KUTOJITUMA KWA BIDII 10.HAKI BADALA YAKE WENGI NI MADIKTETA

Wanaume nao siku hizi wanasusa,wakikasirika wanasusa chakula,wanasusa tendo la ndoa wanasusa,wanasusa... Sasa wewe kichwa unaposusa means umeshindwa kumsimamia mkeo so yupo free sasa kufanya anachotaka,kuna tabia zinaanza kujitengeneza sasa baadae unalalamik, hali kadhalika kukosa kujiamini,kitu hakiwa hadi mtu mwingine akuambie kinafaa ni hatari kwa mwanaume...

Daaah ok nimechoka kuandika nahisi inatosha ila...!!!
 
Hasa hawa wa dar...ni bure kabisa...wanapaka mpaka mikorogo_mwanaa wa maiskiiii...?!!!!

Mwanaume badala ya kujitambua na kujiamini...wanaanza kulialia na kukimbilia vijichipsi kuku magengeni.
 
Kuweka mgomo au wengine mnaita kususa sio uanaume? if that's the case, then screw uanaume.
 
Kuna mijanaume mingine aiachi pesa ya kula akirudi akikuta mboga nzuri anajilamba ata ailizi wala kukoloma pesa umepata wapi. nae Huyo mwanaume
 
Mi nafikiri hata tabia uliyoionesha mtoa thread ya kuandika maneno mengi bila kuhit point siyo tabia ya kiume, be short, brief and clear! Vipi kuhusu experience yako kwa wanawake? Umeish na mwanamke/wanawake kwa muda gani? Siyo unaleta theory hapa! Life is not a rehearsal!
 
Wanaume siku hizi mambo yao kwenye uanaume hayapo kwenye uanamke yapo kiasi utadhani ni watu wasio na jinsia.....
Majukumu muhimu ya kiume mnayakimbia mnachobakiza kusema ni mwanaume kichwa cha familia kama majukumu huyataki my dear we sio kichwa cha familia ni kichwa cha ****.
Siku hizi kulia ndo kazi yenu kubwa, kuliko kulia bure heri mchukue tenda ya kulia misibani atleast kilio chenu mkigeuze mtaji.....
I remember those time when men were men
 
1. watu wote wamejawa na tamaa kila mtu anataka apate kitu bila jasho, mf. tumesoma wanaume wengi hasa vijana wanasema wanataka wamama wa kuwalea
2. mtoto wa kiume kukosa muda mwingi wa kukaa na wajomba/baba/babu/vijana wenzake na kujua majukumu yao
 
Back
Top Bottom