Mkuu kumbe nawe mwigizaji mzuri tu...Kupenda sana ki ukweli si kuzuri kabisa Kwa kuumizwa huku kila wakati ni Bora kujifunza kuigiza tu ili wote tuwe sawa
Pole sana kama yamekukuta.Naam mdada anakuwa mwenye amani na furaha tele kwa kuwa amekuweka pahali sahihi na moyo wake unaamini kuwa wewe ndiwe mtu sahihi kwake.
Hahahahahahaha ila kuna ukweli aisee! Ila tatizo nao huwa wanatusumbua sana mwanzoni mpaka akija kukubali unakuwa huamini kama kweli ndio kakubali au anaegesha tu maana kuna wengine unajipendekeza sana ndio anakuja kukuelewa baadae!Nafsi imenisuta nimeshindwa hadi kukoment.
Siyo wanaume tu. Hana wanawake wa namna hiyo wapo. Hapa suala linakuja kama we ndo umeguswa ni KE basi utalaumu ME. Na kama ni ME utalaumu KE. Suala linabaki ni nani kamfanyia timing mwenzake.Umekutana na mdada hana muda nawe, ukavutiwa nae, ukamshawishi weee! Shawishii weeee! Mdada wa watu, akaanza kukufikiria, akakutafakari, akakuwaza, mwishowe akaona isiwe shida, akakukaribisha.
Kakukaribisha kwenye conscious mindyake, baada ya muda automatically akakufanyia uhamisho wa kukupeleka kwenye subconscious mind yake. Naam mdada anakuwa mwenye amani na furaha tele kwa kuwa amekuweka pahali sahihi na moyo wake unaamini kuwa wewe ndiwe mtu sahihi kwake.
Masikini ya MUNGU, kupitia kujitoa sana kwa mkaka, mkaka anajua tu kuwa sasa yuko kwenye sakafu ya moyo dada huyu. Hapo ndo anaanza vitimbi, vurugu, kutojali, na kukusema ovyo, "anajipendekeza tu, wala simpendi" Kweli?
Kama usingelimshawishi angejipendekeza kwako?
Kafanya kosa kukupenda kwa dhati?
Angekukataa na kukuzodoa mbele za watu ungejisikiaje?
Jiweke kwenye nafasi yake, vaa viatu vyake pitia maumivu yake kisha toa tathimini, nao wana moyo kama wewe braza meni
Nyie wanaume dizaini hii mnafanya hadi sisi wenye tabia nzuri tusipate wa dhati aisee.
Muongopeni MUNGU.
Naingia kwenye mafunzo ili niwe muigizaji pia nadhani nitakua muigizaji mzuri zaidiMkuu kumbe nawe mwigizaji mzuri tu...
Safi sana mkuu na kwa kweli ufanikiwe huenda ukaiokoa tasnia yetu ya Bongo movies...Naingia kwenye mafunzo ili niwe muigizaji pia nadhani nitakua muigizaji mzuri zaidi