Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,246
- 7,111
Ahoua kazi yake ni mcheza mpira,anajua kabisa kufunga goli kwake ni Pesa ,utajiri na maisha mazuri.
Anajua kabisa akifunga goli hasa katika michuano hii ya CAF atazawadiwa fedha nyingi, fedha za mama,mashabiki na wafadhiri.
Anajua jina lake litaandiikwa kwenye vitabu vya CAF,Clabu ya Simba na magazeti yote Afrika.
Anajua kabisa soko lake litapanda na bei yake itapanda.
Anajua kabisa umaarufu wake utaongezeka,hakuna mtu asietaka umaarufu,hata Mimi natamani umaarufu.
Anajua atasifiwa kwa kuipeleka Simba hatua za juu.
Hayo ni machache sana,lkn Kuna mengi sana mchezaji hua anatamani kufunga magoli mengi zaidi.
Kwa kifupi mchezaji anajua mpira ni magoli na faida ya kufunga magoli kuliko hata sisi mashabiki.
Wanasimba wenzangu Ukiona mchezaji kama Ahoua au kapombe amekosa goli maana yake sio kwamba hataki,hajui,Hana uwezo au amefanya makusudi.
Anagalie ni ameshafunga mara ngapi,na ukiangalia mechi ya Znz Ahoua alifunga goli ambalo ndio linatupeleka SA tukiwa mbele.
Jamani eeh hakuna alieweza kujua mawazo ya Ahoua kuamua kupiga mwenyewe bila kutoa pasi,huenda Kuna kasoro aliiona kwa Ateba na Mutale ambayo sisi watazamaji hatukuiona.
Jamani eeh mpira pia ni mahesabu,na pengine alipiga hesabu zake kwa haraka akaona Bora ashuti yeye kuliko kutoa pasi,kwani hakuna ushahidi kua Kila pasi huzaa goli,Kuna wengine pia hukosa au hunyang'anywa.
Mfano yeye kapewa pasi na Mpanzu lkn kakosa.
Kumbukeni mpira ni mchezo wa bahati na makosa.
Unaweza kulenga goli bahati ikawa Yako ukafunga au kama sio bahati Yako ukakosa.
Ni kawaida na mara nyingi ukiwa shabiki na mtazamaji ni rahisi kukosoa na kuona wachezaji wanakosea lakini hakika sio kazi rahisi hivyo,wanaocheza ndio wanajua ugumu.
Kumbukeni timu pinzani nayo Ina kocha,imefundishwa,inacheza,inazuia,na piq inataka ushindi.
Hata kwa maaskari Kuna mafunzo ya kulenga shabaha(Range),kwa mfano wakipewa risasi kumikumi,Kuna wakati askari mmoja anaweza kupata zote na Kuna wakati anapata kadhaa.
Kumbuka siku pia hazifanani,
Mfano wawindaji Kuna siku wanafanikiwa kupiga wanyama na Kuna siku wanakosea shabaha.
Hebu tumuangalie Ahoua ameifungia Simba magoli mangapi na assist ngapi ya mechi za ndani na za nje, akiwa amekaa ndani ya Simba Kwa Muda Gani, ukilinganisha na mchezaji kama Chama mfano.
Hebu tufikirie kama Ahoua ana mwaka mmoja ndani ya Simba, lakini amefanikiwa kuchangia kuiingiza Simba nusu fainali,je akiaa miaka kama aliyokaa Chama, hatuoni kama ataisogeza mbele?
Leo hii mkifatilia taarifa za wachezaji wa Afrika kwa mwaka huu wa 2025 katika michuano hii ya shirikisho,hamuwezi kukosa jina la Ahoua
Jamani eeh kukosa magoli sio kutokujua kucheza,wachezaji wote duniani hukosa magoli.
Pamoja na yote Simba inaenda kuitoa Stellenbosch na kwenda kucheza Fainali.
Tazama video hapa chini.
View: https://vm.tiktok.com/ZMBnTQTPm/