Wanasiasa wetu wana nia ya kumkomboa mkulima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa wetu wana nia ya kumkomboa mkulima?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by enstein1, Aug 7, 2009.

 1. e

  enstein1 Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Naomba maoni ya wanajamii juu ya kauli ya naibu waziri wa wizara ya kilimo na usalama wa chakula wakati anazungumzia kitu wanacho kiita mapinduzi ya kijani yenye kauli mbiu mazao na kipato zaidi kwa mkulima wakati wa ufunguzi wa maonesho ya siku kuu ya wakulima yaani Nane nane huko Mbeya!! http://www.dailynews.co.tz/home/?n=3246&cat=home Kauli hii imenitia mashaka juu ya uwezo wa viongozi wetu kuona mbele na kutengeneza hatma ya taifa letu.

  Ni ushahidi wa wazi kuwa mafuta ya kawaida yaani (fossil fuels) kwa ajili kuendeshea magari na mitambo ya aina mbali mbali, yanazidi kutoweka katika uso wa dunia, kwa sababu mafuta haya huchimbwa ardhini kama madini mengine mfano Tanzanite, Almasi na kadhalika ambayo itafika muda yataadimika kabisa. Mafuta haya yamezidi kupanda bei siku hadi siku na hakuna budi kutafuta mbadala ili kuyafanya maisha yaendelee kama kawaida. Wataalamu wamegundua kuwa baadhi ya mazao ambayo yanaweza kustawi kwenye nchi za tropiki Tanzania ikiwa mojawapo. Mti mfano wa Mbono [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Jatropha"](Jatropha Curcus L.)[/ame] ambao si chakula, ni mti wa kudumu ambao mbegu yake hutoa mafuta yenye sifa za mineral diesel na hivyo ni mbadala mzuri wa nishati hii ambayo hutumika kwa mitambo muhimu kama Malori, Mabasi na Mitambo ya kufulia umeme!!


  Kwa Tanzania ambayo ni Hekta karibu 90,000,000 zinazofaa kwa kilimo na chini ya asilimia kumi (10%) ndiyo tuanaitumia sasa na kulima mazao ambayo hayajamkomboa mkulima wa Tanzania kwa miaka dahali!! Mazao ya nishati ingechukuliwa kuwa ni fursa nyingine ya kuwatafutia wakulima wa Tanzania kupata chakula na kipato zaidi kama wito ulivyo katika mapinduzi haya ya kijani.

  Naona waziri anajichanganya mwenyewe kwa kutoa kauli ambayo inapingana na mapinduzi ya kijani, na huenda hakufanya utafiti wa kina kwa kuona hali halisi ya nchi yetu na hatma yake kutokana na dhahma za nishati na badala yake alishikilia umbumbu ule ule wa kusikiliza wazungu wanasema nini?

  Ngoja nitoe mfano wa mkoa wa Rukwa, zaidi wilaya Mpanda, ni wilaya ambayo haina kabisa zao la kudumu la biashara, hali hii imewafanya wengi wa wakulima kugeuka watumwa wa ardhi yao kwa kuishi kwa shughuli zilezile kila mwaka pasi kupiga hatua katika maisha na kuishia kuzeeka na kufa masikini huku wakiwa na utajiri wa ardhi.

  Wilayani Mpanda kuna kampuni imejitokeza na kujenga kiwanda cha kukamua mafuta ya Mbono na mpango ni kuyasambaza wilayani humo na nchini kote Tanzania. Wakulima wanashauriwa kupanda miti ya Mibono (Jatropha) kwa kuchanganya na mazao mengine na katika wigo za nyumba na mashamba yao. Mbono imekuwa ni fursa muhimu kwa wilaya ya Mpanda kuwa na zao la kudumu la biashara, kama ilivyo kwa wilaya zingine maarufu kwa chakula kama Mbozi huko Mbeya ambayo ni maarufu kwa kutoa mahindi lakini pia huzalisha kahawa kwa wingi tu na kahawa si chakula kimsingi!! Sasa kwa dhana hii ya waziri ina maana kuwa mikoa ya chakula kama Mbeya, Iringa, Morogoro, Kigoma na Ruvuma isilime pia chai, pamba, tumbaku, kahawa na kadhalika? Kwa nini waziri asifike huko akajielimisha jinsi inavyofanyika Mpanda kabla ya kutoa kauli ya kuchanganya?

  Kauli za wanasiasa zinaheshimika sana, lakini zinapozua maswali kibao namna hii zinashusha sana hehima zao na kututia wasi wasi kama kweli huwa wanapata muda wa kufikiria mustakbari wa nchi yetu. Huenda hawajui hali halisi anayoishi mkulima wanayemzungumzia na athari anazozipata kwa kupanda kwa bei ya nishati isivyo kawaida!!

  Mi nilidhani waziri angeandaa elimu ya kilimo endelevu cha mazao ya nishati, na waziri wa nishati angetupa lengo la kupunguza utegemeyi wa mafuta ya Uarabuni walau kwa miaka kumi ijayo walau kwa asilimia!!

  Wanajamii naomba maoni!

   
 2. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,434
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Inawezekana nia wanayo lakini detail design ya wataalamu inkosekana zaidi wanasiasa wanadandia kwa mbele na zaidi wameshatangulia wao wataalamu wamelala.

  Manake wengine tuko vijijini huku bado hatujaona nini maana ya kumkomboa mkulima kama wakuu wanavyonadi. Manake kama mbolea bado hupatikanaji wake haumpi nafasi mkulima kupata, mbegu na pembejeo zingine bado hazipatiani kiivyo tukizungumzia utaalamu wa kilimo bado wataalaumu wako busy na semina na maboresho, mikopo haiendani na mahitaji ya mkulima tukizungumzia masoko baada ya soko hulia mkulima na amezidi kunyonywa kila kukicha na wachuuzi wananeemeka na serikali haina habari na wala haijui nini wajibu wake baada ya soko hulia.

  Sera ya kilimo bado ni msamiati mgumu sana sio tu kwa wakulima bali kwa watunga sera na wasimamizi na sera zenyewe zimebaki katika makablasha.
   
Loading...