Wanasiasa wetu ni wasomi au wana elimu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,410
38,702
Tangu Magufuli ateue Baraza la Mawaziri, kumekuwa na msisimko wa aina yake kwani baraza hilo limesheheni wasomi wengi waliobobea kwenye fani zao. Wasomi hao ambao wengi wana umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea ni wabobezi wasio tia shaka!

Lakini wengi wao walikuwapo kwenye nyadhifa mbali mbali kabla ya uteuzi wao wa kuwa Mawaziri. Wakati mwingine huwa linazuka swali linalotatiza sana watu wengi. Hivi hatuendelei kwa kuwa hatuna wasomi wa ngazi za Ubobezi kama nchi za wenzetu au mfumo wetu wa Elimu unaotoa wasomi tulio nao si timilifu!?

Wakati kama taifa nilishangazwa na watu hata wasomi wetu waliotafsiri kuwa Lowassa ana shahada ya Sanaa toka chuo kikuu cha Dar es salaam. Nilijiuliza tatizo ni lugha au ni uelewa wetu wa mambo? Kwa uteuzi wa Magufuli, Jee tatizo la nchi yetu ni kwamba hatuna wanasiasa wasomi au wanasiasa wasomi tulionao elimu yao ni tatizi?
 
Mtoa mada sijakuelewa unaposema '' walitafsiri kwamba lowasa Ana shahada ya sanaa''
 
Tatizo ni mfumo wa elimu kaka,wala sio kiwango cha elimu.Tuna maprof,doctors na Engineers wengi sana hapa nchini lkn Hatuoni michango yao...ndipo tunapojiuliza,hiv hii elimu ni ya kwenye vyeti tu?
 
Tatizo ni mfumo wa elimu kaka,wala sio kiwango cha elimu.Tuna maprof,doctors na Engineers wengi sana hapa nchini lkn Hatuoni michango yao...ndipo tunapojiuliza,hiv hii elimu ni ya kwenye vyeti tu?

Mbona hao maprofesa na madoctors walio wengi wamepata hizo masters na Phd s zao huko huko ulaya na USA mnakodai kuna elimu bora ? ?
 
Mtoa mada sijakuelewa unaposema '' walitafsiri kwamba lowasa Ana shahada ya sanaa''
Walitafsiri kwamba "Bachelor of Arts" ni shahada ya sanaa ya Uigizaji! Na ndiyo maana Lowassa alipokwenda Mbagala wakasema anatumia Elimu yake ya Sanaa aliyoisomea chuo kikuu cha Dar es salaam!
 
Walitafsiri kwamba "Bachelor of Arts" ni shahada ya sanaa ya Uigizaji! Na ndiyo maana Lowassa alipokwenda Mbagala wakasema anatumia Elimu yake ya Sanaa aliyoisomea chuo kikuu cha Dar es salaam!
Ni Bachelor of Arts in Theatre Arts mkuu. Yule mzee ni mtaalamu wa maigizo aliyebobea!
 
Mbona hao maprofesa na madoctors walio wengi wamepata hizo masters na Phd s zao huko huko ulaya na USA mnakodai kuna elimu bora ? ?
Elimu na Usomi ni vitu viwili tofauti kabisa ingawa vinategemeana. Usomi unatokana na kufaulu mitihani wakati Elimu ni uwezo wa kutafsiri maarifa uliyoyapata shuleni. Kwa mfano kama mtihani wa kupata shahada unahusisha swali la 2 + 2 =? basi kwa watakao kuwa wameelewa wataandika 4 na watakao kuwa wamekariri nao pia wataandika 4, na wote watakuwa wamefaulu na kutunukiwa shahada! Lakini mmoja atakuwa ni msomi tu na mwingine atakuwa ni msomi mwenye elimu.

Lakini Elimu ni uwezo wa kujua ile nadharia ya 2+2=4 unawezaje kuitumia katika maisha. Kwa mfano una vyumba viwili vya kulala na una wageni wanne wa Jinsia mbili tofauti wasio na mahusiano. Hapo Elimu ni kujua kwamba wageni wa kiume wawili watalala kwenye chumba kimoja na wale wa kike wawili watalala kwenye kingine kilichobaki. Kama utataka kuwalaza wote chumba kimoja au ukawachanganya bila ya kujali jinsia zao, basi wewe utakuwa ni msomi lakini usiyeelimika. Usomi usio na mantiki ni ukaririfu.

Wasomi wetu kwenye hili la kutafsiri kile walichojifunza shuleni ni shida sana, hata wawe wamesoma kwenye shule za nchi yoyote unayoijua wewe!
 
Walitafsiri kwamba "Bachelor of Arts" ni shahada ya sanaa ya Uigizaji! Na ndiyo maana Lowassa alipokwenda Mbagala wakasema anatumia Elimu yake ya Sanaa aliyoisomea chuo kikuu cha Dar es salaam!

Alaaaa kumbe, na mimi walivyo sema hivyo, nikadhani alisoma mambo ya uigizaji, maana Kuna kitengo hicho pale udsm. Kumbe ni BA. Duh.
 
Ni Bachelor of Arts in Theatre Arts mkuu. Yule mzee ni mtaalamu wa maigizo aliyebobea!
Hili jambo lilishajadiliwa humu na kutolewa ufafanuzi kwamba Lowassa amesomea Ualimu! Hata kwenye maelezo yaliyowahi kutolewa na waliosoma naye wanasema hivyo. Ila hakuna kumbukumbu kama kuna mahali au shule aliyowahi kufundisha!!
 
Mimi nadhani tatizo kuu la wanasiasa wetu au tuseme viongozi wetu ni UZALENDO........na uzalendo sio tu kusema kuwa wewe ni MTANZANIA bali unatakiwa uonyeshe kuwa wewe ni MTANZANIA na unaipenda TANZANIA kwa moyo wako wote na akili yako yote..........TANZANIA pamoja na matatizo katika mifumo yetu ya elimu lakini tumebahatika kupata wasomi mbali mbali waliobobea katika Nyanja mbalimbali za kielimu.......Lakini wasomi wetu hawa wachache wamegeuka wamachinga wa taaluma zao kwa ajili ya siasa.......Wanatumia taaluma zao zilizotokana na kodi za walalahoi na wakulima wachovu kuliangamiza taifa lao kwa manufaa yao binafsi na vibaraka wao........

Ni wasomi wetu hawa hawa wanaohusihwa na kashifa mbalimbali za wizi na ubadhilifu wa mali za umma....ni wasomi hawa hawa tuliowaamini na kuwapa ridhaa za kutuongoza ndio waliolitia taifa hasara kubwa kwa kuingia mikataba ya kifisadi na ya wizi kwa ajili ya matumbo yao yasiojua kushiba wala kuvimbiwa.......

Ni wasomi wanaotudanganya kwa kutuletea takwimu za uongo na kweli kuonyesha kuwa uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya roketi ilihali hali halisi ya maisha inazidi kuwa mbaya kwa waliowengi......Ni wasomi hawa hawa waliodiriki kutuambia kuwa tutakula nyasi ikibidi ili tu ipatikane ndege ya raisi......Ni wasomi hawa wanaoshirikiana na wawekezaji uchwara na kuhujumu rasilimali zetu......

Kwa maelezo hayo unaweza ukaona kuwa ni jinsi gani wasomi wetu walivyokosa uzalendo na kugeuka kuwa wachumia tumbo na watumwa wa wanasiasa.........

Wito wangu ni kwamba kila mwananchi anatakiwa aonyeshe UZALENDO kwa taifa lake
 
Mimi nadhani tatizo kuu la wanasiasa wetu au tuseme viongozi wetu ni UZALENDO........Wito wangu ni kwamba kila mwananchi anatakiwa aonyeshe UZALENDO kwa taifa lake
Huwezi kuwa na uzalendo kama huna Elimu. Kama wewe ni msomi lakini huoni umuhimu wa kizazi kijacho kufaidika na ulichosoma shuleni zaidi ya familia yako, basi jua kuwa wewe huna elimu, kwani kama una elimu utajua tu kwamba hiyo familia yako inategemea familia zingine ili kuweka jamii indelevu! mwenye duka la thamini ya milioni 100 haitaji kuwa na mteja wa kununua vitu vya shilingi milioni 100 bali wa chini ya hapo. Kwa ivo uzalendo ni Elimu!!
 
Ninapotaja uzalendo ninamaanisha kuwajibika kwa TAIFA lako......UZALENDO uwe wa kwanza kwa kuwa kupitia kwayo ndio utajua thamani ya elimu yako kwa taifa lako na kupitia huo uzalendo ndio majukumu kwenye taifa lako kama kiongozi.......
 
Siwezi kujua ni kitu gani kinachoendelea ndani ya akili ya JPM, lakini wasomi wengi wamekuwa wakishindwa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa sababu ya kuingiliwa na siasa. Unakuta mkurugenzi wa manispaa ana PHD lakini anafanya kazi na diwani mwenye elimu ya darasa la saba, hapo hakuna uwiano wa fikra za kikazi. Nadhani kuwa JPM ameamua kuwajaza wasomi huku akiandaa mazingira ya elimu zao kuwa na faida ya moja kwa moja kwa maisha ya mtanzania wa hali ya chini. JPM alishawahi kusikika akiongelea uhusiano wa kikazi kati ya mainjinia wa wizara ya ujenzi na wakuu wa wilaya na mikoa ambao shule zao ni ndogo. Naamini wasomi wengi wakipewa uhuru wa kufanya kazi bila ya kuingiliwa na urasimu mwingi tulionao, wataweza kufanya mapinduzi makubwa ya kimaendeleo. Paul Kagame wa Rwanda ameweza kuwatumia wasomi kwa faida ya uchumi wa Rwanda, kwanini sisi tushindwe?.
 
Tangu Magufuli ateue Baraza la Mawaziri, kumekuwa na msisimko wa aina yake kwani baraza hilo limesheheni wasomi wengi waliobobea kwenye fani zao. Wasomi hao ambao wengi wana umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea ni wabobezi wasio tia shaka!

Lakini wengi wao walikuwapo kwenye nyadhifa mbali mbali kabla ya uteuzi wao wa kuwa Mawaziri. Wakati mwingine huwa linazuka swali linalotatiza sana watu wengi. Hivi hatuendelei kwa kuwa hatuna wasomi wa ngazi za Ubobezi kama nchi za wenzetu au mfumo wetu wa Elimu unaotoa wasomi tulio nao si timilifu!?

Wakati kama taifa nilishangazwa na watu hata wasomi wetu waliotafsiri kuwa Lowassa ana shahada ya Sanaa toka chuo kikuu cha Dar es salaam. Nilijiuliza tatizo ni lugha au ni uelewa wetu wa mambo? Kwa uteuzi wa Magufuli, Jee tatizo la nchi yetu ni kwamba hatuna wanasiasa wasomi au wanasiasa wasomi tulionao elimu yao ni tatizi?
Siyo hatuna wabobezi na wala siyo elimu yetu ni finyu. I can prove wasomi Wahandisi ambao hapa kwetu walionekana si lolote si chochote, lakini baada ya kwenda Botswana,wanafanya mambo makubwa. Naamini na taaluma au tasnia zingine ni the same. Huwa mara nyingi nawatumia wataalam wetu mahiri kama Tido Mhando,Prof Tibaijuka na Mzee Omar Nundu kama sample ya watu ambao ni Watanzania waliodeliver sana huko nje lakini kilichotokea baada ya kuja nchini sote tunakijua.
Hivyo tatizo ni mifumo yetu ya kiuongozi, kiutendaji ni mibovu!
 
Ninapotaja uzalendo ninamaanisha kuwajibika kwa TAIFA lako......UZALENDO uwe wa kwanza kwa kuwa kupitia kwayo ndio utajua thamani ya elimu yako kwa taifa lako na kupitia huo uzalendo ndio majukumu kwenye taifa lako kama kiongozi.......
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja. Lakini kujua thamani ya elimu uliyo nayo kwa faida ya taifa si ndiyo elimu ninayoisema!? Kama mtu hana utambuzi wa wapi aliposimama anaweza kujua kama anakwenda mbele au anarudi alikotoka? Huwezi kuwa Mzalendo kama hujui faida ya kimaadili ya kuwa mzalendo. Kama taifa tunaangalia zaidi faida ya kuwa na mali kuliko faida ya kuwa na maadili ndiyo maana uzalendo umepungua!!
 
Ndugu Mleta Mada...

Heshma kwako zitangulie.
Mimi upande wangu WASOMI wetu wengi wana ma degreee na PHDs, Lakini bado hawajaelimika..

Kama nikikunukuu msomi aliye elimika ni tofauti na msomi aliyekariri kupass..
Wengi wetu tunaojiita wasomi ni mizigo ndio maana tunalalamika kila kukicha na kukosoa bila kuonyesha njia..

Tuamke tuelimike kwakutumia usomi wetu tulete mabadiliko kwa Taifa Letu...
 
Hili ni tatizo kubwa kwa wa africa na sio tanzania tu sababu kubwa ni mila , desturi na utamatuni. Vinasababisha tuwe wabinafsi na wapenda mali ili tupate heshima. Wenzetu wanatumia usomi wao kusaidia na kubadilisha mambo dunia ili wapate kueshimiwa na kukumbukwa .
 
Back
Top Bottom