Wanasiasa wetu na vita dhidi ya wazee

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
3,864
4,095
Rais ametoka kauli ya kutokuwa na imani na wazee,
Kuwa ndio wameifikisha nchi hapa kutokana na wizi na ufisadi pia.
Na baadhi ya viongozi pia wamekuwa wakiwatuhumu wazee
Je,ni kweli sasa utu uzima sio dawa? Na uzee ndio jalala?
Wazee sasa hawana thamani wala hawaaminiki tena,hivyo watuachie vijana tujenge taifa?
Ama ni upotofu tu wa wanasiasa wetu,lakini wazee bado ni muhimu.
 
Mzee anaanzia miaka mingapi?
Magufuli hajui history ya tanzania:

Vijana wakiongozwa Na Nyerere at 39 yrs age ndiyo waliongoza nchi kwa mara ya kwanza Wengine wengi walikuwa chini ya umri wa Nyerere. Hawa ndiyo wameleta yote tuliyonayo leo
 
Mimi sijapenda kauli hii kuwatuhumu wazee moja kwa moja sababu hata sisi vijana tunaelekea kwenye uzee
 
Kama wazee wameiba, basi hawajaiba uzeeni, waliiba katika ujana wakati wanaongozwa Na shinikizo kubwa la kutaka kuishi kisasa(kwa wakati Wao), kumiliki mali nyingi, nyumbandogo na michepuko nk. Hivyo hulka ya tamaa kubwa ipo katika umri wa ujana!, na njia pekee ya kukabiliana na ufisadi na rushwa ni kuwa sheria zenye afya nzuri na usimamizi wa dhati!, mzee Warioba aliliona hili akasisitiza maadili kuwa sheria, akagomewa na makofi juu, wakalazimisha yabaki kuwa miiko!, leo tunaaminishwa ujinga eti maadili yamilikiwa na vijana(ambao hata kazi tunatafuta kwa rushwa).
 
Vijana na wao watakuwa wazee siku moja mbaya zaidi hawatopenda vijana washike madaraka kimsingi wazee ndio wenye hekima maana washayaona hivi kweli kijana kwa watu kama economic hit men tutatoka kweli?badala ya kuboresha maslahi ya watumishi wote tunaboresha ya viongozi sasa kila mtu anapenda kuongoza kwa nini tusichague viongozi kutoka na michango yao iliyotukuka katika jamii?vijana ni wakutumwa kazi wajifunze maarifa ya dunia hii ili siku moja wawe viongozi wazuri
 
Rais ametoka kauli ya kutokuwa na imani na wazee,
Kuwa ndio wameifikisha nchi hapa kutokana na wizi na ufisadi pia.
Na baadhi ya viongozi pia wamekuwa wakiwatuhumu wazee
Je,ni kweli sasa utu uzima sio dawa? Na uzee ndio jalala?
Wazee sasa hawana thamani wala hawaaminiki tena,hivyo watuachie vijana tujenge taifa?
Ama ni upotofu tu wa wanasiasa wetu,lakini wazee bado ni muhimu.
Wazee wanaomba rushwa na wako slow sana kufanya maamuzi.

Wapumzike
 
Nayeye mwenyewe Akiwemo inchi imebaki na aman miaka yote hiyo na wazee wetu ndio walioipigania na uzalendo wa kutosha leo hii tunawaona hawafai? Umasikin huu umeletwa na serikal ya ccm awaache wazee wapumzike kwa aman na kula pension zao hata hivo wapo walio itumikia vyema inchi na mafao hawajalipwa hatuna haja ya kuangalia nyuma tena amepewa inchi sasa ni wakati wakutuletea maendeleo tu aachane na tuhuma na kuwalaumu watu hata hivyo naona amekua muongeaji sana huku sioni unafuu wa maisha Vitu vinazid kupanda bei pesa nayo haionekan
 
Anawaogopa wazee sababu wana misimamo, mf. Maalim, Lowassa, Kingunge, Sumaye.
Mtu mzima hatishiwi nyau. Yeye anataka kufanya kazi na wanaomtetemekea.
 
Mtajua wenyewe bwana!Msitusumbue na hamtaki kupiga kura hamtaki kufanya usafi kutwa kushinda kwenye mitandao tu huku kulalamika na kukosoa fanyishweni kwa nguvu tu maana hakuna namna nyingine!eeeeh.
 
Magufuli hajui history ya tanzania:

Vijana wakiongozwa Na Nyerere at 39 yrs age ndiyo waliongoza nchi kwa mara ya kwanza Wengine wengi walikuwa chini ya umri wa Nyerere. Hawa ndiyo wameleta yote tuliyonayo leo
pamoja na umasikini tulionao, au?
 
Collective accusation.
Sote ni wazee watarajiwa ( kama tutajaaliwa kuishi miaka mingi).
 
atafanyakazi na vijana hatateua wazee,Mtoto wa mkulima mkuu wa chuo kikuu, Ana Makinda mwenyekiti wa tume, hawa nao ni vijana?
 
Back
Top Bottom