Wanasiasa wetu na udandiaji wa matukio

Wanasiasa wetu na udandiaji wa matukio

Shagiguku

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
409
Reaction score
138
Ndugu zangu Great Thinkers leo tena napenda tushee/tushirikiane juu ya jambo hili ambalo nimekuwa nikiliona kwa muda mrefu likifanywa na wanasiasa wetu. Na hapa naomba niunguze sauti na kunong'ona kidogo kwa chini chini "WANASIASA WETU HAPA TANZANIA WANATABIA YA KUDANDIA MATUKIO NA KUTOKUYAFIKISHA MWISHO.""

Hali hii ya kudandia matukio unaweza kuiona katika mifano mingi tu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea hapa nchini lakini hawaendi nayo hadi mwisho wake na kutuletea matokeo ya "mdandio wao" katika tukio husika.

Kwa mfano:

1. Baada ya "baadhi" ya wana nchi wa ntwara kuandamana kuhusu suala la gesi, tuliona baadhi ya wanasiasa wetu wakilidandia tukio hilo, lakini kabla hatujafika nalo mbali tayari wamekwisha liacha na sasa wamedandia tukio jingine.

2. Kwa sasa wanasiasa wetu wamedandia tukio la wanafunzi kufeli mitihani na baadhi yao wanaonekana kufurahia watoto wa taifa hili kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho, tumesikia baadhi wanataka kuitisha maandamano ya nchi nzima kwa wanafunzi waliofeli (ili iweje hapo kwa kweli mimi sifahamu) lakini ninachofahamu kwa uhakika ni kwamba watafanikiwa kuwaandamanisha hao watoto (kama kibari cha maandamano kitatolewa na jeshi la serikali yetu "sikivu") kwa sababu hao watoto ni "innoncent" wanaotumiwa tu kama kon****.d...&&&&..m ya kiume na kutupwa baada ya shughuli na tena kwa sababu ni "teenagers" basi wanafuaata ile inayoitwa na wasomi "mob-psychology" lakini nyuma ya pazia baada ya maandamano hayo ya "WANAFUNZI WALIOFELI NA WANASIASA WALIOFELI" ukimchukua kijana mmoja ukamuuliza "Hivi kwa nini ulikuwa unaandamana leo.....!!!!????" kwa hakika hatakupatia jibu ambalo linathibitisha uhalali wa kuandamana kwake.

3. Hapo siku za nyuma wanasiasa wetu walidandia na kushabikia tukio la mgomo wa madaktari, ambalo kwa sasa lipo likizo na muda si mrefu litarejea kazini kwa maana wanasiasa wetu wamefeli kulitatua.

4. Lakini pia kuna kipindi wanasiasa wetu walidandia tukio la kuzama kwa meli "zetu" katika bahari ya hindi, ambalo mwisho wake kupitia wanasiasa hatukuona kwa maana tayari walikuwa wamEFELI hata kabla ya kulidandia na kulishabikia tukio lenyewew.

5. Ikumbukwe pia kwamba kumekuwa na kawaida ya kudandia na kushabikia kuwataka wahusika katika tukio fulani lililotoke WAJIUZURU nyazifa zao ili kuonesha uwajibikaji wao, jambo ambalo hatujaona mtu akijiuzuru kwa sababu wanasiasa wetu wameFELI katika uwajibikaji, lakini pia hata hao wanao wataka wenzao wajiuzuru nyazifa zao nao pia waMEFELI kwa kuwa tukiwaendea kwa undani ndani ya vyama vyao kuna madudu mengi sana ambayo wameyafanya na wanaendelea kuyafanya lakini hawataki kujiuzuru ili kuonesha mfano wa uwajibikaji kwa vitendo kwa maana hiyo na wao pia WAMEFELI kabla hata ya kuwataka wenza wajiuzuru.

6. Na sasa wanasiasa wetu wanataka kuwaandamanisha watoto wetu WALIOFELI form four kwa sababu tayari wao wanasiasa wetu hawa WAMEKWISHA KUFELI tayari kabla hata hayo maandamano hayajaanza kwa sababu hili suala hawatakwenda nalo hadi mwisho wake na kutuonesha sisi waNANZENGO "athari - positive or negative" ya maandamano yao wao na watoto wa taifa hili.

7. Zaidi ya yote wametega masikio wakisubiria tukio jingine litokeee hivi karibuni ili walidandie na kulishabikia kwa kuwa hawa wanasiasa wetu WAMEFELI kuzungumzia ishuzi za nguvu juu ya taifa letu hili na mwisho wa siku wamekuwa wakirumbana juu ya hoja na maisha binafsi ya mtu kana kwamba sisi wananzengo maisha ya mtu binafsi yana tija kwetu. Utawasikia flani hakumaliza form six, flani alisoma cho kikuu cha kise.....n***&&&g...e%%%%m...a huko wapi sijui, au huyo ni masalia tu amehama huku anatafuta ulaji huko nk nk
Hali hii yote inasababishwa na wanasiasa wetu hawa KUFELI kutafuta na kujenga hoja zenye mashiko juu ya mstakabari wa taifa letu hili tuliloachiwa na MWALIMU JK ORIJINO.

8. Hapa sijazungumzia tukio la kikombe cha babu kule Loli, mauwaji na uchomaji wa makanisa baina ya waislamu na wakristo huko zanzibar, buseresere na kwingineko.

NDUGU YANGU GREAT THINKER UNAWEZA KUONGEZEA PIA NA WEWE TUKIO AMBALO UNAONA WANASIASA WETU WALILIDANDIA LAKINI KABLA HALIJAKWISHA WAKAACHANA NALO NJIANI.

Napenda kuwasilisha.

Nakala kwa:
1. Wanasiasa wetu - kwa taarifa.
2. Great thinkers wote - kulingalia suala la udandiaji wa matukio kwa upana wake
3. Moderator - tafadhari usiitupe kapuni hii thread.
 
Rangi ya gamba lililoshindikana kujivua hili HATA MAWAZO YAKIMAGAMBA PIA, AU NI BWANA MAENDELEO!?
 
Back
Top Bottom