Wanasiasa watupe strategies namna watakavyo tatua matatizo sio ahadi

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
381
261
Imefika muda sasa wanasiasa wawe wazi kwa kila tatizo,chanzo cha tatizo na walink sera za vyama vyao na vision/mission na objective zao watakavyotekeleza ahadi wanazotupa. Wanatuahadi watakuza elimu,afya,uchumi na maisha bora kwa kila mtanzania.
Watanzania waleo si wakupewa ahadi za maneno,tunataka watueleze kinaga ubaga watatutatulia vipi matatizo hasa ya msingi.Mwl Nyerere alitambua wazi maadui wakubwa ni ujinga,maradhi na umaskini. Ujinga alileta elimu ya watu wazima,umaskini alileta siasa ya kilimo cha ujamaa na kuanzisha viwanda na afya alitibu bure.
Maadui wa leo ni rushwa,ufisadi na umaskini kwa watanzania,watupe plan hata kwa waraka tuusome ili tuwaelewe sio ahadi za majukwaani.
Watanzania tuwe waelewa japo kwa elimu ndogo tuliyonayo lakini hata mie imeniwezesha kujua vision,mission,objective(smart) na plan of action. Najua nimetumia hiyo lugha ya kimombo sio kwamba naifahamu ila ndivyo nilivyofundishwa na kwa uelewa wangu mdogo,wanasiasa wasituburuze. Kama hali ya sasa iko hivi,je kwa vizazi vijavyo vyetu watakuwa wageni wa nani?
Watanzania tusidanganyike kwa ahadi ambazo hazitekelezeki,ni bora watuambie tutatatua matatizo haya machache kwa kuwa tuna kiasi hichi cha fedha zetu kidogo si ahadi tele fedha hatuna. Ni jambo ambalo haliingii akilini wabunge kukaa Bungeni miezi kupitisha bajeti isiyo na fedha na matokeo yake tumekosa fedha ya kuitekeleza na mkuu wa nchi kuishia kuwa omba omba ili kuokoa jahazi.
Tuweke uzalendo kwanza,tuangalie kesho si mlo wa leo kesho hatuji tutakula nini?
Tuchambua mambo critically,Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu tusitengwe kwa vyama,dini na ukabila kwa maslahi ya nchi.Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom