PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
"Wanasiasa 'wangu' imara, bora, jasiri katika orodha ya wanasiasa 10 kwa mwaka 2016"
1. GODBLESS JONATHAN LEMA,
~ huyu ni mbunge wa Arusha mjini, mwamba, jasiri, asiyetetereka, huyu amekumbana na changamoto hasi nyingi katika ubunge wake.., siyo kwamba tu amefanikiwa kuingia katika 'nyoyo' za watu wa Arusha, hapana, ndiye mbunge aliyepata umaarufu mkubwa sana katika mkutano wa 5 wa bunge la 11, ingawa katika mkutano huo wa 5 (mwezi Novemba) hakuwepo bungeni., hadi sasa yuko gerezani, Kisongo, Arusha akipigania dhamana yake.., ni mtu jasiri haswaa, anasimama kwenye kweli yake.., asiyeogopa kusema dhamira yake bila kujali nani ataumia na nani atafurahi.., Lema is the Man!
2. TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU;
~ huu ni mwamba haswaa, Mbunge kutoka jimbo la Singida Mashariki (mbunge), huyu amefanikiwa haswaa kutekeleza wajibu wake kama mwanasheria mkuu wa chama chake (CHADEMA), ni msaada mkubwa wa idara ya sheria katika chama chake, amepambana na kesi ngumu na kubwa sana kwa Mwaka huu., ikiwepo kesi maarufu nchini inakwenda kwa jina la 'Dikteta - uchwara'., (ipo hadi sasa), huyu pia ni mbunge wa pili kwa kusumbuliwa na jamhuri (kwa kukamatwa na kuhojiwa), yeye na Lema wamekamatwa, wamehojiwa na kuwekwa lupango kuliko wanasiasa wote nchini kwa mwaka 2016.
3. HUSSEIN MOHAMMED BASHE
~ ni mbunge wa Nzega mjini, anatoka chama kinachoongoza dola (chama ambacho wabunge wake bungeni kazi yao ni kupiga makofi na vigelegele tu), ni nadra sana kuona mambo ambayo yanafanywa, yanazungumzwa na Bashe (kama yanaweza kutoka katika vinywa vya wanasiasa wa chama chake), mwaka huu amewasilisha bungeni hoja binafsi iliyokusudia kuliomba bunge kujadili na kupitisha Azimio la kuitaka serikali kuunda tume ya kitaalamu (PPCE) ya kufanya mapito ya mfumo wa elimu nchini.., mtu makini sana.
4. BEN-RABIU WA SAANANE;
~ huyu ni kijana, mwanachama wa CHADEMA, amewahi kuhudumu katika nafasi kadhaa katika chama hicho, ni msomi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa., mwaka 2016 amefanya kazi kubwa, haswa alipoendesha zoezi kubwa sana la kuhoji elimu ya Rais kwa mantiki, vigezo, hoja na akili kubwa, alifanikiwa kupata uungwaji mkono mkubwa sana katika kampeni yake hiyo., na maswali yale (kutoka kwa Ben) hayakuwahi kujibiwa kwa hoja na wahusika.., kwa sasa Saanane haonekani baada ya kutoweka tangu 8-11-2016, hajulikani alipo.., ni kijana jemedari sana, mpambanaji na asiyeshindwa na kitu kwa urahisi..,
5. JOSEPH LEONARD HAULE;
~ huyu ni mbunge wa Mikumi, jimbo hilo ni moja kati ya majimbo katika mkoa wa Morogoro, ni mmoja kati ya wabunge wakiokutana na changamoto nyingi hasi katika jimbo lake, mafuriko, migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji (ukizingatia hii ndiyo mara ya kwanza kuingia katika siasa rasmi).., amejitahidi kupambana na changamoto hizo, na amefanikiwa sehemu kubwa, ingawa bado kuna changamoto kubwa sana ya migogoro ya wakulima na wafugaji.., ni mmoja kati ya wabunge waliochangia na kuuliza maswali mengi katika bunge la mwaka 2016..,
6. EDWARD NGOYAI LOWASSA;
~ huyu ni mwanachama wa CHADEMA, mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, mwanasiasa mkongwe, mmoja kati ya viongozi, wanasiasa wenye Mvuto na ushawishi miongoni 'mwa' wanasiasa wa nchi hii.., baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2015, amefanikiwa kutulia kwenye chama chake, anafanya siasa tofauti na watu wengi walivyofikiri (kwamba huu ndiyo mwisho wake wa kisiasa, baada ya kuhama CCM), amefanikiwa kufanya siasa ya ardhini katika majimbo na kanda nyingi kwenye oparesheni ya chama hicho inayoitwa 'CDM ni msingi'.., ameifanya hiyo kazi kwa weledi mkubwa sana, ni mmoja kati ya wanasiasa ambao wana hekima, uvumilivu, wasiokuwa na kinyongo, ghilba na majivuno.., kuna mengi ya kujifunza na kusema kutoka kwa Lowassa..,
7. ESTHER AMOS BULAYA;
~ huyu ni mwanamke wa shoka, huyu ni jemedari, amekuwa katika siasa za ushindani kwa muda mrefu, amekuwa mkosoaji mzuri sana wa dola hata wakati yupo katika chama dola (CCM).., alihama ba kujiunga na upinzani.., katika uchaguzi mkuu wa oktoba 2015 akafanikiwa kuangusha mbuyu na jabari wa siasa za nchi hii, Steven Masatu Wassira.., Wassira hakutaka kukubali kushindwa, akakimbilia kufungua kesi ya uchaguzi katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza, (kesi ikawa inasikilizwa katika halmashauri ya manispaa ya Musoma).., kesi ilikuwa ya moto.., lakini mwisho wa siku, Esther Bulaya alifanikiwa tena kumgaragaza Wassira katika maamuzi ya mahakama.., ni mwanamke jasiri, katika bunge hili la 11 ni mmoja kati ya wabunge waliofungiwa kisa kuhoji kwanini Bunge siyo mubashara kupitia TBC..,
8. SEIF SHARIF HAMAD (MAALIM);
~ huyu ni katibu mkuu wa Civic United Front (CUF) chama cha tatu kwa ukubwa nchini kwa rasilimali watu na nyadhifa za kisiasa, huyu alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Zanzibar.., aliongoza chama chake kususia marejeo ya uchaguzi wa pili baada ya uchaguzi wa awali kufutwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, Maalim anaamini alishinda uchaguzi wa awali, hivyo hakuona haja ya kushiriki uchaguzi wa marejeo.., huyu ni mwanasiasa mkongwe wa siasa za Zanzibar, amekwivaa kweli, kwa mwaka 2016 nilipenda namna alivyoweza kulibeba suala la Zanzibar katika medani za kimataifa, na pia bila kuhatarisha usalama na utulivu wa Zanzibar.., ni mtu ambaye alikuwa ameushikilia usalama wa wakati ule na utulivu wa wafuasi wake.., nampongezi kwa hilo.., ni mtu ambaye ni sura ya CUF, wanajivunia kuwa na mtu kama huyu!
9. ZITTO ZUBEIRY KABWE;
~ huyu ni kiongozi mkuu (mfalme) wa chama cha cha ACT-wazalendo, ana jina lake maarufu sana anaitwa 'AYATOLLAH' wakimfananisha na yule 'mtawala mwenye cheo kikubwa katika taifa la Iran' yaani 'Supreme Leader of Iran', Zitto amefanikiwa kuongoza halmashauri yake ya Kigoma ujiji kwa mafanikio makubwa sana, kuna mengi yamefanyika chini ya halmashauri hiyo, ambayo iko chini ya chama chake.., Zitto katika bunge hili la 11 amefanikiwa kujenga hoja kubwa (2) na nikazielewa sana, katika mjadala wa TBC kurusha matangazo ya bunge na pia katika mjadala wa wizara ya viwanda na biashara.., lakini Zitto amekwama katika suala la uongozi wa chama chake, ameshindwa kuvuna wanachama wapya na amepoteza wanachama wengi, tena wenye majina makubwa..
10. JOSHUA SAMUEL NASSARI;
~ huyu ni mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki katika mkoa wa Arusha, mmoja kati ya wabunge wachache ambao katika majimbo yao ya uchaguzi wananchi wanatamani awe mbunge wa maisha, Mbunge wa wakati wote.., Nassari amefanikiwa kufanya mambo makubwa sana katika jimbo la Arumeru Mashariki.., ametoa ambulance, ametoa msaada wa visiwa, ameshiriki katika tatuzi za migogoro ya ardhi, amewawakikisha wananchi wake jimboni na pia wakati huo yuko katika masomo yake nje ya nchi.., ni mbunge kijana sana, wakati ule anaingia bungeni kwa mara ya kwanza alipewa jina la 'Dogo Janja'.., Nassari sifa yake kubwa yuko tayari kushirikiana hata na shetani kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Arumeru Mashariki.., ni mbunge wa kupigiwa chapuo haswa..,
.., hii ni orodha ya wanasiasa 10 bora (kwa mwaka 2016) kati ya orodha ndefu ambayo niko nayo hapa.., nimejitahidi kueleza dhima, muktadha na sifa Shawishi za kwanini hawa ni bora 10 kati ya wale wengi (kwangu).., huu utakuwa ni utaratibu wangu wa kila mwaka na kila mara kuleta orodha hii.., ahsante!
Mwananchi wa kawaida,
Martin Maranja Masese (MMM)