abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Written by mkulima // 30/03/2011 // Habari // No comments
http://www.mwananchi.co.tz/componen...uZ3VsaXdhLXR1bWUteWEta2F0aWJhLW1weWEuaHRtbA==Tuesday, 29 March 2011 21:20//
Mwandishi Wetu
MUSWADA maalumu wa kuunda Tume ya kukusanya maoni na kupendekeza muundo wa Katiba mpya ya Tanzania, unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Aprili, mwaka huu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa muundo wa tume hiyo hautawashirikisha wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani wala kiongozi yeyote wa kisiasa.
Tume hiyo inayotarajiwa kuwa na wajumbe 30, itaundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na wajumbe wake watakuwa ni wanataaluma, hususan wanasheria na kwamba suala la jinsia litazingatiwa.
Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa Tume itaundwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani na inatarajiwa kuwa na majukumu mbalimbali ikiwamo kuwahamasisha watu kujua maana na muundo wa Katiba.
Majukumu mengine ya tume hiyo yaliyotajwa kwenye muswada huo ni kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuchunguza na kuainisha muundo wa Katiba kulingana na mifumo ya kisiasa, kidemokrasia, uongozi, sheria za kiutawala na Serikali.
Mara baada ya Bunge kupitisha muswada huo, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuusaini na kuiunda haraka iwezekanavyo tume hiyo ili ifikapo Juni mwaka huu ianze kazi yake.Kamati hiyo itatoa rasimu ya katiba hiyo mpya ikipendekeza pia muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utakavyokuwa.
Mchakato wa kuunda tume hiyo unakuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wananchi kuwa watulivu akisema suala hilo litaratibiwa kwa umakini ili kuwa na katiba bora ambayo itawasaidia Watanzania kwa muda mrefu.
Tamko la Rais Kikwete la kuunda tume hiyo ndilo lililozima wimbi la madai ya Katiba mpya lililoshika kasi miongoni mwa watu wa kada mbalimbali ikiwamo wanasiasa, wasomi na wananchi wa kawaida.Katika mijadala hiyo, Katiba iliyopo imeelezewa kuwa imepitwa na wakati na haiendani na mahitaji ya mazingira ya sasa ya nchi.
Vuguvugu hilo lilianza mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Novemba mwaka jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai kuwa Katiba ya sasa haitoi haki ya kidemokrasia kwenye uchaguzi.
"Wanasiasa waenguliwa Tume..." kwani walikuwemo kwenye Tume?Wanasiasa waenguliwa Tume
Hili la wanasiasa kutokuwepo limekaa kisiasa zaidi hata zitolewe sababu zipi.nguzo za maendeleo kwa mujibu wa azimio la arusha(kama sikosei) ni watu,ardhi na siasa safi.kuna mambo ya kisiasa lazima kundi lao lihusike direct maana wapo wanasiasa wanasheria n.k.fatilia uteuzi wa hao wataalam kama hujakuta wote wanakadi za ccm!Kwa maana hiyo Tume itawajibika kwa raisi, au?
Kwani hoja ya katiba mpya ilianzishwa na wanasheria? Wanasiasa lazima wawepo. Hatutaki changa la macho.
Kinachojadiliwa hapa ni Katiba ya MUUNGANO, Muungano ni wa sehemu mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar ili kutenda haki ni lazima iwe hivyo. Katiba iliyopo ndio inayopigiwa kelele kua haitendei haki upande mmoja,pia hao wajumbe wataangalia pande wanazotoka kuona mahitaji/maslahi/mapungufu ya kila upande. Kumaliza matatizo ni lazima pande mbili zilizoungana zikae upya kujadili aina ya muungano/katiba utakaonufaisha pande zote.kama idadi sawa zanzibar in wakazi wangapi na bara in wakazi wangapi?
Kwa maana hiyo Tume itawajibika kwa raisi, au?
Tuesday, 29 March 2011 21:20
Mwandishi Wetu
MUSWADA maalumu wa kuunda Tume ya kukusanya maoni na kupendekeza muundo wa Katiba mpya ya Tanzania, unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Aprili, mwaka huu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa muundo wa tume hiyo hautawashirikisha wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani wala kiongozi yeyote wa kisiasa.
Tume hiyo inayotarajiwa kuwa na wajumbe 30, itaundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na wajumbe wake watakuwa ni wanataaluma, hususan wanasheria na kwamba suala la jinsia litazingatiwa.
Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa Tume itaundwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani na inatarajiwa kuwa na majukumu mbalimbali ikiwamo kuwahamasisha watu kujua maana na muundo wa Katiba.
Majukumu mengine ya tume hiyo yaliyotajwa kwenye muswada huo ni kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuchunguza na kuainisha muundo wa Katiba kulingana na mifumo ya kisiasa, kidemokrasia, uongozi, sheria za kiutawala na Serikali.
Mara baada ya Bunge kupitisha muswada huo, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuusaini na kuiunda haraka iwezekanavyo tume hiyo ili ifikapo Juni mwaka huu ianze kazi yake.Kamati hiyo itatoa rasimu ya katiba hiyo mpya ikipendekeza pia muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano utakavyokuwa.
Mchakato wa kuunda tume hiyo unakuja baada ya Rais Kikwete kuwataka wananchi kuwa watulivu akisema suala hilo litaratibiwa kwa umakini ili kuwa na katiba bora ambayo itawasaidia Watanzania kwa muda mrefu.
Tamko la Rais Kikwete la kuunda tume hiyo ndilo lililozima wimbi la madai ya Katiba mpya lililoshika kasi miongoni mwa watu wa kada mbalimbali ikiwamo wanasiasa, wasomi na wananchi wa kawaida.Katika mijadala hiyo, Katiba iliyopo imeelezewa kuwa imepitwa na wakati na haiendani na mahitaji ya mazingira ya sasa ya nchi.
Vuguvugu hilo lilianza mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Novemba mwaka jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kudai kuwa Katiba ya sasa haitoi haki ya kidemokrasia kwenye uchaguzi.
My Take: Nionavyo mimi ni kweli wanasiasa wanatakiwa wakae pembeni wasiingilie mchakato wa katiba mpya.Wanasiasa wanatakiwa washiriki mchakato wa katiba mpya kwa kutoa maoni na pia uwahamasisha wananchi watoe maoni kwa Tume ya Katiba.Hii itasaidia mchakato wa Katiba mpya uende haraka na Katiba mpya ipatikane kabla ya 2015.
Mkuu hivi na wewe kama great thinker kweli umeingia kwenye huu mkenge na mchezo wa kunguni kutoka juu ya shuka kujificha chini ya shuka?. Huu ni mchezo wa kitoto ambao CCM wanataka kuucheza ili kulinda masilahi yao. Huwezi kusema wanasiasa wasiwemo wakati wateuzi wa tume hiyo ni wanasiasa tena wote wa kutoka CCM. Hakuna jipya hapa kama mteuzi ni Mwanasiasa tume hiyo itakuwa answerable kwa mwanasiasa na hakuna mtu atakayekuwa tayari kuteua watu ambao hana imani kuwa watamlindia masilahi yake. Kinachotakiwa kufanyika hapa zaidi ya hili changa la macho ni.
Ilitakiwa Muswada upelekwe bungeni wa kutaka tume hiyo iundwe na
1. Mwakilishi wa kila chama chenye mbunge mmoja au zaidi bungeni
2. Kila taasisi ya dini yaani waislam na wakristo watoe wawakilishi wawili wawili
3. TANGO, au umoja wa NGO utoe mwakilishi mmoja
4. Taasisi za elimu ya juu za serikali zitoe wawakilishi wawili
5. Taasisi za elimu ya juu za binafsi zitoe mwakilishi mmoja
6. Serikali ya Jamhuri itoe wawakilishi wawili na ya Zanzibar wawili
Kazi za hii tume ambayo katika muswada huo na budget yake iwekwe kabisa itakuwa ni
1. Kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa tume miongoni mwao ambao kazi zao hazitakuwa beyond organising public hearings na kukusanya maoni ambapo baada ya kila mkutano kila mjumbe anapewa kopi yake na kazi ya katibu ni kuwa na maoni yote kwa muda wowote na wakati wowote electronically, I mean kwenye video na muhtasari kwenye hard copy.
2. Tume hii iwe huru kuajiri wanasheria na wataalam waliobobea katika fani mbalimbali katika kuhakikisha kuwa kazi yao inaenda vizuri wakiwemo wa kisheria, IT, fedha etc.
3. Kuyaunganisha mawazo ya wananchi wote na kuyafanyia tathmini ili kuondoa yanayopingana na kisha kuchapisha rasimu yake kama katiba na kuirudisha tena kwa wananchi kuijadili kwa totality na kuongeza ama kufanyia marekebisho baadhi. Na baada ya hapo inapigiwa kura na wajumbe wa tume hiyo kwa kigezo kuwa kilichomo ndani ya rasimu ni maoni solely ya wananchi na hakuna kipengele chochote kilichopachikwa either na wanatume au nje. Ili Rasimu ipite ni lazima wajumbe wote waikubali si kwa kuwa yaliyomo yamewafurahisha la bali kwa kuonesha kuwa kumbukumbu zao za maoni ya wananchi na kilichomo havitofautiani.
4. Baada ya hapo rasimu hiyo inaanza kunadiwa kwa wananchi kwa ajili ya kuipitishwa kwa referendum na tume ya kusimamia referendum hiyo inachaguliwa na kuundwa na Tume hiyo kwa wajumbe wote kuwakubali watendaji wa tume kwa sauti moja.
Wakati wa referendum sasa hapo watu wanaweza kuchukua upande na kazi ya tume inakuwa imefikia kikomo pale tu rasimu hiyo inapokuwa imepitishwa na asilimia si chini ya 60% wananchi ya wapiga kura wote walioandikishwa na tume ya uchaguzi ya referendum ambayo itapata maagizo yote kutoka kwenye tume ya katiba, Mchakato huu utatakiwa uwe umekamilika mwishoni mwa 2012 ili kutoa nafasi kwa vyama na serikali kujiandaa na uchaguzi wa 2015 kwa kutumia katiba mpya.
HUU MCHAKATO UKIFANYIKA NDIYO UTAKUWA UMEWAENGUA WANASIASA KATIKA KUINFLUENCE OUTCOME YA TUME HII NA SI KWA KUCHAGULIWA NA SHEIN AU KIKWETE.