Wanasiasa wa leo ni "photocopy" tu ya kizazi cha wanasiasa waliopita

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Habari wakuu,

Nchi yetu imekuwa ikiendeshwa kama "gari bovu" kwasababu watu tuliowabidhi nchii hii ni wanasiasa "fake".Kizazi cha wanasiasa halisi kilishapita na hakitorudi tena na itabaki kuwa historia tu.

Migogoro na uozo kuanzia kwenye vyama vya siasa mpaka serikalini ni matokeo ya kuwa na wanasiasa fake.

Ukichagua mwanasiasa photocopy(fake) ni sawa tu na kununua bidhaa fake ambayo itakusumbua tu na pengine utaishia kujuta tu kama ambavyo tunajuta sasa.

Ndugu mwananchi mwenzangu wewe pigania maisha yako tu na kamwe usiwaamini wala usiweke matumaini yako kwa hawa wanasiasa photocopy waliokuja kuchuma tu na siyo kuifanya nchi ichume kutoka kwao.

Kama kizazi hiki cha wanasiasa photocopy wa leo ndio kingepigania uhuru wa nchi yetu,hakika kingeweza hata kuhongwa na wakoloni na kusaliti umma na kamwe tusingepata uhuru.

Ni hatari kwa mwanasiasa kuchuma kutoka kwenye nchi yake badala ya nchi kuchuma kutoka kwa mwanasiasa wake.
 
Back
Top Bottom