Wanasiasa ndio binadamu wanafiki zaidi duniani

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Huyu ndio hua anatuhubiria kuwa ndege hazina faida kwa watanzania. Kwa hali hii basi wanasiasa ni watu wanafiki Sana hapa duniani anaweza pinga ama kusifi kitu kwa masilahi yake.

FB_IMG_1600185921210.jpg

Mifano ni hii;​

Mch Peter Msigwa alipomuomba Radhi mzee Kinana kwa kupaka matope kuwa ni Jangiri kwa masilahi yake ya kisiasa. Naamini baada ya uchaguzi Kuna watu wengi sana wataomba radhi kwa huu unafiki unao endelea.

Sasa hivi Kuna Wana siasa wanapinga Tanzania kupata 60% kwenye bomba la mafuta.

Wengine wanapinga Ujenzi wa bwawa la umeme kwamba watanzania hawana haja nalo kwa sasa.

Watanzania hawali barabara na madaraja, kipindi Cha masika daraja likikatika kwa siku mbili tu utawasikia wakisema hakuna miundombinu ya kutosha.

Hatuna haja na ndege huku yeye anapanda, hapo wamesahau zile kauli zao kuwa ni aibu kubwa kwa nchi Kama Tanzania kukosa ndege hata moja.

Kuna mwanasiasa mmoja yeye alituambia kuwa nchi hii imeliwa sana wakati yeye alikuwa ndani ya baraza la mawaziri kwa miaka 20.
 
Hakika mkuuu kama mwenyekiti wa chama.Ni mnafiki hasa.

Leo utasikia maendeleo hayana vyama. Kwesho utasikia msiwachague wapinzani hata kama ni wazuri.

Leo utasikia tumepata mkopo kutoka kwa wenzetu rafiki zetu. Keshoutasikia tunajenga kwa fedha zetu wenyewe. Hatutaki hela za mabeberu.
 
Nakubali kuna wanasiasa wanafiki lakini si wote.

Wanasiasa wanafiki zaidi ni hawa hapa kwa order ya tokea juu kwenda chini:

Jiwe, mpara magamba, yule spika wa Mbeya, yule wa kongwa, bashiri, mpole mpole, hawa kina Msukuma, hawa wa Lindi ni umbumbu tu.
 
Na wale walio tuambia Lowasa ni fisadi papa na kutuletea nyaraka za ushahidi huku wakimtaka kujiuzulu uwaziri Kisha wakaja kumuimbia pambio kuwa ni Rais wao wa mioyo wakamnadi kwa nguvu zote na kumfagilia barabara apite na hawa tunawaweka kundi gani?
 
Hakika mkuuu kama mwenyekiti wa chama.Ni mnafiki hasa.

Leo utasikia maendeleo hayana vyama.
Kwesho utasikia msiwachague wapinzani hata kama ni wazuri.

Leo utasikia tumepata mkopo kutoka kwa wenzetu rafiki zetu.
Keshoutasikia tunajenga kwa fedha zetu wenyewe. Hatutaki hela za mabeberu.
Kwahiyo ulitaka m/kiti wa ccm ampigie kampeni mgombea wa upinzani kwamba mchagueni huyu ndio anafaa amuache wa chama chake?

Siasa za namna hiyo uliwahi kuziona nchi gani mkuu?
 
Hakika mkuuu kama mwenyekiti wa chama.Ni mnafiki hasa.

Leo utasikia maendeleo hayana vyama.
Kwesho utasikia msiwachague wapinzani hata kama ni wazuri.

Leo utasikia tumepata mkopo kutoka kwa wenzetu rafiki zetu.
Keshoutasikia tunajenga kwa fedha zetu wenyewe. Hatutaki hela za mabeberu.
Ambaye amewahi kuzitoa hizo kauli HANA AKILI TIMAMU.
 
Akili zenu ni za kuvukia barabara tu!Kwani kabla ya JPM walikuwa hawapandi ndege?mambo ya ndege zingeachiwa sekta binafsi kulingana na uhitaji na mazingira ya sasa!
Wewe una akili za kufanyia nini Kaka?
 
Unafiki ni asili ya mtu na hauna mahusiano na kazi ya mtu,kama mwanasiasa mnafiki hata akiwa mfanya biashara atabaki kuwa mnafiki,akiwa shekhe au mchungaji atabaki kuwa mnafiki,akiwa mwalimu au daktari atabaki kuwa mnafiki tu,unafiki hauna mahusiano na harakati za kisiasa maana kuna wanasiasa wanamuamini Mungu vizuri tu.
 
Hakuna Mtanzania asiyependa maendeleo. Ujinga tunao ukataa sisi wengine ni huu wa kutuambia eti sitawapandisha madaraja yenu, kwa sababu ninanunua kwanza ndege!

Huu uonevu ndiyo unao tusababishia wengine tuzichukie hizo ndege. Huwezi kumnyima mtu haki yake kwa kisingizio kingine.

Leo hii wafanyakazi walio ajiriwa mwaka 2014, 2015, 2016,2017 na kuendelea, na watakao ajiriwa mwaka huu wa 2020 mshahara wao utafanana! Hili ni jambo lisilokubalika kabisa kwenye taratibu za kiutumishi.

Na ninakuthibitishia, hakuna mfanyakazi wa nchi hii mwenye akili timamu, atakayeichagua ccm mwaka huu kwa ngazi yoyote ile. Katika hili, mkubali tu magufuli amefeli vibaya.
 
Wanakwambia ndege hazina umuhimu wakati wao ndo wapandaji wakubwa wa ndege.

Watu wapo kutetea maslahi binafsi hakuna anayejali maslahi ya nchi kwa sasa wala kwa vizazi vijavyo. Wapinzani hawawezi file mbali maana wengi wao wana ajenda binafsibinafsi huku wakijificha kwenye kichaka cha upinzani. Watu walizoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi....

Sasawatapendaje maendeleo wakati-

Ndege Zikiwa za serikali zinakua hazina umuhimu, heri zisiwepo tulete wabia tupigedili

Tuue reli tulete malori tupige pesa,

Tusilinde madini yetu tuwaite wageni waje tuwauzie kisirisiri serikali ikose mapato sisi tupige pesa

Tuue hospitali za umma tufungue za kwetu tuweke bei za juu tupige pesa asiye na pesa afe tuu,

Tuue public schools tuanzishe private school tupige pesa.......

Tusijenge barabara, wala reli, wala vivuko, wala mahala.. wakulima walime mazao yao wakose pa kuyahidhi tukayanunue kwa bei ya kuwaumiza tuuze nje ya nchi kwa njia za panya tupige pesa

Tusitumie kiinglishi shuleni halafu sisi ndio tuwe tunaingia mikataba ya kizungu na wazungu wabebe madini hadi makinikia, samaki hadi mapanki tupige pesa

John Pombe Joseph Magufuli amejua kuwanyoosha. Awamu ya kwanza mabarabara, usafiri wa anga, maji, umeme, huduma za afya zimeboreshwa sana..... tulieni awamu ya pili sekta ya elimu iimarishwe

Dam55 tutaelewana tuu kidogokidogo
 
Watu wapo kutetea maslahi binafsi hakuna anayejali maslahi ya nchi kwa sasa wala kwa vizazi vijavyo. Wapinzani hawawezi file mbali maana wengi wao wana ajenda binafsibinafsi huku wakijificha kwenye kichaka cha upinzani. Watu walizoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi....

Sasawatapendaje maendeleo wakati...
Asante kwa mawazo yako Ila tupo tutakao tofautiana na wewe.
 
Akili zenu ni za kuvukia barabara tu!Kwani kabla ya JPM walikuwa hawapandi ndege?mambo ya ndege zingeachiwa sekta binafsi kulingana na uhitaji na mazingira ya sasa!
Hakuna ndege iliyokuwa inatua kigoma
 
Back
Top Bottom