Wanasiasa na Wachumi nisaidieni: Uchumi wa nchi hukua unapotumia zaidi au kidogo ? Hasa fedha inapokuwa ya mkopo?

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,285
2,000
1. Tunajenga reli ya kisasa ikikamilika, tusubirie endapo itajitokeza mizigo.
2. Tumejenga uwanja mkubwa kule ngambo ya Rubondo, umekamilika, tunasubiria midege ijitokeze au itue kwa kwa bahati kwa kupotea njia.
3. Tumenunua ndege, taarifa imetolewa tutasubiri sana hadi kuanza kupata faida.
4. Tuligharamika sana gesi ya Mtwara, tumeambiwa juzi ni 6% ya gesi ya bomba inatiririka, itahitajika kuongeza uwekezaji ili itiririke zaidi.
5. Umeme wa mto Rufiji utaongeza umeme ili baadae wawekezaji waje waukute uwatoshe, hii nayo ni uyumkini kama watakuja.
Swali langu, kwa haya yote, inakuwaje tusikie kuwa uchumi bado unakua?
Kuna mtu aliniambia, ingekuwa fedha zote hizo ni za ndani, kimahesabu ingeonyesha Uchumi unakua kwa vile umespend ulichozalisha. Sasa tofauti ni kuwa hizi ni pesa za mikopo, vipi hapo? Naomba kujuzwa wajameni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom