kagoshima
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,535
- 6,867
Nimepenyezewa habari za uhakika kwamba Katibu wa CCM aliyepo ziarani Morogoro, anatarajiwa kutembelea pia Chuo cha kilimo SUA siku ya Jumapili asubuhi. Hivyo basi wafanyakazi wote bila kukosa ( ni lazima) wanatakiwa wawepo kumpokea kiongozi huyu wa chama. Kwa wale wakristo hakuna kuabudu. Siku hiyo ni maalumu kumuona kiongozi wa chama cha mapinduzi.
Shida yangu siyo huyu mweshimiwa kwenda SUA. Ila Maswali haya yanahitaji majibu.
1. Kwanini anaenda Jumapili siku ya ibada?
2. Kwanini haendi siku za kazi kisheria (Monday to Friday)
3. Siasa zimekuwa zaidi ya Ibada kwa Mungu ?
4. Ni nini hasa anachokuja kuongea huku kiongozi wa chama kinachohitaji siku ya ibada kutumia?
Wanasiasa mwogopeni Mungu. Jumapili ni siku ya wakristo kuabudu . Sio kila kitu siasa siasa tu