thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Kinachonisikitisha ni pale mnapoandaa maandamano lakini hamtokei na familia zenu, waandamanaji baadhi huuwawa na wengine huambulia kifungo,na cha kushangaza huwa mnawatelekeza magerezani bila msaada wa kisheria.
Mnawatumia wananchi kama daraja la mafanikio yenu kisha mnakaa meza moja na mahasimu wenu na kugonga cheers.
Kwanini hamkumbuki hata kuwapa fidia wafuasi wenu kwa jasho lao na damu yao angalu kuwafuta machozi na machungu walioyapata katika kuwasapoti?
Kuna vijana wengi sana baadhi yao wamekufa, walemavu,na wengine wapo magerezani ,mnampango gani nao kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2020?
Au ndio tunasubiri kuandaa wengine wa kuleta vurugu kwa kuwanywesha gongo na kuwavutisha bangi ili muweze kupanda ngazi kuu?
Tuwe na huruma na watoto wa watu, wanategemewa pia na familia zao
Sent using Jamii Forums mobile app