Wanasiasa mna dhambi kubwa sana mnapojidai mnatetea maslahi ya umma wakati ni maslahi yenu binafsi

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
6,641
2,000
Kinachonisikitisha ni pale mnapoandaa maandamano lakini hamtokei na familia zenu, waandamanaji baadhi huuwawa na wengine huambulia kifungo,na cha kushangaza huwa mnawatelekeza magerezani bila msaada wa kisheria.

Mnawatumia wananchi kama daraja la mafanikio yenu kisha mnakaa meza moja na mahasimu wenu na kugonga cheers.

Kwanini hamkumbuki hata kuwapa fidia wafuasi wenu kwa jasho lao na damu yao angalu kuwafuta machozi na machungu walioyapata katika kuwasapoti?

Kuna vijana wengi sana baadhi yao wamekufa, walemavu,na wengine wapo magerezani ,mnampango gani nao kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2020?
Au ndio tunasubiri kuandaa wengine wa kuleta vurugu kwa kuwanywesha gongo na kuwavutisha bangi ili muweze kupanda ngazi kuu?

Tuwe na huruma na watoto wa watu, wanategemewa pia na familia zaoSent using Jamii Forums mobile app
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,522
2,000
Ni vyema pia ukawazungumzia na wale wanaosign mikataba kwa kivuli cha kwa niaba ya Watanzania huku 10% percent zinaingia kwenye mifuko yao kwa manufaa ya Wake, mahawala na watoto zao.

Wakumbuke na wale wanaotuambia kutwa kucha elimu bure huku watoto wao wamejazana pale FEZA na kwingineko.

Wakumbuke na wale wanaotuambia tuna huduma bora za Afya halafu wanakwenda kutibiwa India na ulaya.

Wakumbuke na wale wanaoiba mali za umma wakiwa na nyadhifa kwenye ofisi za Umma halafu wanazihonga kwa malaya na kusomesha watoto ulaya.

Wakumbuke na wale makada wa chama waliofirisi mali za umma halafu bado wako mjengoni wako busy kusema ndioooo..
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
6,641
2,000
Sawa chadomo imepenya hiyo
Ni vyema pia ukawazungumzia na wale wanaosign mikataba kwa kivuli cha kwa niaba ya Watanzania huku 10% percent zinaingia kwenye mifuko yao kwa manufaa ya Wake, mahawala na watoto zao.

Wakumbuke na wale wanaotuambia kutwa kucha elimu bure huku watoto wao wamejazana pale fedha na kwingineko.

Wakumbuke na wale wanaotuambia tuna huduma bora za Afya halafu wanakwenda kutibiwa India na ulaya.

Wakumbuke na wale wanaoiba mali za umma wakiwa na nyadhifa kwenye ofisi za Umma halafu wanazihonga kwa malaya na kusomesha watoto ulaya.

Wakumbuke na wale makada wa chama waliofirisi mali za umma halafu bado wako mjengoni wako busy kusema ndioooo..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
7,021
2,000
Kinachonisikitisha ni pale mnapoandaa maandamano lakini hamtokei na familia zenu,waandamanaji baadhi huuwawa na wengine huambulia kifungo,na cha kushangaza huwa mnawatelekeza magerezani bila msaada wa kisheria .

Mnawatumia wananchi kama daraja la mafanikio yenu kisha mnakaa meza moja na mahasimu wenu na kugonga cheers.

Kwanini hamkumbuki hata kuwapa fidia wafuasi wenu kwa jasho lao na damu yao angalu kuwafuta machozi na machungu walioyapata katika kuwasapoti?

Kuna vijana wengi sana baadhi yao wamekufa, walemavu,na wengine wapo magerezani ,mnampango gani nao kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2020?
Au ndio tunasubiri kuandaa wengine wa kuleta vurugu kwa kuwanywesha gongo na kuwavutisha bangi ili muweze kupanda ngazi kuu?
Tuwe na huruma na watoto wa watu ,wanategemewa pia na familia zao

Kuna wale wanasiasa wanaojidai kuwajali wanyonge, lakini ilpotoka ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ikianika upotevu was tril 2.4, wanasiasa wale wakamfanyia zengwe wakamfukuza.

Dah wanasiasa hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom