Wanasiasa:chanzo cha umaskini tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa:chanzo cha umaskini tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Myakubanga, Jan 1, 2012.

 1. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Uchaguzi mkuu umekwisha mwaka 2010 na kuchaguliwa serikali inayoongozwa na CHAMA CHA MAPINDUZI(Bila kujali uhalali wake kama kulikuwa na uchakachuzi au la).Lakini jambo la kushangaza mno ni kwamba mijadala inaendelea kila kona ya nchi yetu:maofisini,mitaani,vijiweni,makanisani,misikitini na kwenye mitandao ya kijamii juu ya nani anafaa kuwa rais 2015,nani anafaa kuwa mbunge,madiwani nk.
  Huu ni utamaduni hatari kwa nchi yetu,kwamba muda wote tulumbane kuhusu chaguzi zinazofuata,huku tukisahau kuhimizana
  kufanya kazi kwa Juhudi na maarifa!Bila shaka nyuma ya mijadala hii mikali inayo husisha kuchafuana na kusafishana mitandaoni,kupeana sifa za kweli na uongo wapo wanasiasa wanaotafuta kwa hali na mali uongozi mwaka 2015.Anyway,si jambo baya kusaka madaraka,lakini ni jambo la busara kuhimiza watu kufanya juhudi katika shughuli za maendeleo na kutafuta kujengeka kisiasa kwa kufanya hivyo!
  Ni kweli watanzania wengi(mimi nikiwemo) wamechoka na utawala mchovu wa CCM,lakini ni vema watanzania tukakazana kufanya juhudi na maarifa kukuza vipato vyetu,na mwaka 2015 tujitokeze kupiga kura na kuleta mabadiliko!
  Kugeuka taifa la uchaguzi si jambo jema kwa taifa letu!
  MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
Loading...