Ras John I
Member
- Oct 3, 2017
- 39
- 22
Huwezi ongelea maendeleo ya dunia bila kuitaja Afrika, Afrika ndiye mama mwenye kuinyonyesha dunia na kuifanya istawi kila kitu kizuri duniani basi Afrika kipo tuna kila aina ya madini ma mali asili mbalimbali lakini mpaka leo Afrika imebaki nyumba ukilinganisha na mabara mengine. Swali kubwa la kujiuliza ni nani wa kuiamsha Afrika iweze kutoka kwenye usigizi huo wa pono? Ni nani wa kuiambia Afrika ijitambue ili iweze kutambua nguvu ambazo inazo? Leo ningependa kuongea ni kwa jinsi gani Wanasiasa wamekuwa chanzo cha Anguko la Afrika.
Mwanasiasa ni nani?
Mwanasiasa ni mtu yeyote mwenye kutaka uongozi kwenye ofisi, madarasani na hata kwenye jamii zetu kwa kutoa ahadi ambazo anajua fika kuwa kamwe hawezi kuzitekeleza. Ila huzitoa kwa sababu tu ana matamanio ya kupata kitu Fulani kutoka kwenye uongozi huo anaoutaka.
Mwanasiasa mara nyingi huwa na mawazo ya kuvuna mara tatu ya kile alichokipanda na ndio maana yuko tayari kuuza mali zake ili apate pesa za kuwahonga wananchi na yeye aweze kupatata nafasi hiyo ya uongozi.
Ipo tofauti kubwa sana na ambayo wengi kutokana na upofu wetu tumeshindwa kuigundua tofauti hii kati ya,
(a) Kiongozi
(b) Mwanasiasa.
Kiongozi huwa kiongozi siku zote lakini mwanasiasa hawezi kuwa kiongozi mara zote na hii inatokana na dhumuni na lengo kuu wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza watu dhumuni ambalo kila mgombea huwa nalo moyoni mwake.
Wazee wetu wengi ambao walishiriki kwa hali na mali kupigania uhuru na ukombozi wa Afrika wengi wao walikuwa ni viongozi na wala hawakuwa wanasiasa na ndio maana tumeweza kuwashuhudia wengi wakiondoka madarakani na umasikini wao huku wakiamini kutumia mali za walalahoi vibaya ni dhambi kwa ulimwengu na kwa mungu “hakuna mwanasiasa anayeondoka madarakani akiwa masikini, atakuwa masikini wa roho lakini sio masikini wa vitu.” Wazee wetu hawa waliondoka madarakani wakiwa na matumaini makubwa ya kuwa na Afrika endelevu yenye kuleta tabasamu kwa mama na mtoto Afrika.
Mungu awabariki na kuwalinda wale walio hai na awapumzishe mahala pema peponi wote walio tangulia peponi. Amina.
Nikiachana na utangulizi huo leo nataka nisimame hadhadarini na kutamka waziwazi bila kificho kuwa kwa mtazamo wangu na akili zangu timamu kabisa napenda kusema kuwa kwa asilimia 80% “Anguko la bara la Afrika limesababishwa na wanasiasa tulio nao.” Na zifuatazo ni sababu zinazonipelekea mimi niwe muumini wa Imani kuwa anguko la Afrika chanzo ni wanasiasa wetu;
Wanasiasa wengi wapo madarakani kwa ajili ya masilahi yao binafsi na wala sio mustakabali wa mataifa yao. Kama ambavyo nimekwisha ongelea jambo hili kwenye utangulizi wangu hapo juu swala hili lipo wazi kabisa wanasiasa wengi Afrika wanaingia madarakani kwa lengo kubwa la kujilinda na kuweza kuchota kodi za walala hoi kwa ajili ya matumizi yao binafsi tunaweza wote kufikiria ni wanasiasa wangapi wana mali nyingi ambazo wala haziendani na kipato chao wanachopata na kama hili ni gumu basi wote tunaweza kutafuta na kujua nini baba yangu mpendwa Rais Mstaafishwa wa Gambia ndugu Yahya Jammeh, hapo tutaweza kuona sababu kubwa hasa ya anguko la Afrika.
Wanasiasa wengi hawajui kusoma na wale wachache wanaojua kusoma hawaelewi walichokisoma. Wewe kama mwafrika usie na elimu kubwa tu unaweza kukaa chini na kufikiria kiundani ni nini chanzo cha mikataba mibovu ya mali asili za Afrika? Je ni wananchi wa Afrika au ni wanasiasa wanaotia sahihi na kuifungia mikataba hiyo ndani? Na unaweza ukatumia akili ndogo tu kujiuliza hivi mkataba unasainiwa kwanza kabla ya kusomwa au unasomwa ndipo utiwe sahihi? Na kama huwa unasomwa ndipo unatiwa sahihi ni kwanini basi tunakuwa na mikataba mibovu ambayo haina manufaa makubwa kwa waafrika Zaidi akutufanya tuwe watumwa. Ukiweza kujibu haya maswali basi mara moja unagundua kuwa wanasiasa wamekuwa chanzo kikubwa cha anguko la Afrika.
Wanasiasa wengi ni waoga wa kupokea ukweli na kuufanyia kazi. Kuwa raisi, waziri au hata mbunge hakumfany mtu awe Mungu. Na kukufanya wewe uwe unajua kila kitu wanasiasa wengi wa Afrika wamekuwa miungu wenye kujua kila jambo, umeme, maji, madini, samaki, kilimo, afya, elimu, vyote hivi wanasiasa wa Afrika wanavijua hawapendi kupokea maoni mazuri kutoka kwa wataalamu wa vitu hivyo kwa kuogopa huenda kutekeleza sera za mtu mwingine aliyebobea kwenye Nyanja hiyo kutawapotezea umaarufu hapa ndipo unakuta mwanasiasa anaamua kuchanganya masomo ya “Fizikia na Kemia” liwe somo moja halafu tunategemea kupata mainjinia wa kuliendeleza bara hili la Afrika. Na kutokana na mambo kama hayo tunaishia kushuhudia bara letu la Afrika likiishia kuanguka kila kuitwapo leo.
Wanasiasa wengi Afrika ni chanzo kikubwa cha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita kubwa vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Afrika huchochewa na wanasiasa ambao mara nyingi unakuta wamegoma na hawataki kutoka madarakani hata pale ambapo mambo yamewashinda, na kama tujuavyo popote penye vita maendeleo ni ngumu kupatinaka hivyo kutokana na uwepo wa wanasiasa wenye uchu wa madaraka imekuwa ni chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe na mwisho tunashuhudia wote anguko la Afrika.
Wanasiasa wengi huogopa mabadiliko hasa mabadiliko chanya. Kati ya vitu ambavyo wanasiasa wengi wa Afrika wanaogopa basi ni maadiliko hasa mabadiliko chanya hawakotayari kabisa kukubaliana nayo. Na pale ambapo kiongozi atakuwa amefanya jambo baya basi atakaye mkosoa lazima “akione cha mtema kuni.” Wengi huamini kuwa wao wenyewe ndio wako sahihi kuliko watu wengine wote waliokwenye nchi zao bila kujua kuwa kila siku yapo maarifa mapya na kila kizazi kinapaswa mtu mwenye kuendana na kizazi husika wapo wanasiasa wengi Afrika ambao wameshika nyadhifa za uraisi tokea nchi zao mpaka leo hii wakiamini kwamba hakuna wengine wenye weledi wa uongoza kama wao. Mawazo hayo mgando yamekuwa kisababishi kikubwa cha kutoendelea kwa bara la Afrika.
Wanasiasa wengi huamini kuwa Afrika na sisi waafrika wenyewe hatuwezi kuendelea mpaka tutegemee misaada ya wahisani. Tumekuwa tukishuhidia hata kwenye vyombo mbalimbali ya habari jinsi wanasiasa wengi wanavyo furahia na kujiganmba kupokea misaada kutoka nchi mbalimbali nje ya bara la Afrika hasa Marekani na Uchina. Misaada ambayo mingi haitusaidii Zaidi ya kuendelea kutubomoa kila kuitwapo leo.
Misaada mingi mikubwa ambayo tunapewa huja na mashariti na kupangiwa jinsi ya kuitumia, tunaweza tu kujiuliza ni kwanini misaada mingi huletwa kwa ajili ya kutengeneza miundombinu barabara na reli na sio ujenzi wa viwanda vikubwa? Jibu ni jepesi tu kuwa kama Afrika itaweza kuwa na miundombinu barabara na reli iliyo mizuri basi itakuwa ni rahisi kutoa malighafi za Afrika kuzipeleka katika nchi hisi wahisani
Ifike pahala tusijisifu tu kwa kuwa na urafiki mzuri kufikia wakati ambao tunasaidiawa kujengewa maktaba bure tusiisifie tu maktaba ila tujiulize je kutoka kwenye maktaba hii inayojengwa tutaweza kupata hata ujuzi mdogo wa kusindika nyanya ili tuweze kumsaidia yule mkulima kule kwa bibi naye anufaike na kilimo chake?
Leo naomba niweze kuishia hapa lakini ni malize kwa kusema maneno machache nayo ni “ndugu zangu wa Afrika naomba nipende kuwa kumbusha kuwa Afrika haitoweza kuendelea kwa kutegemea watu kutoka nje sisi wa Afrika wenyewe ndio wa kuiendeleza Afrika sera zao za kupunguza na kuondoa umasikini Afrika hazina msaada wowote Zaidi ya kuzidi kutengeneza wigo wa umasikini emdelevu Afrika. Afrika itaendelea pale ambapo wote tutaamua kusimama kupambana kwa machozi, jasho na damu kuwa na Viwanda endelevu hivi tu ndivyo vitaweza sio tu kufuta umasikini bali ni kuondoa neno umasikini katika kamusi ya Afrika.”
Asanteni sana.