Wanasiasa acheni ubinafsi, wapimwe wafanyakazi wa afya kwanza ndipo na nyie mtafuata.

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,312
Naona sasa tumeanza kuelewana. Mbunge mmoja tuu kupata maambukizi ya corona mmeshataharuki. Tulieni hivyohivyo msitake kujifanya uhai wenu ndio wa muhimu zaidi kuliko watu wote hapa nchini.

Frontline fighters wa hii vita ni wafanyakazi wa afya. Mpaka sasa kuna idadi kadhaa ya hao wapambanaji wameshaukwaa huu ugonjwa na wanapambania maisha yao. Pamoja na hayo cha kusikitisha mpaka sasa hakuna anayeona umuhimu wa hawa wapambanaji kupimwa wote ili wale walio na asympomatic infections wajitenge ili wasiendelee kuwaambukiza wafanyakazi wengine na wagonjwa pia.

Tulitegemea kwa mkoa kama Dar basi ingekuwa mandatory wafanyakazi wote kupimwa kila baada ya wiki au wiki mbili. Lkn hakuna hiko kitu na wameachwa wapambane na hali zao. Sina uhakika sana pia kama wamepewa PPE za kutosha za kupambana na huyu kirusi.

Sasa iweje nyie wabunge kuugua mmoja tuu mnataka mpimwe wote? Kati yenu na hawa wapambanaji nani ana priority kubwa? Kwa nini mnajijali nyie zaidi kuliko wapambanaji halisi walio mstari wa mbele wa mapambano?

Tunaomba kabla hamjajipima nyie basi muhakikisha mmewapima hawa frontline fighters vinginevyo picha mtakayotupatia tutaitumia kisawasawa mwezi wa kumi kunako sanduku la kura.

Screenshot_20200420-163350.jpg
 
Sierra Lione wameonelea wawapunguzie mzigo wa kodi wafanyakazi wa afya, wawalipe risk allowance, wawape makazi ya muda pamoja na huduma za msingi, wawakatie bima ya maisha endapo mfanyakazi wa afya atafariki basi familia ipate compensation n.k.

Sisi hapa wanasiasa wetu wanajifikiria wao tuu na afya za familia zao. Mkumbuke huu ugonjwa ukiupata hakuna kusafirishwa nje ya nchi kama mlivyozoea, hivyo kuweni makini sana na kuwalinda wafanyakazi wa afya maana ndio our only hopes.

IMG-20200420-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom