Wanasheria wapo wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria wapo wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Mar 21, 2012.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Tumeshuhudia hivi karibuni mgomo wa madaktari na tishio la mgomo mkubwa wa waalimu.

  Licha ya kutetea maslahi yao, wadau wa migomo hii wamekua kwa kiasi kikubwa wakidai uboreshaji wa huduma wanazotoa kwa wananchi. Hivyo basi wafaidika wakubwa wa migomo hii ni sisi wananchi.
  Lakini kwa nini Waanasheria mpo kimya, ni kusema kwamba sekta yenu imekamilika?Inatoa huduma kama inavyotatikana? Mbona kila siku tunalalamika kubambikiziwa kesi, hamsikii ? Raia Kulala mamia kwenye selo ndogo hamuoni ? Kukaa rumande bila kufikishwa mahakamani? Nakala za hukumu kutopatikana kwa muda muafaka?
  Inakuaje vigogo wa rushwa wapo nje? Wanasheria mnasemaje juu ya mikataba mibovu mliyosaidia kusaini? Mnaridhika na katiba ya sasa? Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria unaofanywa na vigogo..mf. Malima na bunduki ya kivita , mbona mpo kimya? Inakuaje wawekezaji wananyanyasa raia kupitia wanasheria?

  Wanasheria wana nafasi kubwa sana ya kuleta maendeleo na mageuzi ya kweli nchi hii lakini ni WABINAFSI MNO.
  Ni WANASHERIA waliomuangusha Musharaf huko Pakistan.
   
 2. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Unamsema mwanasheria kama Ridhiwani,chenge au nani?hao si ndo walewale wanapitia mlango wa mbele na kutoa mlango wa nyuma?(emergence door)
   
Loading...