Wanasheria mnahitajika hapa

mitindo huru

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2016
Posts
1,610
Reaction score
1,602
Habari za jumapili wadau?
Nimeandika kwa kifupi ili iweze kueleweka, pia naomba usome hadi mwisho ili uweze kuelewa vizuri.
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Iko hivi kuna rafiki yangu alipanga nyumba eneo la Tabata jijini dar es salaam, wakati anaendelea kukaa katika hiyo nyumba akaonana na dalali na kumwambia Kama akipata nyumba ambayo ina vyumba viwili vya kulala amjulishe sababu anategemea kuhamisha familia kutoka Moshi na kuja dar hivyo atahitaji nyumba ya kutosha zaidi kwa familia,
Baada ya wiki mbili dalali akarudi na kumwambia rafiki yangu nyumba imepatikana ila rafiki yangu akamwambia dalali Bado hajafanikiwa kupata pesa na pia sehemu anayokaa bado pango la miezi miwili halijaisha hivyo dalali asubirie,
Dalala akarudi kwa mara ya pili kwa rafiki yangu akiwa na huyo mwenye nyumba kubwa mpya, mwenye nyumba akamwambia rafiki yangu naomba amia kwenye nyumba na utakuwa unanilipa laki mbili kila mwisho wa mwezi lakini rafiki aligoma na akasema kwa wakati huo hakuwa na pesa na pia sehemu anayokaa bado Kodi ya miezi miwili haijaisha, ila mwenye nyumba alimbembeleza rafiki yangu aamie hivyo hivyo na pesa atakuwa analipa taratibu, rafiki yangu ikabidi akubali kwa sababu yule mwenye nyumba alikuwa anaumwa hivyo pia alikuwa anahitaji pesa kidogo kwa ajili ya matibabu.

Sasa tatizo lilianzia hapa rafiki yangu alifanikiwa kulipa kwa miezi miwili ila kwa mwezi wa tatu alilipa laki moja na ikabaki laki moja, hapa mwenye nyumba akaanza utata anakuja kwa rafiki yangu anaongea lugha za kejeli na mda mwingine anaenda na wajumbe ila mjumbe akisikiliza maelezo anaona yule mwenye nyumba ni mkorofi.

Rafiki yangu akapata dharula mke wake akajifungua kwa operation na matatizo kibao hivyo ikambidi arudi Moshi kuangalia familia hivyo ikambidi hata biashara afunge ili amuuguze mke wake kwa ukaribu zaidi. Ikumbukwe huku nyuma aliacha deni la laki moja.
Baada ya wiki mbili akataka kumpa funguo mdogo wake ili akaangalie nyumba na pia akalipe deni Dar es salaam, ila kabla hajafanya hivyo akampigia sim jirani yake kujua maendeleo ila jirani yake akamwambia mwenye nyumba kaja kuchukua vyombo vyake na nyumba ni tupu, baada ya miezi miwili jamaa alivyoona mke wake amepata nafuu ikabidi aende Dar kujua hatma ya vyombo vyake,

Alivyofika, mwenye nyumba akamwambia jamaa hajui vyombo vyake Nani alichukua jamaa akauliza majirani na pia mjumbe ila wote wakamwambia vyombo alichukua mwenye nyumba jamaa akarudi tena kwa mwenye nyumba ila mwenye nyumba anagoma kusema ukweli vyombo vilipo ili siku ziendelee kuongezeka kwa kuwa jamaa hakuwa na makazi mengine dar es salaam ikabidi arudi Moshi na biashara ya dar es salaam akaifunga rasmi baada ya kurudi Moshi jamaa alitafuta kazi nyingine ambapo alipata biashara ya kupeleka mzigo Kenya hivyo mda mrefu alikuwa Nairobi mda mwingine Moshi kwenye familia sababu mke wake bado Hali haikuwa nzuri.

Akipata mda wa siku chache kuja dar bado mwenye nyumba anagoma kusema kwamba alitoa vyombo na wakati majirani wote wanajua alichukua vyombo ni yeye kwa kuwa alikuwa anafikia nyumba ya wageni akawa anashindwa kufatilia hilo Jambo kwa ukaribu, hivyo ikabidi aende kwenye ofisi ya mtendaji kule nako taarifa zilipofika akaambiwa vyombo alichukua mwenye nyumba, mwenye nyumba ndio akakubari kwamba kweli alichukua hivyo vyombo na akataka fidia ya miezi karibia kumi na moja ambayo alikaa na vyombo na wakati baada ya kutoa vyombo katika hiyo nyumba alipangisha, rafiki yangu akasema yeye hawezi kulipa ela yeyote sababu vyombo havikuweko ndani ya nyumba aliyopanga. Hivyo rafiki yangu akatoa laki moja aliyokuwa anadaiwa na laki moja nyingine ni Kama usumbufu kwa kuhamisha vyombo, ila mwenye nyumba akagoma akasema anataka laki tano, hivyo mwenye nyumba akasema anapokea hiyo laki mbili ila atatoa baadhi ya vyombo na vyombo vingine atavitoa baada ya hiyo laki tatu kumalizika rafiki yangu kuona hivyo akaona ni bora akubali sababu vyombo vyake ni vya thamani kubwa ukilinganisha na hiyo ela kumbuka hayo makubaliano yanafanyika ofisi ya mtendaji kabla rafiki yangu ajaona vyombo vyake.
Sasa rafiki yangu alivyofika kuona vyombo balaa likaanzia hapo kumbe mwenye nyumba vyombo aliviweka kwenye store ya nje ambayo haijasakafiwa kakuta vyombo vimeharibika karibia vyote kuanzia jagi la umeme, feni ipo vipande vipande, neti ya vyuma nayo imekatika nguo zimeoza, mashuka yameoza kwa unyevu, ndoo zilikuwa zinatumiwa kuchanganyikiwa rangi, vyombo vya chakula vina marangi, kitanda kilianza kuoza sababu ya unyevu kwenye hiyo store. vitu alivyovikuta salama ni vile ambavyo mwenye nyumba alikuwa anatumia Kama godoro. Ila vitu vingine Kama Samsung flat screen inch 32, HP printer, Friji kubwa milango miwili, oven, sofa seti, full HP computer desktop n.k mwenye nyumba alishauza. Jiko la gesi kakuta linatumika mwenye nyumba kagoma kutoa sababu eti mtungi una gesi hivyo hadi uishe.
Madai ya mwenye nyumba ni kwamba amefanya hivyo ili kufidia mda aliokaa navyo hivyo vyombo na ni Kama mwaka na wakati vyombo alivitoa kwenye nyumba ila alivichukua kuvitumia na vingine havikuwa sehemu salama na vingine aliviuza na nyumba alipangisha mda mfupia baada ya kutoa vyombo.
Rafiki yangu kaona hawezi kulipa hata hiyo laki tatu iliyobakia sababu vitu vyake vingi vimeharibika na vingine havipo.

Sasa wanasheria na pia wadau wengine wenye uzoefu na haya mambo tunaomba msaada juu ya hili Jambo ili huyu rafiki aweze kupata vyombo vyake na pia kuelimishwa uhalali wa hili Jambo.
Pia ni hatua gani ziweze kufatwa ila haki ipatikane.
Natanguliza shukrani za dhati, hili jambo ni serious jamani naomba masihara yasiwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu ni wapole sana, kwanini Mungu asinifanye kama huyo jamaa, mimi tungegawana majengo ya serikali, kwanza unaanzaje kuingia ndani kutoa vyombo bila kiongozi yeyote wa serikali, huo ni wizi. Fungulia kesi huyo mbulula.

Ingawaje hii ni stori ya upande mmoja.
 
Huo ndio ukweli ndugu Molembe, mwenye nyumba alienda kutoa vyombo na Mtendaji wa mtaa, ila inavyoonekana Mtendaji mwenyewe ni kijana mdogo halafu ni Kama muhuni muhuni, maana inaonekana hilo jambo walilipanga na huyo mwenye nyumba ili waweze kunufaika na vyombo vya huyo jamaa. Ila mtendaji wa kata alivyosikia hiyo taarifa alisikitika sana sababu anamfahamu huyo mwenye nyumba kwamba ni mkorofi siku nyingi.
Jamaa yangu ndio anaomba Ushauri wa nini Cha kufanya, maana akafikiria hadi kwenda kwa Waziri wa nyumba na Makazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First thing first, makubaliano ya kulipa kodi yalikuwaje? Nasema hivyo kwa sababu mwenye nyumba anauwezo kisheria kukamata mali zilizomo ndani na kuziuza kufidia kodi anayodai kama kuna default

Lakini hiyo inafanyika baada ya kutoa notisi/ilani.

Kwa hiyo vyovyote vile itakavyokuwa, ili kujua alichokifanya landlord ni makosa, basi ni lazima kujua masharti ya makubaliano yao.

Nashindwa kuamini au tuseme kushawishika kwamba tenant alivitelekeza vitu vyake vya thamani kwa muda wote huo. Na hata kama kulikuwa na dharura ni lazima angelikuwa amefanya mawasiliano na mwenye nyumba.

Hivyo, narudia tena bila kujua makubaliano ya malipo, na status ya mahusiano yao ya kimkataba alipoondoka, ni vigumu kuhukumu moja kwa moja kwamba alionewa.

And yes, may be landlord anaweza kuwa unfair lakini aliyoyafanya pia ukakuta yapo ndani ya sheria! Baada ya kusema hayo, pole yake!
 
kweli kuna binadamu ni wapole mpaka kero,inakuwaje mwanume mwenzio anakufanyia hivyo na wewe upo tu.
 
Umeelezea vizuri,
Kwa mujibu wa jamaa na maelezo niliyotoa juu ni kwamba makubaliano ni kwamba deni lilibaki laki moja, pia hamna default yeyote sababu mwenye nyumba alikuwa ameshapata mpangaji mwingine hivyo lengo lake ni kutoa vyombo ili apangishe nyumba.
Sasa inakuwaje vyombo kavitoa na vimeharibika vingine kauza na bado anatak a fidia?
Hapo ndio msaada wa kisheria unapohitajika na muongozo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kinacho nishangaza mpole sana yani zaidi ya sana Kweli mwanaume unaletewa usenge Kama uo.
Hii sio story ndugu, ni jambo limetokea kweli, ila nadhani kwa kuwa haujawai kukutana nalo unaweza ukafikiri ni story.
Ila msaada wako wa mawazo ni muhimu sana ili tuweze kumsaidia huyu ndugu apate haki yake

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri ni huu
Atambue thamani ya mali yake baada ya hapo aende mahakamani kudai fidia kwa thamani ya hizo mali zake zilizoharibika ,pamoja na mahangaiko/mental agony for sure he has a course of action.....jambo la msingi akumbuke kuwa na risiti zinazoonyesha thamani ya hizo mali maana wanasheria wenyewe wanakwambia gharama halisi lazima zithibitishwe....
 
Mambo muhimu ya kuzingatia.
Baada ya kujua vitu vyake havimo ndani ya nyumba na kupata ushahidi kwa majirani na serikali ya mtaa. Kwanini hakwenda kutoa taarifa kwa polisi?
Mkataba wake wa kodi unaisha lini na baada ya yeye kuhama huyo mwengine kahamia baada ya muda gani?
Anao ushahidi wa vyeti vya mkewe kama alikuwa akiumwa?
Kwanini ifike mwaka ndio aende kudai vitu vyake?
Alicho kifanya landlord ni ujambazi kwasababu alikataa kuchukuwa vitu mwanzo baadae kakubali, huo ni ujambazi hapo angeweka ripoti polisi landlord agewekwa ndani kwa ujambazi.
Rafiki yako kwa sasa anatakiwa akusanye ushahidi wote kutoka kwa majirani,serikali ya mtaa na kwenda polisi kufungua kesi ya madai pamoja na wizi kwa landlord wake.


Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Na sisi watanzania tulivyo kuwa hatuna tamaduni ya kutunza risiti kazi kweli.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri mkubwa,
Thamani ya mali zake zote anafahamu, kuhusu risiti jamaa anasema zilikuwepo katika draw ya dressing table ila hiyo dressing table mwenye nyumba pia aliuza..!!
Msaada wako kisheria kuhusu hilo Jambo la risiti unahitajika sana ndugu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…