Lakini duniani kote haijapata kutokea kwamba harakati za kudai uhuru na haki vilisitishwa kwa kuua au kufunga viongozi wao. Hakuna utawala uliokuwa na nguvu kama ule Apartheid kule SA, enzi za kupigania uhuru. Makaburu walidhani wakimfunga Nelson Mandela, basi harakati zingerudi nyuma. Watawala dhalimu wanachosahau ni kwamba kadri udhalimu wao unavyozidi ndivyo hamasa ya harakati huongezeka.
Hata sasa kwa hapa Tanzania jamii lazima itajiuliza Kuna nini hasa kinachohofiwa na watawala kuwa na Katiba mpya au tume huru ya uchaguzi