Wanaovaa hovyo Vyuoni Kudhibitiwa.

Wanaovaa hovyo Vyuoni Kudhibitiwa.

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,576
Reaction score
28,497
SERA ya kudhibiti mavazi yasiyoendana na maadili, yanayovaliwa na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini, inaelezwa itakuwa muarobaini kwa wanafunzi husika.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) cha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Faustine Bee, alisema serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha sera hiyo ambayo wanaamini itakuwa msaada mkubwa wa kulinda uvaaji vyuoni.

Alisema kuwa chuo hicho pamoja na vyuo vingine haviwezi kuwaruhusu wanafunzi, hasa wa kike kuvaa mavazi ya nusu uchi yanayoshushia heshima vyuo na utu wa wahusika. Prof. Bee alisema kuwa pamoja na sera hiyo kuwa hatika hatua za mwisho, walengwa ambao ni wanafunzi, nao watashirikishwa ili kutoa maoni yao juu ya mfumo stahiki wa mavazi hayo na kuongeza wakubali wasikubali sera hiyo ni mhimu kwa lengo la kudumisha heshima ndani ya jamii.

Alisema suala la nidhamu ni muhimu kwa lengo la kujenga maadili mema ndani ya jamii na kuongeza kuwa vijana wengi wamejiunga na vyuo wakitokea kwa wazazi wao, lakini wamekuwa na uhuru wanaoutumia vibaya.

Prof. Bee alisema kama vijana wataendelea kulelewa kwenye maadili mema, taifa litakuwa na kizazi chenye staha. Kwa mujibu wa Prof. Bee, mchakato wa sera hiyo ya mavazi ukikamilika utarasimishwa rasmi na mwanafunzi atakayeikiuka ataondolewa chuoni hapo. Katika hatua nyingine, chuo hicho kimekaribisha wawekezaji watakaojenga hosteli na sehemu za chakula kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wanachuo na wafanyakazi wake.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Nina mashaka na CV na IQ ya huyo prof. nyuki. Chuokikuu ni kitu cha kimataifa, sasa mwanafunzi va kimataifa eg. from america utamlazimishaje sera zako za mavazi ya utamaduni wako wakati na yeye ana wa kwake? ndo mana vyuo vyetu vingi vinakosa sifa ya kuwa vya kimataifa.
 
ndiyo maana hiyo MUCCOBS sijui MKOBA itabakia CC ya SUA milele
 
Sifa ya msomi ni kujielewa na kujitambua,haiwezekani mtu unavaa skin tyt, half min skirt,open n' short tops kama unaingia club huku unaingia darasani,in short wanafunz wengi wa kike Muccobs wanavaa vibaya hawazingatii code of ethics,hongera Prof. Bee kwa kuliona hilo na kujitahidi kujitafutia ufumbuzi.
Ushauri: Angalieni wanafunzi wengi wa sheria wanavovaa kuzingatia legal attire ya black n white suti wanavopendeza na kuonekana kweli ni wasomi na wako tofauti na wenzao ambao unashindwa kujua anasomea course gani ukahisi labda kuna course mpya ya kujiuza.
 
Nina mashaka na CV na IQ ya huyo prof. nyuki. Chuokikuu ni kitu cha kimataifa, sasa mwanafunzi va kimataifa eg. from america utamlazimishaje sera zako za mavazi ya utamaduni wako wakati na yeye ana wa kwake? ndo mana vyuo vyetu vingi vinakosa sifa ya kuwa vya kimataifa.
Kwani mtu akitoka America ndio hatakiwi kufuata taratibu za Tanzania. Wewe unayejiona una IQ ya maana ndio bure kabisa kichwani, yaani hapo umeona kuwa umetoa hoja?
 
Wasiishie kwenye mavazi tu,maadili mengi yanakiukwa vyuoni.
 
Prof kasimama kwenye Maadili yetu Ukumbuke sisi Watu weusi ni Watu wa kukumbushwa Mda wote,ukikaa Kimya wanafunzi watavaa nguo za Ajabu ajabu matokeo yake ni majanga,Pia Ukumbuke si kila Tabia za Wamarekani ni Bora na Utamaduni wa America si Sheria eti lazima tuu-u-copy ,Tanzania ni Nchi huru ipo huru kujiamulia taratibu za kujistili mwili ,Mbona kule Uarabuni wazungu wakienda huko huvaa Kama wenyeji .
 
Kwani mtu akitoka America ndio hatakiwi kufuata taratibu za Tanzania. Wewe unayejiona una IQ ya maana ndio bure kabisa kichwani, yaani hapo umeona kuwa umetoa hoja?

Ni kweli sisi Tz ni Nchi huru hatuhitaji kuishi kwa ku-copy ya America ,kwanza ujue huko America kuna wala unga ,wavaa milegezo wengi hata wajinga Pia wapo wengi . Lazima tuishi kwa kukiamini kile cha kwetu.
 
Wasiishie kwenye mavazi tu,maadili mengi yanakiukwa vyuoni.

Kumbuka Tz kila kitu kinawezekana ndio Maana Maadili yameporomoka sana lakini Si Viongozi wa Upinzani wala Waziri au hata wabunge na Wasimamizi wa Sheria Kama jaji Mkuu ,IGP na Mwanasheria Mkuu wanaweza Kuthubutu Kupiga Marufuku Uvaaji wa Nguo chini ya kiuno ( kata .K. ) a.k.a MLEGEZO sasa ni Miaka 500 mlegezo umeshika kasi huku Uvaaji mwingine wa hovyo nao ukishika kasi zaidi, Sasa Hali ni Ngumu kuwazuia itakuwa ngumu sana Kama ilivyo Vigumu kwa Serikali kuhamia Dodoma. Prof tunakomba Profesa ujitahidi ikibidi aende Bungeni akaonane na Spika ili Wabunge wazinduke walikemee hili janga kwa vitendo.
 
Ni Tz pekee ambapo Viongozi wa juu wanaogopa kuwakemea wale wavaaji nguo zisizozingatia maadili Nchi zingine Viongozi wamethubutu Mfano nenda Rwanda au Uganda utaona .
 
Sifa ya msomi ni kujielewa na kujitambua,haiwezekani mtu unavaa skin tyt, half min skirt,open n' short tops kama unaingia club huku unaingia darasani,in short wanafunz wengi wa kike Muccobs wanavaa vibaya hawazingatii code of ethics,hongera Prof. Bee kwa kuliona hilo na kujitahidi kujitafutia ufumbuzi.
Ushauri: Angalieni wanafunzi wengi wa sheria wanavovaa kuzingatia legal attire ya black n white suti wanavopendeza na kuonekana kweli ni wasomi na wako tofauti na wenzao ambao unashindwa kujua anasomea course gani ukahisi labda kuna course mpya ya kujiuza.
Tatizo Prof yupo peke yake Hana Msaada ! Waziri na wabunge na vyama vya Upinzani wapo busy na mengine hapa kwenye maadili wamepapuzia sana,wanawaogopa Wavaa Milegezo wanadai ni wapiga Kura wao kwani wakithubutu kupiga marufuku Milegezo watakosa kura.
 
Sifa ya msomi ni kujielewa na kujitambua,haiwezekani mtu unavaa skin tyt, half min skirt,open n' short tops kama unaingia club huku unaingia darasani,in short wanafunz wengi wa kike Muccobs wanavaa vibaya hawazingatii code of ethics,hongera Prof. Bee kwa kuliona hilo na kujitahidi kujitafutia ufumbuzi.
Ushauri: Angalieni wanafunzi wengi wa sheria wanavovaa kuzingatia legal attire ya black n white suti wanavopendeza na kuonekana kweli ni wasomi na wako tofauti na wenzao ambao unashindwa kujua anasomea course gani ukahisi labda kuna course mpya ya kujiuza.

Hahahaha eti course ya kujiuza.
 
Kwani mtu akitoka America ndio hatakiwi kufuata taratibu za Tanzania. Wewe unayejiona una IQ ya maana ndio bure kabisa kichwani, yaani hapo umeona kuwa umetoa hoja?

tegemea prof atapata upinzani mkali sana kutoka watu wa dini wanayoiita dini huru isiongilia uhuru wa mtu
 
Tatizo lipo kwenye Mfumo wetu wa Elimu Maana Vijana wengi siku hz ni watukutu,wengi husoma kijanja janja kwa kuiba Mitihani,kukariri,nyenzo,nk hatuna wasomi wa Ukweli 60% wasomi ni Feki , ktk Mfumo huu ndipo pamezalishwa Wanafunzi wasiojitambua wapenda Mavazi ya ajabu ajabu,mavazi mitego,ni vigumu kwa sasa Maana Tabia imeshakuwa Sugu mno . Njia pekee ya kumaliza Tatizo ni kwashirikisha USAID ,Serikali za mitaa,wajumbe wa nyumba kumi,wakuu wa mashule,Vyuo,taasisi zote wavalie njuga kwa pamoja kinyume na hapo Profesa atajisumbua kupoteza mda.
 
SERA ya kudhibiti mavazi yasiyoendana
na maadili, yanayovaliwa na wanafunzi
wa vyuo vikuu hapa nchini, inaelezwa
itakuwa muarobaini kwa wanafunzi
husika. Akizungumza na waandishi wa habari
hivi karibuni, Mkuu wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Ushirika na Biashara
(MUCCoBS) cha Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA), Profesa Faustine Bee,
alisema serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha sera hiyo ambayo wanaamini
itakuwa msaada mkubwa wa kulinda
uvaaji vyuoni. Alisema kuwa chuo hicho pamoja na
vyuo vingine haviwezi kuwaruhusu
wanafunzi, hasa wa kike kuvaa mavazi
ya nusu uchi yanayoshushia heshima
vyuo na utu wa wahusika. Prof. Bee alisema kuwa pamoja na sera
hiyo kuwa hatika hatua za mwisho,
walengwa ambao ni wanafunzi, nao
watashirikishwa ili kutoa maoni yao juu
ya mfumo stahiki wa mavazi hayo na
kuongeza wakubali wasikubali sera hiyo ni mhimu kwa lengo la kudumisha
heshima ndani ya jamii. Alisema suala la nidhamu ni muhimu
kwa lengo la kujenga maadili mema
ndani ya jamii na kuongeza kuwa vijana
wengi wamejiunga na vyuo wakitokea
kwa wazazi wao, lakini wamekuwa na
uhuru wanaoutumia vibaya. Prof. Bee alisema kama vijana
wataendelea kulelewa kwenye maadili
mema, taifa litakuwa na kizazi chenye
staha. Kwa mujibu wa Prof. Bee, mchakato wa
sera hiyo ya mavazi ukikamilika
utarasimishwa rasmi na mwanafunzi
atakayeikiuka ataondolewa chuoni
hapo. Katika hatua nyingine, chuo hicho
kimekaribisha wawekezaji
watakaojenga hosteli na sehemu za
chakula kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya
wanachuo na wafanyakazi wake.
IFM na CBE walishaanza kitambo na wamefanikiwa sana...wajifunze kwao,internal system imebanwa yaani mpaka raha!
 
Enzi zetu sisi kuna kikundi kilikua kinaitwa "Punch".
Kikundi hiki kilikua kinasaidia sana 'kudhibiti' maadili pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Enzi zetu sisi kuna kikundi kilikua kinaitwa "Punch".
Kikundi hiki kilikua kinasaidia sana 'kudhibiti' maadili pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

hiv hawa si ndo walikuwa wanapiga m.a.n.d.e?
 
mbona kwenye swala la wanafunzi kucheleweshewa pesa yao ya field hajaongelea,angetumia uprofesa wake kuishauri serikali itumie njia gani kutatua kero za wanafunzi
 
Back
Top Bottom