Wanaotaka Utajiri bila kutaka kupata hasara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,493
5,528
Nimebahatika kufanya kazi na watu tofauti tofauti hapa nchini hasa wajasiriamli wadogo na wale wa kati.Binafsi pia nimefanikiwa kufanya aina mbalimbali za biashara,ndogo na za kati,local na internationa.Nimefanikiwa kupata hasara katika biashara na kupata faida na pia nimefanikiwa kufanya kazi za kuajiriwa katika katika kampuni ndogo kampuni kubwa na kampuni za kati.Nimebahatika pia kufanya kazi na watu wa mataifa mbalimbali Afrika na nje ya Afrika.

Katika hayo niliyapitia naweza kusema nimejifunza mengi sana na nimefanya makosa mengi sana na kupoteza mengi sana.Nimepata uzoefu mkubwa sana na pia bado ninajifunza mambo mengi sana.

Leo nataka kuzungumzia watu ambao wanataka kupata mafanikio na hawako tayari kutake risk.Nimekutana nao wengi sana.Watu wanaotaka urahisi wa maisha,uhakika na utajiri.Wanaotaka mafanikio ya ujanja ujanja.Watu hawa wengi wao huishia kupata kile wanachohofia.HASARA na KUSHINDWA.

Mifano iko mingi sana mingine ni ya watu niliokutana nao humu JF na wengine nje ya JF .

Kwa kawaida kabisa huwa ni vigumu kupata mafanikio bila kuwa katika hatari ya kupata hasara na kuwa tayari kupoteza.Iwapo unataka kufanikiwa ni lazima uwe tayari kujifunza,na katika hili lolote linaweza kutokea ikiwamo kupata hasara.Unapotaka kufanikiwa katika biashara na utajiri lazima urisk kiasi fulani na wewe uwe tayari kupoteza kiasi fulani.
Usitake njia rahisi ambayo ina kupa guarantee ya kufanikiwa bila kuelewa au kujifunza kitu kipya.Tafuta kujifunza na kupata uzoefu kwa gharama yoyote ikiwamo kutumia muda wako na pesa zako.

Kwa kutegemea malengo yako ni lazima uwe tayari kupoteza kiwango fulani cha pesa na muda katika kujifunza.Iwapo unalenga kufanya biashara za Milioni 100 na kuendelea basi uwe tayari kutumia angalau milioni ishirini kujifunza tu.Na iwapo unahitaji kufanya biashara ya angalau bilioni moja basi uwe tayari kutumia angalau milioni 100 kujifunza tu.Iwapo unataka kufanya biashara ya milioni kumi basi uwe tayari kutumia angalau milioni moja kujifunza tu.Na iwapo unataka kufanya biashara ya Milioni moja basi uwe tayari kutumia angalau TZS laki moja kujifunza.

Ninaposema uwe tayari kujifunza simaanisha kwenda darasani tu bali ni kwa kutembelea maeneo,kutafuta taarifa,kutafuta network ya watu nakuelewa zaidi kuhusu fursa iliopo na faida zake na gharama zake pamoja uwezo wako wa kuweza kuitekeleza.

Unapotaka kupata mambo makubwa lazima uwe tayari kutoa pia.Ukiwa mzito kutoa utakuwa unapoteza tu kila siku bila kujua sababu ya kupoteza.

Nawatakia kila heri katika mapambano yenu ya maisha.Mbarikiwe
 
Nice
 
Back
Top Bottom