wanaotafuta wachumba wa ukweli hawa hapa

mabwepand

Member
Jul 16, 2012
86
22
Mm ni kijana ambaye Mungu Mwenyezi kanibariki katika maisha hela ya kutafuta mboga haipigi chena nimemaliza chuo kikuu plus elimu nyingine ya juu,katika mahusiano nilishapita kwingi na kuwa na wachumba ambao hatimae wlikuja niumiza na kusema hata kuoa sitaki tena kwa kipindi kirefu kidogo madada wa mjini kama ujuavyo wapo kimasilahi zaidi ya upendo nikawa naomba Mungu anipatie msichana wa kufanana nami awe mke wangu,Baada ya muda nilirudi kijiji kwenda kutafuta mke kiukweli nashukuru nilipata mke tena nasema mke ni mrembo mzuri ana ucha Mungu na isitoshe nilimkuta bikra kwa hiyo vijana wenzangu madada wa mjini tuachane nao au tuwe makini nao ila ujue mke wa ukweli wapo kijiji na tusiwadharau wazee wetu wakati wa kuoa ni vyema ukawataarifu nao wanaweza kukupatia mke mwema pia,ila turudi vijijini mwetu kuna wanawake wenye heshima na wazuri.Happy new year all ladies and Gents
 
ngoja aje ajanjaruke mjini ndio utashangaa na roho yako...kwanza wee na yeye the way u see the world ni tofauti...utatiambia
 
Mkuu Hongera sana kama wewe ulibahatika, Nadhani ndio Mungu alikujibu hivyo WEWE, ila kusema wake wako vijijini au mijini sio sahihi mkuu. Mi nadhani tuendelee kuomba kama wewe ulivyoomba Mungu naye atatujibu kwa namna yake, kama ni kijijini sawa, mjini sawa, nje ya nchi sawa.

Maneno ya hekima yanasema:-
''Mithali 19 : 14 - Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana''
 
Kuna ndugu yangu naye aliamua kama wewe; lkn sasa hivi anajuta maana Mnyamwezi Yule kalijua jiji na hivi mzuri. Mwanzoni tulifikiri kaka yetu ana makosa hasa baada ya kuwa na uhusiano mdada mwingine.
Lkn baada ya kikao cha Mke na Mume; tulinyanyua mikono.

Hivyo kama umepata Mke mwema shukuru Mungu; bado kuna waliopata virgins mjini na waliopata ****** bush.

Point niliyoiona ni kushirikisha watu hasa wanaomfahamu binti ktk utafutaji; lkn swala la mjini vs vijijini; utuulize sisi tunaointeract na watu wa vijijini.
 
Mkuu nakushauri huyo mke wako mpya iwapo unataka aendelee kuwa mke mwema na asiuumize moyo wako, endelea kuishi naye huko huko kijijini. Lakini ukimleta mjini akishajanjaruka, kosa.
 
wewe nae kwa hiyo ukimkuta bikira ndio hamgombani?hajikukutenda?hilo ni bomu ndugu yangu subiri lilipuke puuuuuuuu!af kuna tofauti kubwa sana ya aliyesoma na ambaye hajasoma.
 
Ha ha ha haa haaaaaaa! Mmmeanza kutangaza kuwa wake wanapatikana vijijini?! Ngoja batoto ba mujini batangulie huko kubasubirini. Munacheza na batoto ba mujini nyie? Lol!
 
Hahahahah so batoto ba mujin banaweza kutangulia kijiji kuwangoja eeeh?? Ujanja kupata lol
Ha ha ha haa haaaaaaa! Mmmeanza kutangaza kuwa wake wanapatikana vijijini?! Ngoja batoto ba mujini batangulie huko kubasubirini. Munacheza na batoto ba mujini nyie? Lol!
 
Hata mjini mabikra tupo!!!!!
hungera kwa kupata muke, ila mjini shule shamba kilimo!!!!!
 
Mm ni kijana ambaye Mungu Mwenyezi kanibariki katika maisha hela ya kutafuta mboga haipigi chena nimemaliza chuo kikuu plus elimu nyingine ya juu,katika mahusiano nilishapita kwingi na kuwa na wachumba ambao hatimae wlikuja niumiza na kusema hata kuoa sitaki tena kwa kipindi kirefu kidogo madada wa mjini kama ujuavyo wapo kimasilahi zaidi ya upendo nikawa naomba Mungu anipatie msichana wa kufanana nami awe mke wangu,Baada ya muda nilirudi kijiji kwenda kutafuta mke kiukweli nashukuru nilipata mke tena nasema mke ni mrembo mzuri ana ucha Mungu na isitoshe nilimkuta bikra kwa hiyo vijana wenzangu madada wa mjini tuachane nao au tuwe makini nao ila ujue mke wa ukweli wapo kijiji na tusiwadharau wazee wetu wakati wa kuoa ni vyema ukawataarifu nao wanaweza kukupatia mke mwema pia,ila turudi vijijini mwetu kuna wanawake wenye heshima na wazuri.Happy new year all ladies and Gents

Usidharau NAZI....EMBE tunda la msimu!!!
 
Hongera. Hayo ni majibu ya maombi yako ndg yangu, mshukuru Mungu na endelea kumuombea mke wako mpenzi ili asibadilike, na mumche Mungu wote.

Ila ndg zangu, mke mwema hutoka kwa Bwana, mke mwema hatoki kijijini au mjini, haijalishi ametoka pembe gani ya nchi/dunia, Mungu yeye hana mipaka, humpa mtu kulingana na anavyoomba au anavyoona yeye kuwa inafaa
 
Binafsi naona kama ni mapema sana kuanza kummwagia misifa hapa jamvini !! sana sana ungeishi nae japo miaka mitano hivi manake ndoa ni safari na safari ni hatua, hubadilika kama kinyonga hawa viumbe !!
 
Salam mkuu sina nia ya kukukatisha tamaa bali ningependa kukupa matumaini zaidi. Ukweli ninaye mke wa aina hiyo na kwa sasa naugulia. Nakushauri umuendeleze kama hana elimu na mfundishe kwa upole na uangalifu sana kaka.

Nadhani kazi unayo, maana unaweza kujuta zaidi ya pale mwanzo. Usiyazingatie sana haya nisemayo maana ni mawazo yangu tu. chambua na fanyia kazi ya maana.
 
mapema sana mkuu mshukuru mungu kwa kupatia mke mwema asijechanganyikia na atakayoyaona mjini ukaachwa solemba
 
Back
Top Bottom