Wanaorejesha fedha za EPA watajwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaorejesha fedha za EPA watajwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 23, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Date::10/22/2008
  Wanaorejesha fedha za EPA watajwe

  Maoni na Uchambuzi
  Mwananchi

  WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo amefahamisha kuwa hadi sasa kiasi cha Sh61 bilioni kati ya Sh133 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT), zinazodaiwa kuliwa na mafisadi zimeisha rejeshwa serikalini tangu ufuatiliaji wake uanze Januari, mwaka huu kwa amri ya Rais Jakaya Kikwete na Bunge.

  Waziri Mkulo alisema mbali na fedha hizo, mali zisizohamishika zimekamatwa na kwamba kufikia mwishoni mwa mwezi huu kiasi kikubwa cha fedha kitakuwa kimekusanywa.

  Oktoba 30, mwaka huu ndiyo siku ya mwisho kwa mafisadi wa EPA kurejesha fedha hizo kama alivyoahidi Rais Kikwete wakati akilihutubia Bunge la Bajeti mwaka huu.

  Hata hivyo taarifa hiyo inaendelea kuleta utata kama kweli zimekusanywa, kutokana takwimu tofauti zilizowahi kutolewa siku za nyuma. Awali alisema zimekuwanywa Sh60 bilioni, baadaye Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikasema zimerudishwa Sh64 bilioni na Rais akaliambia Bunge kuwa ni Sh53.9 bilioni. Swali letu ni kwamba tufuate taarifa ipi, ya Mkulo, ya CCM au Rais?

  Tunashauri kwamba ili kuwafanya wananchi waiamini taarifa hiyo, serikali inatakiwa kuwa wazi kwa kueleza fedha hizo zimetunzwa wapi, kutoka kwa nani na mali zilizokamatwa ziko wapi ni za aina gani (kama ni nyumba ngapi, mashamba na nyinginezo).


  Serikali inatakiwa kufahamu kwamba, mpaka sasa Watanzania wengi ukiachia mbali viongozi na wapambe wa CCM, hawaamini kuwa fedha hizo zipo, hivyo ni wajibu wake kuwatoa wasiwasi huo kwa kuweka wazi takwimu zote za urejeshaji na hatua kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote na si kuendelea kutoa maneno ya kisiasa ambayo wamechoka kuyasikia.
   
Loading...