Wanaonunua pesa chakavu pamoja na Dola wanazipeleka wapi?

zabron k

JF-Expert Member
Nov 11, 2015
923
1,058
Wakuu naomba kuuliza,

Karibu miji yote mikubwa kuna wafanyabiashara ndogo ndogo wananunua fedha chakavu na dola chakavu.

Hizi fedha wanapeleka wapi au wanafanyia nini?
 
Wanapeleka BOT kubadilisha,haukatwi chochote ukipeleka buku unapewa buku,ila kama imeharibika sana kuna sehemu unapita unakuta makaratasi na gundi,unaziweka vizuri kisha unapitisha kwenye dirisha ambalo lipo hapo,inahakikiwa kisha unaelelezwa dirisha jingne la kwenda kupokea chako
 
Kumbe ni fursa aiseeeeeeeeeee
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna mtu ainiuzia 5000 mbovu kwa 2000. Nilipoenda bank CRDB Mafinga nilipewa 5000 mpya. So nafikiri wanazipeleka bank kubadirisha kwa thamani halisi huku mtaani wananunua kwa thamani ya chini sana.
 
Ndio wanazinunua kwa bei ya chini tofauti na thamani yake na wakizipeleka benki wanachukua yenye thamani ile ile bila makato yoyote.
 
Kwa noti ni benki yeyote unapewa mpya ila kwa sarafu wanaweza kukuambia upeleke Bot
 
Wanapeleka BOT kubadilisha,haukatwi chochote ukipeleka buku unapewa buku,ila kama imeharibika sana kuna sehemu unapita unakuta makaratasi na gundi,unaziweka vizuri kisha unapitisha kwenye dirisha ambalo lipo hapo,inahakikiwa kisha unaelelezwa dirisha jingne la kwenda kupokea chako

Je inahitaji leseni/vibali kufanya biashara hii ya kununua fedha?
Na je nikipeleka dollar, napewa dollar au wanaibadilisha into tsh?
 
Back
Top Bottom