Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.
Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?
Ni kweli, hasa hawa watu ambao wameishi kwa dhiki huwa wanasumbua sana
Wengine wakipata pesa wanakata mawasiliano kwa kuwa wanachoka kuombwa pesa kila wakati. Wabongo mmekuwa omba omba mno ndio maana watu wenye pesa wanawachunia!Ni kweli kabisa watu walioishi au kukulia kwenye dhiki, wakija kupata hela mbona utakoma yaani wanajifanya sio wabantu kabisa. Mawasiliano hawataki kabisa yaani wanaishi kama wanaigiza vile. Vijitu vya hivyo vinakera sana.
Ugeni na ulimbukeni unapochanganyika pamoja
Mkuu pengine mko wengi mnaotaka kumkopa jamaa, na wewe pata zako halafu mringishie ndo dawa yake.Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.
Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?