funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 38,534
- 31,198
Habari wanajamvi.
Nimeona nilete habari ya Mhudumu huyu wa kanisa katoliki ambaye kwangu mimi namuona akiuishi ukatoliki wa kweli na mwenye kuendelea kutukumbusha maana halisi ya wito. Japo media za Tanzania hazimtaji au kuonesha matukio yake mara kwa mara.Hakika nimevutiwa naye na imani yangu kwake na waliomuibua ni kubwa sana.
Mstaafu Paulo Runangaza Ruzoka wa Jimbo kuu la Tabora. Ni katika muktadha huu, Kardinali Protase Rugambwa, “Kardinali Padre” Dominika tarehe 18 Februari 2024, anakabidhiwa Kanisa la “Santa Maria in Montesanto”
Vatican
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.
Makardinali kimsingi ndio washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro ili kukoleza juhudi za toba, haki, amani na maridhiano; kwa kukuza na kudumisha utu na heshima ya binadamu, ili watu waweze kuishi katika mazingira bora zaidi. Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 9 Julai 2023 aliwateuwa Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali watatu ni wale ambao wamejipambanua katika huduma kwa Kanisa na watu wa Mungu katika ujumla wao.
Makardinali wapya wakasimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Makardinali ulioadhimishwa tarehe 30 Septemba 2023 mjini Vatican. Hawa ni Makardinali wanaoonesha ukatoliki wa Kanisa, wanaotumwa kutangaza na kushuhudia upendo wa huruma ya Mungu kwa watu wote wa Mataifa. Makardinali hawa wakaingizwa kwenye Jimbo kuu la Roma ili kuonesha mahusiano na mafungamano kati ya Khalifa wa Mtakatifu Petro na Makanisa mahalia yaliyoenea sehemu mbalimbali za dunia.
Uteuzi na hatimaye, kusimikwa kwa Makardinali wapya ni changamoto kubwa inayowataka kujizatiti zaidi katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo Yesu, kwa kuhakikisha kwamba, imani inamwilishwa katika matendo; daima wakijielekeza zaidi katika huduma kwa watu wa Mungu sehemu mbalimbali za dunia. Makardinali wanaojitambulisha kwa mavazi mekundu, wanaitwa kusadaka maisha yao kwa ajili ya Kristo Yesu na Kanisa lake, tayari kuwashirikisha watu wa Mataifa, ile furaha ya Injili.
Ni mwaliko wa huduma makini kwa watu wa Mungu. Jicho la kibaba linalooneshwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa kutoa kipaumbele cha pekee kwa: Amani, mazingira, maskini na wale wote wanaosukimizwa pembezoni mwa jamii, ni chachu ya matumaini na mapendo ambayo yanapaswa kutawala katika maisha ya watu!
Nashukuru kwa maono na macho mapana ya Vatican na tuendelee kumuombea utumishi mwema!!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Nimeona nilete habari ya Mhudumu huyu wa kanisa katoliki ambaye kwangu mimi namuona akiuishi ukatoliki wa kweli na mwenye kuendelea kutukumbusha maana halisi ya wito. Japo media za Tanzania hazimtaji au kuonesha matukio yake mara kwa mara.Hakika nimevutiwa naye na imani yangu kwake na waliomuibua ni kubwa sana.
Vatican
Kardinali Protase Rugambwa Kukabidhiwa Kanisa Jimbo Kuu la Roma: Utume
Kardinali Protase Rugambwa, “Kardinali Padre”, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tabora, Dominika tarehe 18 Februari 2024, anakabidhiwa Kanisa la “Santa Maria in Montesanto”, lililoko kwenye Barabara la Babuino, namba 198, Roma, kuashiria kwamba, Kardinali Rugambwa sasa ni sehemu ya Wakleri wa Roma, wanaounda Baraza la Makardinali lenye jukumu la kumsaidia Khalifa wa Mtakatifu Petro katika shughuli zake za kichungaji kama Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Roma.Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.