Wanaohujumu vita dhidi ya ufisadi ni wengi

Chunda

Senior Member
Apr 7, 2016
182
251
Wapo wengi wanaohujumu jitihada za Mh. Rais katika kupiga vita ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Wapo baadhi ya watendaji wakubwa kabisa Serikalini ambao kwao juhudi za Mh. Rais kupiga vita ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka hazina maana kwao

Hayo yameshuhudiwa pale ambapo Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi Wizara ya Elimu ameonesha dhahiri akishirikiana na Mkuu wa Taasisi ya umma kwa nia ya kutaka kumhujumu Rais katika vita dhidi ya ufisadi.

Kwa kitambo kirefu Mkurugenzi huyu wa Wizara Mheshimiwa Thomasi Katebalirwe amekuwa akinufaika na fadhila kutoka Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha huku akijisahau kwamba zama za kutetea na kufurahia ufisadi zimekwisha kwa anavyotamani iwe Mh. Rais JPM.

Mkurugenzi huyu huku akifahamu kuwa yeye ni jicho la Wizara katika chuo, alikaa upande wa uongozi wa chuo kuhakikisha ufisadi uliofanywa na unaoendelea kufanywa na menejimenti ya chuo unalindwa na kuendelezwa.

Mkurugenzi huyo wa Wizara alinyamazia na kutetea mkuu wa chuo pale alipomweka Dkt Masudi Senzia kuwa mjumbe wa Bodi ya chuo huku yeye na Mkuu wa chuo wakitambua kwamba Dkt Masudi Senzia ni Makamu Mkuu wa Chuo. Baaba ya malalamiko mengi, Mkuu wa Chuo alimuondoa Dkt Masudi Senzia kutoka kwenye Bodi ya Chuo kwa kile alichoita kwamba muda wa Dkt Masudi Senzia kuwa kwenye Bodi ya Chuo ulikwisha kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha.

Kama hiyo haitoshi, Mkurugenzi huyu wa Wizara alinyamazia na kutetea pale ambapo wajumbe wengi wa Bodi ya chuo kuwa sehemu ya familia ya mkuu wa chuo na wengine ni wapenzi wa Mkuu wa Chuo. Mkurugenzi huyu wa Wizara alinyamazia na kutetea yaliyofanyika tu kwa sababu ananufaika na ufisadi unaofanywa na Mkuu wa Chuo na Bodi kwa ujumla.

Ufisadi mwingi wa chuo umeripotiwa kwenye vyombo vya habari na bado utaendelea kuripotiwa kwa sababu madudu yaliyofanywa na menejimenti ya chuo kwa kushirikiana na mkurugenzi wa Wizara ni mengi na mengine yanatisha.

Hivi sasa kuna kampeni za chini kwa chini zinazoongozwa na Mkurugenzi huyu wa Wizara kuhakikisha uwakilishi unaostahili kuwepo ndani ya Bodi ya chuo unakuwa kwa masilahi yake na Mkuu wa chuo kwa gharama/hasara ya chuo na Serikali.

Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya Bodi nyingi za Taasisi za elimu ya juu kama Chuo cha Ufundi Arusha kunakuwa na uwakilishi wa angalao wafanyakazi wawili kwa maana ya wanataaluma (Academic Staff Association) na Chama cha wafanyakazi (Trade Union). Lakini kinachofanywa na Mkurugenzi huyu wa Wizara pamoja na mkuu wa Chuo ni kutaka kufifisha uwakilishi huo kwa faida binafsi ya Mkuu wa chuo, Mkurugenzi na wajumbe wengine wa Bodi wakilenga kutaka kuendelea na ufisadi wao.

Kwa taarifa, Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha haishirikishi Baraza la wafanyakazi katika kujadili mapato na matumizi ya chuo. Kwa ujumla hakuna chochote chenye maslahi kwa wafanyakazi na Taifa kinachojadiliwa na Baraza la wafanyakazi la chuo. Badala yake kila kitu hujadiliwa na kupangwa na Bodi ya chuo ambayo kila siku Mkuu wa chuo akishirikiana na Mkurugenzi wa Wizara huhakikisha wafanyakazi hawapati nafasi ya kushiriki inavyostahili kwenye Bodi hiyo kwa lengo la kuhakikisha hakuna uwakilishi wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi ili kudhibiti ufahamu wa wafanyakazi juu ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka vinavyofanywa na Mkuu wa chuo, akishirikiana na Bodi ya chuo.

Mkuu wa chuo amefanya kila jitihada na kuhakikisha ndani ya Bodi kunajaa wajumbe watakao ungana naye katika kufanya ufisadi. Cha ajabu ni sasa anapoanzisha matatizo mapya kwa kutaka kuminya uwakilishi wa wafanyakazi akisaidiwa na Mkurugenzi wa Wizara

Wigo wa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni mkubwa pengine kuliko wengi tunavyoweza kufikiri. Kama jitihada za makusudi hazitafanywa na watanzania wenye mapenzi mema dhidi ya watendaji wachache wenye nia ovu ya kulihujumu taifa, matumaini ya kulifanya Taifa la Tanzania kuwa mahali pazuri pa kuishi kama anavyotamani Mh. Rais, inaweza kuwa ndoto.

Hatua ya Mh. Rais kutumbua majipu hadharani inabidi ziungwe mkono kwa dhati. Ukitafakari kwa makini yanayofanywa na mafisadi, mengine yanaudhi sana. Mtu akipewa kazi ya umma anatakiwa kuifanya kwa uadilifu na heshima
 
Inafahamika, huyo mkurugenzi wa wizara pamoja na Nyuhumwa wa DIT walishapewa za kustaafia. Katika Tsh 3.5 bilioni zilizoliwa kifisadi kutokana na miradi mbalimbali ya chuo walipewa mgao wao wa kutosha.

Wakubwa hao hawana hofu hata wakistaafishwa kwa manufaa ya umma, walikwishamaliza kazi yao. Kwa sasa wanakula faida tu.
 
Back
Top Bottom