Rais Samia awataka Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutumia maarifa waliyoyapata katika kazi zao kwa manufaa yao na nchi zao

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
941
614
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wahitimu wa Kozi ndefu ya mwaka 2023/2024 katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutumia maarifa waliyoyapata katika kazi zao kwa manufaa yao na nchi zao.

Rais Dkt. Samia ametoa wito huo leo wakati wa Hafla ya Mahafali ya 12 ya Chuo cha NDC iliyofanyika katika Chuo hicho kilichopo Kunduchi.

Aidha, Rais Dkt. Samia amewarai wahitimu Watanzania na wa mataifa ya kigeni kutoka nchi 15 kuendeleza ushirikiano ili kuweza kupata suluhu za pamoja katika kutatua changamoto za kidunia kwa utaalam.

Rais Dkt. Samia pia amesema Serikali itaendelea kukiunga mkono chuo hicho ili kiendelee kutoa michango chanya katika masuala ya kiusalama kitaifa, kikanda na kimataifa.

Vile vile, Rais Dkt. Samia amekitaka Chuo hicho kuendelea kuwekeza kimkakati kwa taifa kwa kuunga mkono tafiti zenye tija na kushirikiana na taasisi zingine za kitafiti ili kuiwezesha nchi kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

IMG-20240727-WA0198.jpg

View attachment 3054573
View attachment 3054578
Wosia huu ni mzuri, wakatumikie nchi zao vizuri, Kwani kilichowekezwa kwao ni kikubwa. Sio Kwa kwenda kuwaibia nchi zao Kwa faida ya familia zao au watoto wao. Kwani ni hela za umma zilizowafikisha hapo na sio familia zao au watoto wao.
 
Back
Top Bottom