Wanaodharau kusajili line za simu watafungiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaodharau kusajili line za simu watafungiwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, December 24, 2009 2:43 PM
  MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewasisitiza wananchi wanaoendelea kudharau zoezi hilo kuwa endapo kama hawatasajili line hizo zitafungiwa. Zoezi hilo ambalo lipo ukingoni, ambapo mwisho wa usajili wa line hizo ni ifikapo Desemba 31, mwaka huu, na kwa wale ambao hawatafanya hivyo hadi ifikapo Januari mwaka huu laini zao zitafungiwa.

  Akizungumza leo asubuhi, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungi, amesema kwa Tanzania kuna laini za simu zaidi ya milioni 15 ambapo hadi sasa nusu tu ya ndizo zimesajiliwa.

  Amesema malengo ya TCRA ni kusajili angalau nusu ya laini hizo ambapo wananchi wameitikia wito na kuvuka lengo hilo.

  Ameongeza kuwa mbali ya mafanikio hayo pia wamebaini kuwa wakati wakifikia kilele cha usajili huo, TCRA inakabiliwa na changamoto mbalimbali.


  Hivyo amewataka wananchi kutumia fursa waliyopewa hivi sasa kwa kuhakikisha kuwa hadi ifikapo Desemba 31, wawe wamejiandikisha ili kuepuka usumbufu watakaoupata baada ya operesheni hiyo kuisha.

  Kila pande ya jiji na kwingineko watu wamefurika katika zoezi hilo ambapo limebaki siku kadhaa na watu kuonekana kupata muamko wa sula hilo na watu hushonana kwa mawakala mbalimbali wa makampuni ya simu kusajili laini hizo.

  Kutokana na watu kuwa wengi mawakala wengine wa makampuni ya simu huwa toza wananchi kusajili line hizo kwa kuwa wameona watu ni wengi kupita kiasi.
  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3799126&&Cat=1
   
Loading...