Wanaobakwa wasioge, wasibadili nguo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaobakwa wasioge, wasibadili nguo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 9, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewatahadhalisha Wanawake watakaobakwa kutooga au kubadilisha nguo kwa sababu kufanya hivyo kunapoteza ushahidi wa kumtia hatiani Mtuhumiwa.

  Taarifa iliyoandaliwa na Tamwa kupitia Mtandao wake wa kijamii zinasema, Madaktari nchini wameshauri wanaobakwa kufika haraka kituo cha polisi kuchukua PF3 na kuipeleka hospitali kwaajili ya kupata matibabu ikiwamo dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.


  Akinuliwa na Chama hicho, Dk Zuberi Mzige wa hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es S alaam alisema , kumekuwa na tabia ya watoto wa kike wanaofikishwa hospitalini baada ya kubakwa kutokuwa na ushahidi kutokana na kuoga au kubadilisha nguo.

  “Wengine wanafikishwa hospitalini wakiwa wamecheleweshwa hivyo kuwa kwenye hatari ya maambukizo ya HIV” taarifa ilimnukuu.Naye Dk Prisca Berege anayeshughulikia magonjwa ya watoto katika hospitali ya Mwananyama alisema , mji wa Dar es Salaam una tatizo la ubakaji hasa kwa watoto.

  Alizungumza hayo na Wanahabari walioshiriki katika mkutano wa utafiti wa maswala ya ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na TAMWA hivi karibuni katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  “Kila siku hospitali ya Mwananyama lazima tupokee watu watatu waliobakwa ambao ni wanawake na watoto” alisema Dk Barege.

  Dk Barege aliwashauri wazazi kuepuka kuwatuma watoto wao nyakati za usiku na kuwatahadharisha watoto wa kike kuwa makini na uhusiano baina yao na wanaume waliozoeana.

  Alitoa mfano wa binti mmoja ambaye hivi karibuni alibakwa mchana na mwanaume aliyemwamini kama kaka n amwajiri wake baada ya kumwita nyumba ni kwake ili wapange kazi ya kufanya.
   
 2. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ukweli mtupu.Lakini,yategemea kama mhusika anataka kufungua mashtaka...
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kimtazamo akibaki hivyohivyo sio rahisi zaidi kupata mimba??labda wanasayansi watusaidie hapa
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  janabaaaaaaaaaaaaaaa jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...........lol haya sasa utapandaje gari na janaba? si utawanukia wengine?
   
Loading...