Wanaoathiri amani Tanzania hawa hapa

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,181
5,429
Wakuu habarini!. Hakuna mtu hata mmoja ambaye hadi sasa hajaathirika na siasa za Tz kwa namna yoyote ile. Lakini pia hakuna mtu ambaye hadi sasa hajaathirika na imani za kidini za Tz hapa. Yaani vyama vya siasa na siasa zake vimewaathiri wasio wanasiasa na wanasiasa pie kama ambavyo imani za dini zilizopo nchini zilivyowaathiri watu walio waumini wa dini hizo na wasio waumini pia.

Naandika andiko hili kwenu watanzania wote kwa upendo mkuu juu yet kutokana na muendelezo wa matukio mbalimbali yanayotukuta sote wenye dini na wasio na dini,wanasiasa na wasio wanasiasa.

Ninyi wakristo ktk dini mmefundishwa maana ya upendo bila ubaguzi tena huyo yesu mmwabuduye akawaambia wanafunzi wake ambao ni nyinyi kuwa enendeni ulimwenguni kote (maana yake kwa watu wa rangi zote, mataifa yote, imani zote) mkawafundishe atakayeiamini (maana yake Hiari) hiyo injili mumbatize kwa jina langu. Kama mwongozo huo ni sahihi kwanini wakristo wawachukie wasioamini imani yao. Kwanini viongozi wa serikali wa kikristo wawatese wasio wakristo.

Vivyo hivyo mtume Mohammad kupitia mafunzo yake ndani ya kurani tukufu (kwa waislamu waaminio) hajabagua taifa, dini ya mtu wala ukoo wake ameungana na mtume Paulo wa wakristo aliyesema kwa watu wake kuwa nijapofanya mambo yote kama sina upendo mimi si kitu.

Ktk nchi hii hii ambayo wakristo mnajivuna ni ya kikristo tumeshuhudia waliowaislamu na wasio wakiuawa kinyama wakisulubiwa kwa kesi za ajabu.Wafanyao haya kama wakristo wana wachungaji na maaskofu lakini mafundisho hawayafuati.

Vivyo hivyo nchini mnaojivuna kuwa na imani ya Muhammad tumeshuhudia watu wa imani ya kikristo na wasio pia wakiuawa kikatili ktk taifa hili na kuteswa mno. Wafanyayo hayo huingia na kutoka misikitini wakimwacha shehe na mafundisho yake wasiyafuate.

Viongozi wa dini ktk taifa wanapokuwa na amani ktk dini zao hujenga upendo mkubwa ambao huteleza mpaka ikulu ya nchi yao na kuleta utawala bora kwani viongozi hao ama ni waislamu au wakristo ama vinginevyo. Kukosekana kwa amani ktk dini zetu kumepelekea pia kukosekana kwa amani ikulu.

Kama viongozi wa serikali waliopo watakuwa na amani ya kweli huko basi amani hiyo itasaidia waumini ktk nchi zao kupewa ulinzi sawa usio wa upendeleo.

Tunashuhudia muislamu ama mkristo akimgomea muumini mwenzake cheo halali alichoshinda serikalini ama huko wanakoabudu utadhani ukiishi bila cheo utakufa. Mbona wenzenu hatuna vyeo na maisha yanasonga. Wanasiasa mmekuwa chanzo cha machafuko kama ambavyo pia wanadini mmetumika vibaya na wanasiasa.

Nje ya dini na siasa sisi sote ni wamoja tusikubali kutumika vibaya kwa maslahi ya waroho wachache. Fuateni ktk roho na kweli mafundisho ya mitume wenu mkapate kumbariki mwenyezi Mungu wenu. Vyote mnavyotoleana na kumwagana damu mtaviacha lakini ukweli uliopo ndani ya vitabu vyenu vitukufu utabaki kuwa kweli tupu milele.

Nawatakia tafakuri njema, unapotaka kujadili haya kwa afya njema mfikirie jirani yako kuwa ni bora kuliko wewe bila kujali utofauti ama usawa wa imani zenu. Mungu tupatie upendo wa kweli watu wote usio wa kinafiki.
 
Back
Top Bottom