Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania: Haki za Binadamu zinapozingatiwa amani inaendelea kustawi katika Jamii zetu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,911
13,664
WhatsApp Image 2024-09-24 at 18.58.43_f297dcd1.jpg
Katika kuelekea Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 53 wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania, Jumuiya hiyo imesisitiza umuhimu wa kuzingatia Haki za Binadamu kama nyenzo ya kustawisha amani nchini.

Akizungumza Septemba 24, 2024 ikiwa kuelekea mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 27 - 29 Septemba 2024 Katika eneo lake maarufu la Ahmadiyya lililopo Kitonga, Kata ya Mongola, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Seif Hassan.

Amesema misingi ya Dini ya Kislamu inasisitiza na kuwahasa watu kuzingatia Haki za Binadamu bila kujali nafasi zao.
WhatsApp Image 2024-09-24 at 18.58.42_6c8185f4.jpg
Ambapo amesema jamii ikijenga utamaduni wa kuzingatia Haki za Binadamu ni njia muhimu ambayo inaweza kufanya amani iendelee kustawi, amesema kuwa suala la Haki za Binadamu ni la watu wote.

Pia, Seif Hassan ameeleza katika mkutano huo watakuwa na mada mbalimbali ambazo zitajielekeza katika misingi ambayo Binadamu wakiishi itaendelea kuchochea amani katika jamii na Nchini kwa ujumla, minongono mwa mada hizo ni masuala yananyogusa haki za Binadamu na Upendo.

" Mkutano huu unafanyika ili kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwa washiriki, kupata Taqwa, kumjali Mwenyezi Mungu, kuepukana na mabaya, kupata moyo wa huruma, na kuongeza upendo baina yao, na wawe mfano wa kujenga udugu baina yao, na unyenyekevu na ukarimu na tabia ya ukweli vipatikane ndani," amesema wakati akisoma tamko hilo.

Ameongeza "Kwenye Mkutano huu pia hualikwa viongozi wa Kitaifa wa Kiserikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini mbalimbali na jamii kwa jumla ili nao washiriki katika kutoa nasaha zao."

Aidha, amebainisha wazi kupitia mkutano huo Waumini watapata nafasi ya kuzisikiliza hotuba na nasaha za Wataalamu wa Jumuiya ambapo miongozo mwa mambo yatakayozungumzwa ni namna bora ya kuwalea Watoto ikiwemo kujali elimu yao ya dini, kujitahidi kuwa raia wema kwa kuishi kwa amani na watu wote na kuwa watiifu kwa Sheria za nchi.

Sanjari na hilo anaongeza "Pia waumini watakumbushwa juu ya umuhimu wa kujiepusha kuchanganya dini na siasa kwani jambo hilo huleta mkanganyiko na kuzalisha mianya ya ama wanasiasa kuitumia dini vibaya au watu wa dini kuitumia siasa vibaya kwa ajili ya maslahi yao binafsi."

Vilevile, Naib Amir ( Deputy Head) Abdul Rahman Mohammed Ame amesema kumekuwepo na mitazamo kindhani kuhusu kuchnganya dini na siasa, amedai kuwa mada hiyo itajadiliwa vizuri ili wananchi na viongozi waongeze uwelewa zaidi juu ya suala hilo.

Upande wa Amir (Missionary Icharge) Khawaja Muzaffar Ahmad) amesema katika mkutano huo wanatoa nafasi kwa watu wote bila kujali dini zao, kushiriki na waandaaji kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa nyenzo ya kustawisha amani.

"Ningependa kuhitimisha kwa kuwakaribisha watu wote kwa furaha na moyo mkunjufu kwenye mutano huu wa 53 kwa kutumia kauli mbiu yetu maarufu ya Upendo Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote."

Kwa mujibu waandaaji imeelezwa kwa mgeni rasmi katika Mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Itakumbukwa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ni Jumuiya ya kimataifa inayopatikana kwenye zaidi ya Nchi.

212 duniani ikiwa chini ya kiongozi mmoja (Khalifa mtukufu), ambapo inaelezwa kuwa kwa Tanzania wanayo matawi zaidi ya 300.

Pia soma ~ Wazee wa Jumuiya ya Ahmadiyya wakutana Dar kujadili changamoto za maadili na amani
 
Back
Top Bottom