Wanangu ngojeni niwape hili....

Kuna wenzako hata hiyo bahati ya kuitwa hawajapata ndani ya huu mwaka mzima.
 
Umeitwa kujitolea kwa fani uliyosomea au ni kubeba mizigo? Nifafanulie nitakupa mrejesho
 
Komaa mjomba tupo/wapo tu/wanaotamani walau nafasi ya kujitolea ila hawapati, mbali na malipo kuna raha yake na heshima yake kuamka asubuhi na kwenda kazini yani unajua ukiamka unaelekea wapi sio ukiamka viulizo vimekuzunguka kichwa kizima.
 
Mwanzo ulikubaliana upewe posho? Kama hujakubali basi sulubika siku za huzuni ni nyingi zaidi kuliko za furaha.

Mwisho wa siku piga kura kuichagua ccm tena.
 
Komaa tu jombaa..ndo ujue ccm haina undugu na myonge..hapo bado bodi ya mikopo inakusubiri kwa 15% na retention fee 6%..Usisahau kusifu na kuabudu kwa mapambio makuu kwenda kwa malaika mkuu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umeitwa kujitolea kwa fani uliyosomea au ni kubeba mizigo? Nifafanulie nitakupa mrejesho
Nilijipendekeza kwa Steshen master alivyoletwa hapa Arusha, akawa rafiki yangu akaniambia kama atapewa kibali cha kuajiri atanipa nafasi. Kibali hakupewa akaniambia njoo usimamie kitengo cha parcel then tuone nn cha kufanya. Ila cha ajabu mm ndio nimekuwa Porter. Na kuna nyepesi kwamba analetwa karani kutoka makao makuu DSM. Ila mm nimesoma BBA in Accounting. Ushauri wako ni muhimu.
 
Kitu ambacho hata mm naweza kufanya tena kwa ufanisi mzuri sana.
 
Achana na hiyo kitu,focus na mambo mengine.Kwanza station master hana uwezo wa kuajiri mtu. Tafuta mchongo mwingine
 
Afadhali wewe, mwenzako alipewa kazi ya kufagia stoo tena kwa kujitolea huku ana degree yake ya GPA ya 4.3. Wengine wanaomba kujitolea na degree zao lakini hawapewi hata huko kujitolea.
Wewe komaa mvumilivu hula mbivu
 
Usikate tamaa kijana, everyone has a pain story to tell, hebu andika email yako hapa na email yako
 
[emoji23][emoji23]
 
Kuna maeneo ya kujitolea mkuu sio kwenye mizigo hasa kweny mashirika ya serikali ambao ajira zao zinapitia utumishi itakuchukua muda sana. Ila mvumilivu hula mbivu tengeneza channel ya kujua upitie wapi ili ufike pahusika
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…