Wanangu na nyie mtazaa tu

Mzazi haupaswi kutoa kauli yeyeto negative kwa mwanao hata iwe amekutenda vipi,watamkie baraka TU maana kauli zinaumba.
Mungu alipomaliza uumbaji akamuachia mwanadamu.
Ndo maana tunaumba vitu,maisha yetu kupitia kauli zetu.
Maisha unayoyapitia ni matokeo ya ulimi wako au wa watu
 
Pole sana mwamba hapa Kuna jirani yangu watoto wake wawili wa kiume wametushia kumfanyia kitu kibaya baada ya huyo jirani kuwa mtata na kumchapa mmojawapo wa hao vijana wake wawili kisa ni kwamba dogo alipeleka grender kwenye ofisi ya kuchomea Ili fundi aitumie matokeo yake fundi akaenda kunywa chai akamuachia dogo ofisi dogo nae akasepa ofisi ikabaki bila mtu na Iko wazi , huyo jirani akazinguana na fundi Kwa Nini kaacha ofisi bila mtu , fundi akawaka na akasema amlaumu mwanae maanda ndio kamuachia ofisi na alitakiwa kupaka rangi baadhi ya magril Sasa huyo jirani akamwendea dogo na KUMPA kichapo , dogo kasusa na kumwambia dingi yake kwamba hatokaa akanyage kwenye ile ofisi , Mzee akafikiri utani asubuhi yake jirani kamuamsha mwanae huyo aende akafungue ofisi Kuna fundi anakuja kufanya KAZI dogo akagoma kabisa na kumuwekea ugumu babake, baba alivyotishia kumchapa dogo akadinda na kudai akidhubutu kurusha ngumi dogo nae atarudisha na atamfanyia kitu kibaya ikiwemo kumfikisha kwenye vyombo vya dola, dogo YUPO form four, jirani alipagawa akafikia hatua ya kufungashia virago vyake mwanae nje atafute pa kwenda, haya yote yanafanyika mke wa jirani alikuwa kanisani, basi jirani akanifuata nimpe ushauri juu ya huyo mtoto wake maana mtoto alifikia hatua ya kumwambia baba yake kwamba hapa ni Kwa mama yake kama kuondoka aondoke yeye ( jirani)
Baada ya kwenda kuutuliza msala na kutoa ushauri dogo akaendelea kukaza Yaani anataka baba ndie amuombe msamaha mtoto, nikamshauri jirani amuache amalize shule halafu akishaingia kitaa akajitegemee Kwa Sasa amuache kama alivyo ,
Hawa watoto wa kizazi hiki ni balaa tupu
 
Nakuelewa mkuu.
 
Nyie kwann sasa mlishusha mkungu wote wa ndizi si mngechukua hata kichana kimoja au viwili kupoza njaa tu halafu mnakwenda kuomba msosi kwa jurani.
 
Utadhani Aki na Ukwa.
 
Kuna mtu alitupa kisa chake humu humu JF kuwa miaka wakiwa wadogo maza yao alikuwa anagombana sana na dingi yao ika sababu ya utoto na watoto huwa wanakuwa karibu sana na mama zao basi wao ilikuwa ni kulia na mama yao wakiamini baba mbaya.

Umri ulipokwenda madogo wakiwa sekondari form one na mdogo darasa la tano, kuna siku maza yao aliwasha moto kisa mzee kulala nje, ilikuwa usiku madogo wakamshikia baba yao kisu. Mzee alitokwa hadi na machozi akawaambia yaani mnanishikia kisu mimi, na ni baba yenu, mnajua mama yenu anataka nini kwangu?

Mzee akatoka usiku ule ule akaondoka nasikia hakurudi tena tokea lile tukio litokee.

Hawa madogo wakaendelea ishi na mama yao pekee bila dingi hadi kuwa watu wazima na kuanza kujitegemea.

Mwenyezi MUNGU sasa asivyo na masihara, huyu mkubwa akaja kuoa mwanamke ana mdomo kama mama yake.

Kijana akavumilia sana ila baadae yule mwanamke na tabia zake akaanza kumtesa kisaikolojia maana ikawa si kawaida. Kijana akajikuta anamtafuta baba yake popote alipo, akaja kukuta mzee wao alishafariki na alizikwa kitambo. Jamaa alilia sana kwenye kaburi la baba yake, akatamka maneno yote ya kuomba msamaha. Akasema amekua sasa anaelewa kwann baba hakuwa na amani na anajutia siku alimshikia kisu angejua angetulia tu siku ile.
 
hadithi za abunuwasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…