Wanandoa jihadharini na kosa hili katika mahusiano.

My daughter hiyo avatar,ni busu au msunyo???sijakuelewa kabisa.............lol

We nae huna dogo acha kusoma between lines na kuangalia kila kitu aaahhhh mambo mengine si ya kuchana live!!! Unauchuna kiutu uzima
 
Maisha ya ndoa au mahusiano kwa ujumla ili yawe na maana ni lazima kuzingatia mambo kadha wa kadha. Nimekutana na watu wengi ambao kwa namna moja au vinginevyo, ndoa zao zina shida au kwa kiswahili cha mitaani niseme hazijatulia. Kuna sababu nyingi ambazo inaeleweka wazi kuwa ni vyanzo vya migogoro, kila mtu mwenye shida hiyo kama ukimuuliza atakwembia chanzo cha mtikisiko katika ndoa yake. Moja ya sababau hizo ni kukosekana kwa uaminifu, wivu/ kutiliana mashaka kati ya wanandoa, kutotimiza wajibu katika ndoa n.k. Ila kuna jambo muhimu ambalo ni tatizo kubwa kwa mahusiano ya aina yeyote ambayo nimeona ni vema tukumbushane.

Migogoro au dalili za kutokuelewana zinapojitokeza kwenye mahusiano iwe ni wanandoa au marafiki/wapenzi, tahadhari kubwa iwekwe kwenye maneno au kauli ambazo wanaweza kuzitamka wakati wameghadhibishwa na tatizo lililojitokeza. Kuna maneno ambayo hayafutiki moyoni hata uombe radhi kwa namna gani, ni maneno ambayo mtu alielipokea neno hilo huwa likimsumbua wakati wote pengine mpaka mwisho wa maisha yake. Fikiria mtu kama mke/mpenzi wako atakuambu Mwanamke/mwaname gani wewe! Au neno kama "sijui nimeponzwa na nini!" au neno kama "wakiitwa wanaume/ wanawake na wewe utajitokeza?" neno kama "Malaya wewe" n.k hii ni mifano michache, ila lugha ya kebehi na dharau inapoelekezwa kwa wapenzi ujue hudhoofisha sana uhusiano na ujue wazi kuwa neno lako ulilokwisha litamka halitafutika moyoni mwa mwathirika na kamwe litakuwa likimsumbua. Neno lako hilo litakuwa kichocheo muhimu cha kuibua migogoro siku hadi siku hata baada ya miaka kadhaa ya maelewano. Nikichocheo ambacho huweza kukumbushia yaliyopita hivyo kufanya maelewano yawe hafifu hasa ukizingatia kama neno hilo linaukweli au ni neno linalomvunjia mtu heshima katika jamii. Fikiria kama mume/mpenzi wako atakuambia "wachawi wakubwa nyie" nafikiri maneno ya aina hiyo sio rahisi kufutika kwani yanamtizamo mbaya sana katika jamii.

Hivyo basi wanandoa/wapenzi hata marafiki mjihadhari sana kutamka maneno ya kuumiza wapenzi wenu na mengine yanayofanana na hayo ili kujenga mshikamano, upendo pamoja na maelewano katika maisha yenu ya mahusiano. Nakiri wazi kuwa kuna kughadhibishwa ambako kwa hali ya kawaida kusingevumiliwa na ingehitajika kutoa tamko ambalo pengine lingesaidia kumkomesha mpenzi wako ila nataka nikuhakikishie kuwa silaha kubwa ni 'kukaa kimya bila kuonyesha dharau'' Silaha hii ni muhimu sana katika mambo mengi na ukiitumia nakuhakikishia utashinda. Hakuna ushuhuda wowote ambao umewahi kutolewa kuwa lugha ya kuudhi na dharau au lugha inayomvunjia heshima na utu wa mtu mwingine kama wapenzi n.k imeshawahi kusaidia kujenga mahusiano. Kinyume chake maneno hayo ni silaha ya hatari ambayo yakitamkwa hata kwa sekunde moja huweza kusambaratisha hata uhusiano uliodumu kwa mika 80. Hivyo chunga sana kauli zako kutokuelewana kunapoibuka katika mahusiano n.k.

Anold mambo ya kugonga pentagon nayo sometimes si poa sana mpaka naona aibu kuingalia screen ya laptop aahhikkk ha ha haha haya bwana kila la heri UMEONGEA UKWELI MTUPU
 
Maisha ya ndoa au mahusiano kwa ujumla ili yawe na maana ni lazima kuzingatia mambo kadha wa kadha. Nimekutana na watu wengi ambao kwa namna moja au vinginevyo, ndoa zao zina shida au kwa kiswahili cha mitaani niseme hazijatulia. Kuna sababu nyingi ambazo inaeleweka wazi kuwa ni vyanzo vya migogoro, kila mtu mwenye shida hiyo kama ukimuuliza atakwembia chanzo cha mtikisiko katika ndoa yake. Moja ya sababau hizo ni kukosekana kwa uaminifu, wivu/ kutiliana mashaka kati ya wanandoa, kutotimiza wajibu katika ndoa n.k. Ila kuna jambo muhimu ambalo ni tatizo kubwa kwa mahusiano ya aina yeyote ambayo nimeona ni vema tukumbushane.

Migogoro au dalili za kutokuelewana zinapojitokeza kwenye mahusiano iwe ni wanandoa au marafiki/wapenzi, tahadhari kubwa iwekwe kwenye maneno au kauli ambazo wanaweza kuzitamka wakati wameghadhibishwa na tatizo lililojitokeza. Kuna maneno ambayo hayafutiki moyoni hata uombe radhi kwa namna gani, ni maneno ambayo mtu alielipokea neno hilo huwa likimsumbua wakati wote pengine mpaka mwisho wa maisha yake. Fikiria mtu kama mke/mpenzi wako atakuambu Mwanamke/mwaname gani wewe! Au neno kama “sijui nimeponzwa na nini!” au neno kama “wakiitwa wanaume/ wanawake na wewe utajitokeza?” neno kama “Malaya wewe” n.k hii ni mifano michache, ila lugha ya kebehi na dharau inapoelekezwa kwa wapenzi ujue hudhoofisha sana uhusiano na ujue wazi kuwa neno lako ulilokwisha litamka halitafutika moyoni mwa mwathirika na kamwe litakuwa likimsumbua. Neno lako hilo litakuwa kichocheo muhimu cha kuibua migogoro siku hadi siku hata baada ya miaka kadhaa ya maelewano. Nikichocheo ambacho huweza kukumbushia yaliyopita hivyo kufanya maelewano yawe hafifu hasa ukizingatia kama neno hilo linaukweli au ni neno linalomvunjia mtu heshima katika jamii. Fikiria kama mume/mpenzi wako atakuambia “wachawi wakubwa nyie” nafikiri maneno ya aina hiyo sio rahisi kufutika kwani yanamtizamo mbaya sana katika jamii.

Hivyo basi wanandoa/wapenzi hata marafiki mjihadhari sana kutamka maneno ya kuumiza wapenzi wenu na mengine yanayofanana na hayo ili kujenga mshikamano, upendo pamoja na maelewano katika maisha yenu ya mahusiano. Nakiri wazi kuwa kuna kughadhibishwa ambako kwa hali ya kawaida kusingevumiliwa na ingehitajika kutoa tamko ambalo pengine lingesaidia kumkomesha mpenzi wako ila nataka nikuhakikishie kuwa silaha kubwa ni ‘kukaa kimya bila kuonyesha dharau’’ Silaha hii ni muhimu sana katika mambo mengi na ukiitumia nakuhakikishia utashinda. Hakuna ushuhuda wowote ambao umewahi kutolewa kuwa lugha ya kuudhi na dharau au lugha inayomvunjia heshima na utu wa mtu mwingine kama wapenzi n.k imeshawahi kusaidia kujenga mahusiano. Kinyume chake maneno hayo ni silaha ya hatari ambayo yakitamkwa hata kwa sekunde moja huweza kusambaratisha hata uhusiano uliodumu kwa mika 80. Hivyo chunga sana kauli zako kutokuelewana kunapoibuka katika mahusiano n.k.

Great Thinker,,thanks tena
 
Back
Top Bottom