Wananchi waziba njia kusimamisha Mabasi ya UDART leo asubuhi

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,206
18,548
Nimepita maeneo ya kona Kimara na kukuta abiria wametanda barabarani kwenye njia za mwendo kasi.

Baada ya kuulizia ni kwamba toka asubuhi ya saa 11 asubuhi wapo kituoni na mabasi yote yanayo toka kimara na yanayo kwenda kimara hayakusimama kwenye kituo hicho na hapo ilikua ni saa 12 asubuhi kasoro ina maana iuna watu wamekaa zaidi ya dk 40 kituoni bila kusafiri.

Na kituooni hapo palikua giza hakuna umeme. Hivyo abiria baada ya kuona wanapuuzwa wakatoka ndani ya kituo na wakasimama katikati ya barabara ya mabasi yanayo kwenda kimara ili basi lolote litakalo pita lisimame wageuze nalo maana yale yanayo toka kimara yanakuja huku yakiwa yamejaa.

Juhudi zao zimezaa matunda baada ya mabasi kupita ikabidi yasimame kwa amri ya hao abiria, wakapanda kwenda kimara na kisha kugeuza nayo tena hadi kivukoni.

Baada ya kufuatilia kumbe vituo vyote vilikua vimejaa abiria wengi sana wanao subiri usafiri .

Nasikia hii ni mara ya pili abiria kuziba njia ili kupata huu usafiri wa udart.


Walio kuwepo wanaweza kutupa taarifa zaidi

Hizi ni dalili mbaya, UDART jipangeni.
 
Madereva hawana cha kupoteza ujue,wao pesa yao iko palepale, nadhan UDART wanapaswa kuhakikisha asbuh kuna mabas mengi sana walau hadi saa 4 asbuhi,maana KIMARA kuna watu wengi sana na ndio maana mradi umeanzia huko kwanza
Ila tukio la leo limenishtua, wasilichukulie poa, wananchi wameanza kuwa na hasira na haka kausafiri kutokana na uzembe wao usio na maana
 
Hii habari ni ya lini? Naona muda iliyo postiwa na masaa yanayoongelewa ni nyotanyota tu kwangu, labda ni hii hangover ya Valeur inanizingua, ngoja nikajitoe lock labda nikirudi ntaielewa.
 
Binafs huwa natumia MWENDOKASI ila si mida ya asbuh sana wala jioni sana,huwa nawaona wananchi pale Korogwe wamejaa sana asbuh wakisubiri mabasi,lakini pia hata Kimara Mwisho asbuhi kuna watu wengi mnooooo,sijui shida ni nini?
 
Hii habari ni ya lini? Naona muda iliyo postiwa na masaa yanayoongelewa ni nyotanyota tu kwangu, labda ni hii hangover ya Valeur inanizingua, ngoja nikajitoe lock labda nikirudi ntaielewa.
Rudia kusoma mkuu.. ni leo saa 11 asubuhi
 
Back
Top Bottom